Chanzo halisi cha mbwa (Origin of dogs)

Chanzo halisi cha mbwa (Origin of dogs)

Bonobo!

Canis Lupus Familiaris ndiyo jina la hii specie tunayoijua na kuipenda..Almaaruf kama Mbwa!!

Wengi mkiulizwa mbwa wametokea wapi kwa haraka haraka mtasema waliumbwa na Mungu.

Lakini kama maswali mengi kwenye hii dunia, majibu yake huwa sio rahisi kihivyo. Leo tuingie deep zaidi ya hapo tujue hawa mbwa wametokea wapi hasa. Chukua popcorn kabisa, it's history time.

Miaka laki 2 iliyopita, binadamu (Homo sapiens) alianza kuwepo huko Africa,(unaweza kufuatilia pia Chanzo halisi cha binadamu (Origins of mankind))

Miaka laki 1 mpaka 50,000 iliyopita hawa binadamu wa kale wakaamua kuondoka Africa na kwenda Ulaya na Asia kutafuta maisha bora.

Kwakuwa kipindi hiko binadamu kazi kuu waliyokuwa wanaifanya ilikuwa kuwinda na kukusanya matunda (Hawakuwa na kazi kama madaktari, Mainjinia, Wanamziki na maslay queens)

Walipofika Asia (hasahasa Siberia) walikutana na adui mkubwa sana ambaye aliwakwamisha katika kazi yao kuu ya uwindaji..Naye si mwingine bali ni..........(drumroll please🥁).........Canis Lupus (Grey wolf) kwa kizaramo anaitwa Mbwa mwitu

View attachment 2469009

Hawa wanyama waliwasumbua sana watu. na pia, watu waliwasumbua sana hawa mbwa mwitu..Tuwaite Wolves.

Hawa wolves waliwachukia sana binadamu maana walileta competition kwenye kutafuta chakula. Wolves waliona Hawa viumbe wapya waliokuja huku Siberia walikuwa wanauwezo mkubwa sana wa kuwinda kwa kuweka mitego na kushirikiana kwa hali ya juu kuliko wao mbwa mwitu(Wolves).

Kwa msiojua, mbwa mwitu pia huwa wanawinda kwa kushirikiana na kutengeneza plan za kumshambulia/kumvizia au kumkibiza adui mpaka achoke. ni ngumu sana kwa Mbwa mwitu kuwinda peke yake.

Wale mbwa mwitu waliofukuzwa kwenye ukoo (Packs) kutokan na tabia zao mbovu walikuwa wanaishi kwa kuwinda vimnyama vidogovidogo. Lakini kutokana na ujio wa huyu kiumbe mpya (binadamu), competition ya chakula ikawa kubwa, hata hawa wanyama wadogo wadogo ikawa ngumu kupatikana tena.

Wale mbwa mwitu waliofukuzwa na ukoo wakawa wanapata tabu kupata chakula, wakawa wanaishi kwa kutafuta makombo. Kwakuwa Binadamu walikuwa wanaishi kwenye makambi na wanakula nyama na kutupa mifupa (since hawana meno makali ya kutafuna mifupa.)

Hawa mbwa mwitu wasio na packs wakawa wanawavizia binadamu wakitupa makombo wao wanakula. Na hapo ndo ikawa mwanzo wa interaction kati ya binadamu na wolves.

katika wale wolves waliokuwa wanakuja kutafuta makombo, Binadamu wakawa wanachagua wale wasio tishio kwao (wapole, wenye miili midogo, watiifu) na wakagundua kuwa wanaweza kuwatumia kwa faida yao.

Wakaanza kugundua kuwa hawa wolves wanaweza kutumiwa kama walinzi akija Adui wanawahi kumsikia, kwahyo binadamu akaamua kuwa anakaa na hawa wolves ili apate kuzitumia faida zake, with time wakaanza kugundua faida nyingi za hawa wolves ikiwemo kunusa mbali na hata kujua wapi kuna wanyama wa kuwinda, Kupambana na dubu na wanyama wengine wakali, kuchunga mifugo nk.

Watu wakaanza kuwa wanachukua wale wolves wenye tabia na sifa wanazotaka na kuanza kuwabreed wao kwa wao. Hiki kitendo cha kuchagua mbegu za kufuga/kulima zenye sifa unazotaka na kuzitenga ili kupata matokeo unayotaka inaitwa Artificial selection.

Kwa hiyo kati ya miaka 30,000-23,000 iliyopita.. watu walikuwa wanachukua wolves na kuchagua sifa wanazopenda.

