SoC02 Chanzo kipya cha ajira kwa vijana

SoC02 Chanzo kipya cha ajira kwa vijana

Stories of Change - 2022 Competition

JOZEY MAGANGA

New Member
Joined
Aug 28, 2022
Posts
3
Reaction score
0
UTANGULIZI
"Ajira kwa vijana" umekuwa ni wimbo wa Kila siku ambao watu kama wanasiasa na viongozi wengi wa serikali na wasio wa serikali(NGOs) wamekuwa wakiuimba Kila siku na mara nyingine viongozi wa kisiasa wamekuwa wakiuimba kama njia Yao nzuri ya kuwahadaa vijana na wazazi wa vijana hao Ili wapewe wadhifa Fulani wa kimamlaka serikalini na wakishapata mamlaka hayo wimbo huu hauusikii tena au utausikia kwa taaratibu haswa pale vijana wanapokumbusha ufanisi wa utendaji wa wimbo huu!

CHANZO KIPYA NA KIZURI CHA AJIRA KWA VIJANA
Mara nyingi vijana haswa wa kutoka kwenye familia masikini yaani waliosoma na wasiosoma katika nchi nyingi za afrika hususani Tanzania,wanakuwa hawawaelewi viongozi wao wanaposema vijana mjiajiri na muda mwingine huwakashifu vijana wanaohangaika kutafuta kazi za kuajiriwa, Hali hii hupelekea vijana wengi kuwa na migogoro kwa viongozi wao! Serikali inatakiwa kuzingatia vitu hivi hapo chini Ili kuongeza Imani na wigo wa Ajira kwa vijana.

1.Wastaafu wote haswa viongozi wa juu wanatakiwa watumike kujiajiri na kuzalisha ajira zaidi kwa vijana yaani wasiongezewe muda wa majukumu punde wanapostaafu, changamoto kubwa ya vijana kujiajiri ni mtaji hivyo wastaafu wanapostaafu wanakuwa na mafao ya mamilioni ya pesa hivyo pesa hizo watumie kuanzisha viwanda na biashara Ili vijana wapate Ajira Toka kwao na pia wanapostaafu bila kuongezewa muda kutapelekea kijana kukaba nafasi hio! Kitendo cha serikali kuwaongezea muda wastaafu ni kuwadharau vijana.

2.kusiwe na Ajira mara mbili kwa mtumishi mmoja, yaani unakuta mtu ni mwalimu wa chuo Bado anateuliwa kuwa mkurugenzi wa taasisi Fulani yaani anapokea mshahara mara mbili! Kwa kweli inatia aibu kwa serikali na inatia masononeko kwa vijana wenye sifa! Serikali waache kutoa Ajira mara mbili kwa mtu mmoja maana inawaongezea machungu vijana! Iwapo itaacha kufanya hivyo baadhi ya vijana watapata nafasi za Ajira.

HITIMISHO
Serikali inapaswa ijue kuwa vijana wengi hawana dhamana ya kuwezesha kupata mkopo kwahiyo vyanzo viwili hapo juu vitumike!
Viongozi wanapokuwa madarakani miongoni mwao hudharau vijana wanaotafuta Ajira bila kujua chanzo cha mtaji Ili wajiajiri.Hivyo na wao wanapo staafu waje uraiani Ili wathibitishe kile walichokuwa wanaongea walipokuwa madarakani.Nadhani itakuwa ni rahisi na mfano mzuri kwa vijana kwaio wao watakuwa wanamtaji mzuri na WA kutosha uliotokana na kustaafu
 
Upvote 0
Back
Top Bottom