Chaputa national election

Chaputa national election

Socw

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2016
Posts
1,329
Reaction score
2,644
Huu uzi ni maalum kwa ajili ya kufanya uchaguzi wa chama hiki kikongwe hapa nchini. Lengo la kufanya hivi ni baada ya kuona mpasuko wa kichama baada ya kuwa na watu wawili wanaojitangaza kuwa wao ni wenyeviti wa chaputa ngazi ya taifa. Watu hao ni moto wa waji na mwingine sijui ni nani(nimemsahau). Hali hii itahatarisha sana mustakabali wa chama hiki.

Sasa, uzi huu utumike kufanya chaguzi za viongozi wa ngazi ya juu kabisa watakaokuwa watetezi wa maslahi ya chama hiki.

Nafasi zitakazo husika

Mwenyekiti

Makamu mwenyekiti

Katibu mkuu

Katibu saidizi

Mhazini.

Na nguvu aliyopewa mwenyejiti na katiba ya CHAPUTA atateua viongozi wafuatao

Afisa mahusiano wa chaputa

Msajili mkuu wa chaputa

Kamati ya maadili ya chaputa

Wawakilishi wa chaputa wa kila mkoa.

Ni nafasi ya kila mwanachama wa vhaputa kugombea na kujinadi ni kwa namna gani atakiongoza chama hiki kikongwe kabisa.

Karibuni
 
Nimesikitishwa Sana Kupata Taarifa Kama Hizi Kwenye Chama Chetu Pendwa CHAPUTA za Kuwa na mpasuko utakao turudisha nyuma.


Kwanza Kabisa Napenda Kujitambulisha Mwenyekiti Wenu Kvuli Wa CHAPUTA. Japo Kuna Changamoto Nyingi Zinazotaka kuturudisha Nyuma kama hizi za mipasuko.


Hivyo Basi Nachukua Nafasi Hii Kutangaza Nia Na Kugombea Uenyekiti Wa Chama Kubwa CHAPUTA.


Kama Nilivyopambana Kupigania Na Kutetea Vitu Vingi Kwa Maslahi Ya Chama Yetu CHAPUTA.

Na Imani Wanachama Na Member Wote Mtanipa Ridhaa Yenu Na Kuwa Mwenyekiti Bora Kwa Maendeleo Ya CHAPUTA na wanachama Wote.


CHAPUTA CHAMA KUBWA

CHAPUTA HAKUNA VIZINGA

UTAMU NI ULE ULE SWALA NI UTELEZI.


MWENYEKITI AJAE

cc Kichwa Kichafu

Mwenyekiti Kivuli Wa CHAPUTA kwa Sasa
 
Wajumbe/Wagombea wanapswa kuangalia vigezo;

1) Muda wa uwanachama, kwa wanao gombea nafasi za juu kwenye chama. Sio mtu ana kadi ya uwanachama ya mwaka jana tu halafu akimbilie kugombea nyadhifa za juu. Wakati kuna watu toka enzi za mkoloni/Uhuru ni ma member wa CHAPUTA.

2) Kuijua katiba ya chama ipasavyo. (Na kuinadi katiba).

3) Fomu za kugombea ziambatane na CV ya mgombea.

4) Wanachama wa upinzani hawato ruhusiwa kuendelea na nyadhifa zao pindi watakapo amua "kuunga mkono juhudi za mwenyekiti wetu".

4) Kuzingatia maadili/miiko ya chama.

5) Atakae gundulika ni mwanachama wa kamati za fitna kwenye kampeni atachukuliwa hatua kali za kisheria.

6) Muda wa kuchukua fomu na muda wa kuanza kampeni.

7) Tume huru ya uchaguzi kuanzishwa.


Nawasilisha hoja,
 
Back
Top Bottom