Watoto wakizaliwa na hizo sifa zinazotafutwa (Za kimbwa) ndiyo wanafugwa na kuwa bred tena na tena... Hivyo wolves wakawa wanabadilika, na wakibadilika wanachukuliwa tena wale wenye sifa zinazotafutwa mpaka tukafikia kupata mnyama anayeitwa leo Mbwa.

Lakini hizi breed tofauti tofauti za mbwa tunazojua leo zimetengenezwa less than miaka 400 iliyopita.
Hiyo hiyo formula ya artificial selection watu waliitumia (Na bado wanaendelea kuitumia) kutengeneza breed tofuti za mbwa wenye sifa tofauti wanazozitaka.

Unataka mbwa mwenye mbio? Chukua wale wenye miguu mirefu uwabreed wao kwa wao na watoto watakaozaliwa unawachagua wale wenye mbio tu na kuwafuga.View attachment 2469039
Unataka mbwa mwenye nguvu?? Tafuta wenye sifa hizo na kuwabreed pamoja na watoto wasio na nguvu unawatupa pembeni. Unaendelea na wale wenye nguvuView attachment 2469040
Je, untaka mbwa wa kukaa naye na kumchezea?View attachment 2469041
Ukitaka mbwa mwenye sifa mbili labda Awe na nguvu na Manyoya mengi, Unachukua mbwa wawili wenye sifa Hizo na kuwabreed pamoja huku ukichukua wale watoto wenye sifa unazotaka na kuwabreed hao tu.View attachment 2469044
Mpaka leo mbwa na Wolves wanaweza kuzaa pamoja lakini yule mtoto hawezi kuzaa.
Ule mstari unaowaunganisha kama specie moja umeshakatika.

Ipo siku mstari unaowaunganisha German shepherd na Bulldog unaweza kukatika vikaonekana kama viumbe viwili tofauti..

Hii artificial selection haijatuletea Mbwa tu, imetuletea pia Ndizi, Matikiti, Maparachichi, Kuku wa kisasa, Ng'ombe wa kisasa Nk. Nk.
Ni kawaida ya binadamu wakitafuta majibu ya maswali magumu yalio mbele yao wakikosa hutengeneza story za kujibu matamanio yao so hongera kwa stor nzur boss.
 
Hizi sio stories. Hizi ni gunduzi zilizobase kwenye ushahidi wa archeology, genetics,anatomy,molecular biology,biogeography,embryology nk.
Hakuna theory yenye evidence nyingi kutoka field mbalimbali za sayansi kama evolution.

Kwahyo unapoishia kusema ni story tu hautendei haki kazi ya maelfu ya wanasayansi na researchers waliofanya kazi kubwa field mpaka kufikia hii knowledge tuliyonayo hapa.

Lakini pia uzuri wa sayansi sio Sheria au dini kwamba unatakiwa uifuate bila maswali. Sayansi Inabadilika kuufuata ushahidi unapoelekea. Hivyo kama unapinga makala hii au una ushahidi wa facts mbadala wa hizi unaweza kushare pia hapa tuchambue.
Asante.
 
Yes, Basenji ni mbwa zamani sana, hata inawezekana ndiyo mbwa breed ya zamani kuliko mbwa wote waliopo duniani sasaivi.
Lakini haimaanishi Basenji ndiye mbwa wa kwanza kuwepo duniani.
Mbwa aina ya Basenji ni wa juzi tu, almost Miaka 8000 iliyopita, na yes walianzia kuwepo Africa.

Lakini ukumbuke mbwa wameanza kuwepo duniani huko Asia miaka karibia 30,000 iliyopita.
Kwahyo kulikuwa na Breed ambazo sio Basenji zilizoanzia Asia na Ulaya, na watu walizifuga. Ukumbuke pia kipindi kile (mpaka leo) binadamu wanamove sana from place to place, continent to continet...Kipindi cha kuanzia miaka 30,000 mpaka 8000 walisafiri kutoka Asia nakufika Africa wakiwa na mbwa wao, vivo hivo jamii za kiafrica (Kuanzia North Africa kama Egypt iliyoungana na Asia) zilipochangamana na za Asia, zikaiga na zikaanza kufuga hao mbwa na mwishowe ikafika Mpaka DRC ambapo breed ya Basenji ilipoanzia.

