Charles Maurice de Talleyrand: Mtu aliyeongoza mapinduzi mawili, akawadanganya wafalme 20 na kuanzisha bara Ulaya

Charles Maurice de Talleyrand: Mtu aliyeongoza mapinduzi mawili, akawadanganya wafalme 20 na kuanzisha bara Ulaya

Bravo snr

Senior Member
Joined
Aug 16, 2020
Posts
182
Reaction score
477

Charles Maurice de Talleyrand, mmoja ya watu mashuhuri katika shitoria ya ufaransa na Ulaya

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Charles Maurice de Talleyrand, mmoja ya watu mashuhuri katika shitoria ya ufaransa na Ulaya
Mwanamfalme wa Benevento na Dola, Mwanamfalme wa Talleyrand na Périgord, Duke wa Dino, Muhasibu wa Périgord, Rika la Ufaransa, Duke wa Talleyrand na Périgord, Makamu wa Grand Elector Imperial, Mkuu wa Jeshi , shujaa wa agizo la Saint-Esprit, Shujaa wa agizo la Uhispania la ngozi ya Dhahabu, Kamanda Mkuu wa Agizo la Taji la Westphalia ..

Hizi ni miongoni mwa baadhi ya vyeo alivyopatiwa katika maisha yake ya miaka 82 Charles Maurice de Talleyrand, mmoja ya watu ambao takwimu zao zilipendeza na kujadiliwa katika historia ya Ufaransa na Ulaya.
Mwansiasa mwenye uwezo mkuu ambaye alikuwa na ushawishi mkubwa kati ya karne ya 18 na 19 , ambaye aliunga mkono na kuangusha tawala tofauti na ambaye amedaiwa kuwa msaliti aliyedaiwa kubembeleza upande mmoja huku mwengine akiwa na chuki bila kujulikana.
Uwezo wake wa kupewa orodha ndefu ya nyadhfa za heshima ni sawa na utajiri aliokuwa nao , chuki alizovutia na viongozi wengi aliowaongoza na baadaye kuwaachilia hatma yao.
"Aliongoza mapinduzi mawili, akawadanganya wafalme 20 akaidhibiti dunia nzima akamhukumu mwandishi wakati Talleyrand alipofariki mwaka 1838.
''Na huenda idadi hiyo ni ndogo, kwa kuwa wakati wa utawala wa Talleyrands, ni Ujerumani pekee ilikuwa na majimbo huru 300 huku ikiwa na viongozi wengi ijapokuwa hawakuwa wafalme.."
Kati ya falme kuna uwezo mkubwa kwa takwimu hiyo ilikuwa ya juu , anasema mwandishi , muhariri na mkalimani Xavier Roca Ferrer, mwandishi wa wasifu mpya kuhusu muhusika anayemwakilisha kwa jina Talleyrand.
'Shetani' huyo aliyeongoza mapinduzi mawili , aliwadanganya wafalme 20 na kugundua Ulaya.''
Xavier Roca-Ferrer

CHANZO CHA PICHA,IRENE HERNÁNDEZ VELASCO
Maelezo ya picha,
Xavier Roca-Ferrer

Kutoka kuwa Askofu hadi kuwa ''Msaliti"​

Talleyrand, mtu mwenye tamaduni nyingi na mtu bora , alizaliwa katika familia ya Ufaransa 1754.
Alikuwa mwana wa kwanza , lakini kutokana kilema chake , wazazi wake waliamua kwamba hali hiyo ililemaza uwezo wake wa kuwzaa kuwa katika mahusiano mazuri ya ndoa .
Hivyobasi walimwendea mwana wao wa pili na kuamua kwamba ni muhimu asome kazi ya kanisa ambapo atapata usaidizi kutoka kwa mjomba ambaye ni mchungaji.
Na alifanya hivyo: Wakati wa utawala wa Louis XVI alikuwa waziri wa fedha katika kanisa la Ufaransa , wadhfa ambapo ulimpandisha katika kilele cha tasisi hiyo ya kidini na kumfanya kupewa taji la Askofu .
lakini kuwa mchungaji hakukumzuia kuwa na mahusiano mengi na wanawake kadhaa , vilevile haukumzuia kuendelea kucheza kamari mbali na mipango mibaya ya fedha isiohesabika na matukio ya ufisadi.
Ukweli ni kwamba mapenzi ya Talleyrand hayakuwepo katika siasa, masuala ya uchumi, kamare ama wanawake , lakini kuhatarisha Maisha katika sekta zote , ulisema wasifu wake.
Uwezo wa kumiliki taji la Aaskofu ulimhakikishia kupata kiti katika masula ya serikali 1789 na haki ya kuingilia kati katika ujenzi wa Ufaransa mpya.
Na hakupoteza fursa hiyo. Alishirikiana katika kuandika katiba ya kwanza ya Ufaransa , kuhusu haki za binadamu na raia mbali na kujaribu kukuza uongozi wa kifalme Uingereza, na kupendekeza sheria ya elimu ya dunia ilio bila malipo , kitu ambacho miaka mia moja baadaye kiliafikiwa.
Katika bunge la kitaifa , hali mbaya ya kiuchumi ilijadiliwa , Talleyrand alitoa wazo zuri la mtu anayevalia kilemba cha askofu kutaifisha mali yote ya kanisa na baadaye asimamie mali zote .
Pendekezo lake lilifanikiwa , lakini halikupendwa na mamlaka ya kanisa , ambayo tangu wakati huo ilimuona kama msaliti kamili.
Mwaka 1791 Papa alitishia kumpiga marufuku. Lakini Talleyrand aliamua kuondoka katika ukuhani.

