Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Gharama za maisha zimepanda sana, sasa hivi kumudu gharama za mkate asubuhi ili uwe kitafunwa cha kifungua kinywa ni wachache wanamudu.
Hawa watoto wetu wengine hawajazoea kula mihogo ya kuchemsha au viazi vya kuchemsha na chai. Kwa kuwabadilishia tu unaweza kufanya hivi.
Chemsha mihogo mpaka iive, iweke kwenye kinu ikiwa bado ya moto uiponde utapata ugali unaovutana. Ugali huu unaweza kulika na mboga yeyote lakini kama lengo lako ni kutengeneza chapati weka ugali kwenye karai au sinia, weka chumvi, mafuta na hamira na uuache uumuke.
Ukisha umuka kata chapati size unayopenda sukuma kwenye kibao na uoke jikoni.
Chapati hizi huweza kuliwa na mchuzi au maharage kama chakula.