Kwahyo hiyo michoro Huko kondoa ni ya Less than 8000 years Ago, ambapo Basenji alievolve hapa East Africa.
Before walifika mbwa ambao ni Basenji-like (yaani breed ambayo ni baba ao basenji) lakini hao baba zao walikufa na kwenda extint.
Breed nyingi za mbwa duniani hazina zaidi ya miaka 400 iliyopita.

Basenji-like dogs in Egyptian drawingsView attachment 2472216
This can be proven by genetic evidence ambapo Basenji ana DNA inayofanana na Dingo wa Australia kuliko inavyoendana na Fisi wa East Africa.
So it means, Origin ya mbwa wote ni Asia ila walisplit kwa muda, Wengine wakaja kuwa Basenjis in Africa, wengine dingos in Australia.
Dah mkuu unatema nondo kama profesa
 
Ooh basi muoneshe hata sasaivi.
Kuna dogo mmoja nishakutana naye swimmingpool moja morogoro
Dogo alikuwa darasa la tano lakini alikuwa ananiuliza maswali ambayo najua hata professa wa kibongo anaweza kushindwa kujibu.

Nikamuuliza anajuaje yote haya? Akaniambia nyumbani kwao kuna maktaba na ni utamaduni wao kusoma vitabu vingi
 
Bonobo!

Canis Lupus Familiaris ndiyo jina la hii specie tunayoijua na kuipenda..Almaaruf kama Mbwa!!

Wengi mkiulizwa mbwa wametokea wapi kwa haraka haraka mtasema waliumbwa na Mungu.

Lakini kama maswali mengi kwenye hii dunia, majibu yake huwa sio rahisi kihivyo. Leo tuingie deep zaidi ya hapo tujue hawa mbwa wametokea wapi hasa. Chukua popcorn kabisa, it's history time.

Miaka laki 2 iliyopita, binadamu (Homo sapiens) alianza kuwepo huko Africa,(unaweza kufuatilia pia Chanzo halisi cha binadamu (Origins of mankind))

Miaka laki 1 mpaka 50,000 iliyopita hawa binadamu wa kale wakaamua kuondoka Africa na kwenda Ulaya na Asia kutafuta maisha bora.

Kwakuwa kipindi hiko binadamu kazi kuu waliyokuwa wanaifanya ilikuwa kuwinda na kukusanya matunda (Hawakuwa na kazi kama madaktari, Mainjinia, Wanamziki na maslay queens)

Walipofika Asia (hasahasa Siberia) walikutana na adui mkubwa sana ambaye aliwakwamisha katika kazi yao kuu ya uwindaji..Naye si mwingine bali ni..........(drumroll please[emoji1623]).........Canis Lupus (Grey wolf) kwa kizaramo anaitwa Mbwa mwitu

View attachment 2469009

Hawa wanyama waliwasumbua sana watu. na pia, watu waliwasumbua sana hawa mbwa mwitu..Tuwaite Wolves.

Hawa wolves waliwachukia sana binadamu maana walileta competition kwenye kutafuta chakula. Wolves waliona Hawa viumbe wapya waliokuja huku Siberia walikuwa wanauwezo mkubwa sana wa kuwinda kwa kuweka mitego na kushirikiana kwa hali ya juu kuliko wao mbwa mwitu(Wolves).

Kwa msiojua, mbwa mwitu pia huwa wanawinda kwa kushirikiana na kutengeneza plan za kumshambulia/kumvizia au kumkibiza adui mpaka achoke. ni ngumu sana kwa Mbwa mwitu kuwinda peke yake.

Wale mbwa mwitu waliofukuzwa kwenye ukoo (Packs) kutokan na tabia zao mbovu walikuwa wanaishi kwa kuwinda vimnyama vidogovidogo. Lakini kutokana na ujio wa huyu kiumbe mpya (binadamu), competition ya chakula ikawa kubwa, hata hawa wanyama wadogo wadogo ikawa ngumu kupatikana tena.

Wale mbwa mwitu waliofukuzwa na ukoo wakawa wanapata tabu kupata chakula, wakawa wanaishi kwa kutafuta makombo. Kwakuwa Binadamu walikuwa wanaishi kwenye makambi na wanakula nyama na kutupa mifupa (since hawana meno makali ya kutafuna mifupa.)

Hawa mbwa mwitu wasio na packs wakawa wanawavizia binadamu wakitupa makombo wao wanakula. Na hapo ndo ikawa mwanzo wa interaction kati ya binadamu na wolves.

katika wale wolves waliokuwa wanakuja kutafuta makombo, Binadamu wakawa wanachagua wale wasio tishio kwao (wapole, wenye miili midogo, watiifu) na wakagundua kuwa wanaweza kuwatumia kwa faida yao.