Alikuwa na uhusiano wa karibu na Napoleon​

Ugaidi uliwasili, wakati huo ambapo mapinduzi ya Ufaransa yalijawa na itikadi kali na magaidi wakaanza kuwakata vichwa bila kusita..
Talleyrand aliamua kuondoka Ufaransa na kutafuta uhifadhi Marekani, ambapo aliendelea kufanya biashara na kuendelea na maisha .
lakini aliipenda sana nchi yake na mwaka 1796 alirudi Ufaransa. Wakati huo utawala mpya ulikuwa umeapishwa , kwa jina Directory , utawala ambao ulitegemea sana wanajeshi na pamoja kati yao kijana mmoja kwa jina Bonarparte.
Napoleon akimpokea waziri waziri wake wa masuala ya kigeni

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Napoleon akimpokea waziri waziri wake wa masuala ya kigeni
Talleyrand alihudumu kama waziri wa fedha wakati wa utawala wa Directory na akamfanya Bonaparte kuwa Rafiki yake mkubwa , huku Napoleo akiwa amejipatia hadhi ya juu kutokana na ushindi wa jeshi barani Ulaya alifanya mapinduzi akisaidiwa na Talleyrand na kuchukua madaraka.
Serikali mpya iliapishwa , pia ikiwa na mahakama kwa jina la Consulate - ikiongozwa na Napoleon mwenyewe kama concul wa kwanza.
Akifahamu kipaji cha majadiliano cha Talleyrand , kitu cha kwanza ambacho Napoleon alifanya alipochukua madaraka ,ilikuwa kumchagua kuwa waziri wa masuala ya kigeni na kumsifu kwa nyadhfa tofauti.

Njama dhidi ya Napoleon​

Napoléon, akiwa na tamaa kubwa na kwa lengo la kuweza kuzungumza ana kwa ana na wafalme wa Ulaya, aliamua kubadilisha Ubalozi kuwa dola, akijitangaza kuwa Mfalme mnamo Mei 28, 1804.
Na ili Talleyrand asalie kando yake, alimteua Grand Chamberlain, Makamu wa Mteule wa Dola ya Kwanza ya Ufaransa na Mkuu wa Benevento, pamoja na kumpa mshahara mkubwa.
Napoleon Bonaparte alikuwa mfalme