Wakaanza kugundua kuwa hawa wolves wanaweza kutumiwa kama walinzi akija Adui wanawahi kumsikia, kwahyo binadamu akaamua kuwa anakaa na hawa wolves ili apate kuzitumia faida zake, with time wakaanza kugundua faida nyingi za hawa wolves ikiwemo kunusa mbali na hata kujua wapi kuna wanyama wa kuwinda, Kupambana na dubu na wanyama wengine wakali, kuchunga mifugo nk.

Watu wakaanza kuwa wanachukua wale wolves wenye tabia na sifa wanazotaka na kuanza kuwabreed wao kwa wao. Hiki kitendo cha kuchagua mbegu za kufuga/kulima zenye sifa unazotaka na kuzitenga ili kupata matokeo unayotaka inaitwa Artificial selection.

Kwa hiyo kati ya miaka 30,000-23,000 iliyopita.. watu walikuwa wanachukua wolves na kuchagua sifa wanazopenda.

Watoto wakizaliwa na hizo sifa zinazotafutwa (Za kimbwa) ndiyo wanafugwa na kuwa bred tena na tena... Hivyo wolves wakawa wanabadilika, na wakibadilika wanachukuliwa tena wale wenye sifa zinazotafutwa mpaka tukafikia kupata mnyama anayeitwa leo Mbwa.

Lakini hizi breed tofauti tofauti za mbwa tunazojua leo zimetengenezwa less than miaka 400 iliyopita.
Hiyo hiyo formula ya artificial selection watu waliitumia (Na bado wanaendelea kuitumia) kutengeneza breed tofuti za mbwa wenye sifa tofauti wanazozitaka.

Unataka mbwa mwenye mbio? Chukua wale wenye miguu mirefu uwabreed wao kwa wao na watoto watakaozaliwa unawachagua wale wenye mbio tu na kuwafuga.View attachment 2469039
Unataka mbwa mwenye nguvu?? Tafuta wenye sifa hizo na kuwabreed pamoja na watoto wasio na nguvu unawatupa pembeni. Unaendelea na wale wenye nguvuView attachment 2469040
Je, untaka mbwa wa kukaa naye na kumchezea?View attachment 2469041
Ukitaka mbwa mwenye sifa mbili labda Awe na nguvu na Manyoya mengi, Unachukua mbwa wawili wenye sifa Hizo na kuwabreed pamoja huku ukichukua wale watoto wenye sifa unazotaka na kuwabreed hao tu.View attachment 2469044
Mpaka leo mbwa na Wolves wanaweza kuzaa pamoja lakini yule mtoto hawezi kuzaa.
Ule mstari unaowaunganisha kama specie moja umeshakatika.

Ipo siku mstari unaowaunganisha German shepherd na Bulldog unaweza kukatika vikaonekana kama viumbe viwili tofauti..

Hii artificial selection haijatuletea Mbwa tu, imetuletea pia Ndizi, Matikiti, Maparachichi, Kuku wa kisasa, Ng'ombe wa kisasa Nk. Nk.
Ndio hizo GMO
 
Ni nje kidogo ya mada, maana hapa tunaongelea mbwa., nilitaka tujikite kwenye mbwa.

*ila kwa kifupi wolves walitokana na miacids,(from Miacidae family)... hawa miacids na wao walitokana na insectivores wadogo kutoka kipindi cha cretaceous era.(enzi za Dinasours hizo, around 60 million years ago)

Hawa Miacids wameshapotea kwenye uso wa dunia, lakini walikuwa na maumbo tofauti tofauti makubwa kwa madogo, walievolve kutoka kuwa insectivores(wala wadudu) na kudevelop traits zilizowafanya kuwa carnivores(wala nyama) kama Makucha, meno nk.
wajukuu zao ni wengi kama canids (Wolves,dogs, Foxes, Vivverids, Genets (wa Afrika),coyotes, Jackals etc.), View attachment 2469237 Na pia felines kama Paka, Chui, simba pia walitokana na miacis(Genus ndani ya family ya miacidae)View attachment 2469236...Hawa miacids ndio babu wa carnivores wote wa ardhini.View attachment 2469235
Kulikua na wanyama wa hatari sana!
 
Its intresting, Hawa Aurochs ndio kiumbe wa kwanza tuliyempoteza na kurekodi.(Tushapoteza wengi nyuma bila kurekodi)

Julius ceasar 53BC aliandika kuwa hawa Aurochs wapo ujerumani huko na wajerumani walikuwa wanawakamata kwenye mashimo na kutumia mapembe yao kama vikombe vya kunywea.

Binadamu ndio waliopelekea hawa Aurochs kupotea kwenye uso wa dunia kupitia shughuli kama ufugaji, kuna report moja ya 1564 inasema kuwa hawa Auroch hawazaliani vizuri kwakuwa binadamu walipokuwa wanapeleka ng'ombe zao malishoni walipunguza maeneo ya hawa Aurochs kuwa wanaishi na kula, Aurochs wakawa wanakosa mahala pa kukaa na pia wakawa wanawindwa sana.
Kuna Document ilionesha kuwa by 1599 kulikuwa na Auroch 24 tu waliobaki duniani, na majangili wakawa wanaona ukiwa na Pembe lake ni dili kubwa (Kama ilivyo sasa kwa Vifaru).
By 1620 Dume la mwisho likafa...Na lile jike lililobaki la mwisho liliwindwa na kuuliwa 1627.

It is sad, lakini Binadamu tumechangia na tunaendelea kuchangia kupoteza viumbe wengi hapa dunianj kupitia shughuli zetu kama deforestation, pollution nk.

All in all wanyama waliowahi kuishi duniani wakafa na kupotea ni wengi mara 99 kuliko wanyama tuliopo sasaivi.
Yani asilimia 99% ya wanyama wote waliowahi kuwepo duniani wameshapotea.
Noma
 
Hizi sio stories. Hizi ni gunduzi zilizobase kwenye ushahidi wa archeology, genetics,anatomy,molecular biology,biogeography,embryology nk.
Hakuna theory yenye evidence nyingi kutoka field mbalimbali za sayansi kama evolution.

Kwahyo unapoishia kusema ni story tu hautendei haki kazi ya maelfu ya wanasayansi na researchers waliofanya kazi kubwa field mpaka kufikia hii knowledge tuliyonayo hapa.

Lakini pia uzuri wa sayansi sio Sheria au dini kwamba unatakiwa uifuate bila maswali. Sayansi Inabadilika kuufuata ushahidi unapoelekea. Hivyo kama unapinga makala hii au una ushahidi wa facts mbadala wa hizi unaweza kushare pia hapa tuchambue.
Asante.
Sawa kaka hata binadamu alikuwa nyani wakati fulan kutokana na tafiti mbalimbali.
 
Binadamu hakuwa nyani,ila binadamu na nyani walitoka kwenye kiumbe mmoja
 
Its intresting, Hawa Aurochs ndio kiumbe wa kwanza tuliyempoteza na kurekodi.(Tushapoteza wengi nyuma bila kurekodi)

Julius ceasar 53BC aliandika kuwa hawa Aurochs wapo ujerumani huko na wajerumani walikuwa wanawakamata kwenye mashimo na kutumia mapembe yao kama vikombe vya kunywea.

Binadamu ndio waliopelekea hawa Aurochs kupotea kwenye uso wa dunia kupitia shughuli kama ufugaji, kuna report moja ya 1564 inasema kuwa hawa Auroch hawazaliani vizuri kwakuwa binadamu walipokuwa wanapeleka ng'ombe zao malishoni walipunguza maeneo ya hawa Aurochs kuwa wanaishi na kula, Aurochs wakawa wanakosa mahala pa kukaa na pia wakawa wanawindwa sana.
Kuna Document ilionesha kuwa by 1599 kulikuwa na Auroch 24 tu waliobaki duniani, na majangili wakawa wanaona ukiwa na Pembe lake ni dili kubwa (Kama ilivyo sasa kwa Vifaru).
By 1620 Dume la mwisho likafa...Na lile jike lililobaki la mwisho liliwindwa na kuuliwa 1627.

It is sad, lakini Binadamu tumechangia na tunaendelea kuchangia kupoteza viumbe wengi hapa dunianj kupitia shughuli zetu kama deforestation, pollution nk.

All in all wanyama waliowahi kuishi duniani wakafa na kupotea ni wengi mara 99 kuliko wanyama tuliopo sasaivi.
Yani asilimia 99% ya wanyama wote waliowahi kuwepo duniani wameshapotea.
Huna hata kapicha cha Auroch tajiri?
 
Huna hata kapicha cha Auroch tajiri?
images (15).jpeg
images (16).jpeg
images (14).jpeg
 
Back
Top Bottom