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Napoleon Bonaparte alikuwa mfalme
Hata hivyo, pole pole Talleyrand alijitenga na Napoléon ambaye, alipofushwa na ubatili wake na mfululizo wa mafanikio, ambapo alianza kuchukua maamuzi mabaya zaidi.
Uvamizi wa Uhispania na Urusi uliwatenganisha.
"Nilikasirishwa na kila kitu nilichokiona na kusikia, lakini nililazimika kunyamazisha hasira yangu," Talleyrand aliandika katika kumbukumbu zake.
Aliishia kuwasilisha kujiuzulu kwake kama Waziri wa Mambo ya nje, akitaja sababu za kiafya.
Kwa upande wake, Bonaparte, hakuwahi kumsamehe kwa ishara hiyo na kumdhalilisha kila alipoweza
Alimlazimisha hata kuoa mwanamke ambaye alikuwa akiishi naye, na ambaye juu yake askofu wa zamani alikuwa amechoka naye.
Wakati huo, na kwa kuzingatia kwamba Napoléon alikuwa ameacha kuifanyia kazi Ufaransa na sasa alikuwa akifanya kwa maslahi yake mwenyewe, Talleyrand aliamua kuwa wakati umefika wa kummaliza kwa njia yoyote.
Talleyrand alipanga njama kando kando na kufanya kila awezalo kulazimisha kuondoka kwa Napoleon, ambaye mwishowe, alishindwa kwenye Vita vya Leipzig, na akajiuzulu kutoka wadhifa wake mnamo Aprili 1814.
Talleyrand ambaye ni mjanja baadaye aliamua kuunga mkono kupanda kwa umaarufu wa Louis XVIII, adui wa Napoleon na binamu wa Duke wa Enghien, ambaye njama za mauaji yake Talleyrand alikuwa amehusika.
Ingawa hakupenda Bourbons hata kidogo, aliamua kuwa mmoja wao ni bora kuliko Napoleon.
Talleyrand alikuwa mwakilishi wa Ufaransa katika Bunge la Vienna, mkutano wa kimataifa uliokusanyika kuandika upya mipaka ya Uropa baada ya kushindwa kwa Napoleon.
Mkutano wa Viena ambapo Talleyrand aliwakisha Ufaransa

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Mkutano wa Viena ambapo Talleyrand aliwakisha Ufaransa
Talleyrand alikuwa mwakilishi wa Ufaransa katika Bunge la Vienna akifanya "usimamizi mzuri" kulingana na Roca-Ferrer.
"Usimamizi wake katika Bunge la Vienna ulikuwa mzuri sana. Mataifa manne yenye uwezo mkubwa yaliokuwa dhidi ya Ufaransa, yalitaka kuifuta nchi hiyo milele, lakini Talleyrand kwa ustadi alifanikiwa kuibadilisha hali hiyo," anasema Roca-Ferrer.
Lakini Napoléon, aliyehamia mafichoni kisiwani Elba, aliweza kutoroka kutoka eneo hilo na kutishia kuchukua madaraka ya Ufaransa kwa nguvu.
Hali hiyo ilidumu kwa siku mia moja, na kushindwa kwake Napoleon huko Waterloo mnamo Juni 1815 kulimpatia sifa kubwa Talleyrand.

Balozi wa London​

Louis XVIII alifariki manmo mwezi Septemba 16, 1824. Ndugu yake , Count wa Artois, alimrithi kama Charles X .
Lakini mnamo 1830 yale yalioitwa Mapinduzi ya Julai, yaliungwa mkono na Talleyrand, na kumshinikiza Charles X kujiuzulu hatua iliofanya kiti cha enzi kuchukuliwa na Louis Philippe wa Orleans, ambaye alimteua Talleyrand kuwa balozi wa London.
Mkataba wa mwisho ambao Talleyrand alisaini ulikuwa ule wa Muungano wa Quadruple huko London, ambapo Ufaransa, England na Uhispania na Ureno zilishiriki.
"Alipigana maisha yake yote ili kutuliza uhusiano wa nchi ambazo aliamini zilikuwa za kistaarabu zaidi katika bara hili na kuwashawishi kwa ushirikiano ambao ungeweza kuwapendelea wote. Baada ya miaka 400 ya mapambano, alitaka Ufaransa na Uingereza kuelewana, "anasema Roca Ferrer.
"Haijalishi unatazama upande gani," Roca-Ferrer anaendelea, "alikuwa mtu aliyenusurika sana, aliishi miaka mingi na alipitia vipindi hatari sana ambavyo kila wakati aliweza kuepukana navyo ... na akawa tajiri. Kwa hivyo, kila kitu alichofikiria kitamfaidi yeye kilifaidi Ufaransa na kila kitu alichodhani kwamba Ufaransa itafaidika nacho kilimfaidi.

Lakini je alikuwa msaliti?​

"Yote inategemea jinsi unavyoiangalia. Alikuwa mtu ambaye alikuwa akibadilisha maoni yake katika nyakati tofauti. Kwa Talleyrand, mazingira yalibadilisha maoni. Yeye hakuwa mtu aliyejitakia sana , lakini alikuwa mtaalam aliyekuwa na mawazo mema.. Ndani kabisa, kila kitu alichokuwa akifanya kilikuwa akijifikiria yeye mwenyewe na Ufaransa. Kinachotokea ni kwamba kwake vitu vyote vilikuwa vimeunganishwa. Kwa sababu hii, uamuzi wa maadili ni ngumu sana kuutoa ", anasisitiza Roca-Ferrer.
 
Back
Top Bottom