Charles Mkwassa ndiye Kocha mpya wa Timu ya Taifa ya Soka

Mbilimbi Mbovu

Senior Member
Joined
May 25, 2015
Posts
185
Reaction score
119


Taarifa kutoka TFF zinasema kuwa Charles Boniface Mkwassa, ambae kwa sasa ni kocha msaidizi wa Klabu ya Yanga Afrika ameteuliwa rasmi kuwa kocha mkuu wa Taifa Stars na atakuwa akisaidiwa na kocha wa sasa wa Zanzibar Heroes, Hemed Moroco.

Chanzo: Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania

=======================
=======================


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - RELEASE NO. 103

TAREHE 23 JUNI 2015

NOOIJ AWAAGA WATANZANIA, MKWASA KUINOA STARS

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania - TFF, Jamal Malinzi leo ameagana rasmi na aliyekua kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, mholanzi Mart Nooij.


Akiongea na waandishi wa habari leo katika hoteli ya Tansoma, Malinzi amesema wameamua kuagana nae mbele ya vyombo ya habari kama iliyofanyika pia wakati wa utambulisho wake wakati wa kuanza kazi.


"Mpira wa miguu unachangamoto nyingi, watanzania tunasafari ndefu katika mafanikio ndio maana TFF imeanza kuwekeza katika soka la vijana, sababu ndio msingi wa kuwa na timu bora ya Taifa" alisema Malinzi.


Duniani kote chimbuko la timu bora ni soka la vijana na watoto, tukiwa na vijana wengi walioanza kucheza mpira katika umri mdogo wanapofikia umri wa kuchezea timu ya Taifa tutakua na kikosi bora.


Nchi za wenzetu inapofikia kocha kuita wachezaji wa timu ya Taifa anakuwa na wigo mpana, kwetu sisi wachezaji wanocheza soka nje ya nchi wanahesabika, hivyo ni lazima tuanze kuwekeza kwenye soka la vijana.


TFF ilishaanza mkakati huo ndio maana kuna timu za U13, U15 ambazo zitakua zikiingia kambini na kucheza michezo ya kirafiki ndani ya nje kwa lengo la kupata uzoefu kabla ya kushiriki kuwania kufuzu kwa fainali za vijana mwaka 2016.

Kikosi cha U15 kinatarajiwa kufanya ziara mwezi Disemba mwaka huu katika nchi za Malawi, Zambia, Zimbambwe, Botswana na Afrika Kusini, kisha mwakani mwezi April 2016 kitaenda Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya kucheza michezo ya kirafiki.


Naye Mart Nooij aliyekua kocha wa Taifa Stars, akiongea na waaandishi wa habari alisema anawashukuru watanzania wote, serikali, wadau wa mpira wa miguu nchini na TFF kwa sapoti waliyompatia wakati akiwa kocha mkuu wa timu ya Taifa.


Nooij alisema alifurahia maisha yake akiwa Tanzania kwa kipindi chote alichokua akifundisha timu ya Taifa, lakini kwa sababu imefikia mwisho wa ajira yake hana jinsi anaondoka, lakini ataendelea kuikumbuka Tanzania na watanzania wote kila siku kwa ukarimu wao.


Wakati huo huo Rais wa TFF. Jamal Malinzi amemtangaza Charles Mkwasa kuwa kocha mpya wa Taifa Stars akisaidiwa na kocha Hemed Morocco, Mkwasa ambaye ni kocha wa Yanga na Morocco kocha wa Mafunzo watafanya kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ambayo timu ya taifa itakua na michezo ya kuwania kufuzu kwa CHAN na AFCON.


Malinzi amesema uteuzi wa makocha hao wazawa umezingatia vigezo vya makocha wa timu ya Taifa kuwa na leseni A ya ukocha kutoka CAF au zinazofanana kutoka mashiriksho mengine duniani wanaozifanyia kazi, jambo ambalo makocha hao wazawa wamekizi.


Kocha Mkwasa atakua akipewa hudumu zote na masilahi (zikiwemo posho) alizokuwa anapewa kocha aliyeondoka, pia amepewa nafasi ya kuchagua benchi lake la ufundi la kufanya nalo kazi, hivyo nawaomba wadau wa mpira wa miguu na watanzania kwa ujumla tuwape sapoti makocha hao wazawa" aliongeza Malinzi"


Aidha Kamati ya utendaji ya TFF Iimemteua Alhaj Ahmed Mgoyi kuwa mratibu wa timu ya Taifa, lengo la uteuzi huo wa Mgoyi ni kuwa kiunganishi kati ya kamati ya Utendaji na timu ya Taifa.


U15 YAINGIA KAMBINI

Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 ya Tanzania, imeingia kambini jana na kuanza mazoezi leo katika uwanja wa Karume kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya kombaini U15 ya mkoa wa Mbeya siku ya jumapili.


Kikosi hicho kilicho chini ya makocha Bakari Shime na Peter Manyika kitacheza mchezo huo kwa lengo la waalimu kupatawa fursa ya kuwaona vijana hao na kuwaongeza wengine watakaoneka katika kikosi hicho.


U15 ni mpango wa TFF kuandaa kikosi kizuri chenye ubora kuelekea kuwania kufuzu ka fainali za vijana Afrika mwaka 2017 zitakazofanyika nchini Madagascar, ambapo vijana hao watakua na umri wa miaka 16 kufikia mwakani wakati michezo ya kuwania kufuzu itakaponza mwezi Julai, 2016.


NB: Kesho siku ya jumatano kocha mpya wa Taifa Stars, Charles Mkwasa na msaidizi wake Hemed Moroco wataongea na waandishi wa habari saa 5:30 asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume.


Waandishi wote wa habari mnaombwa kuhudhuria bila kukosa.

Imetolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania







 

Attachments

  • Mkwasa.jpg
    24.3 KB · Views: 2,550
Swali: Tulitarajia mtamteua kocha Bora, Mbwana Makata kuwa kocha mkuu, mbona imekuwa kinyume?

Jamal Malinzi: Suala la tuzo za Ligi Kuu tulikwisha litolea ufafanuzi. Na mimi binafsi nitalisimamia hilo kuzitendea haki fedha za wadhamini.
 
Swali: Kuna kawaida ya makocha wa kigeni kulipwa vizuri kuliko makocha wazawa na hivyo kufeli. Je, Kwa Mkwasa itakuwaje?

Jamal Malinzi: Tumempa ofa ya maslahi yote aliyokuwa analipwa kocha aliyemtangulia, yaani Nooij. Ataishi Masaki, atapewa gari na kila posho aliyokuwa anapata kocha Nooij.
 
Swali kutoka kwa mwandishi: Mkwasa atakuwa kocha kwa muda mgani wakati kocha wa kudumu akisakwa?

Jamal Malinzi: Kwanza niliongea na muajiri wake ambaye ni Bw. Manji kupata ruksa yake kisha tukaongea na mwalimu. Mpango tulionao na Mwalimu ni hadi Septemba 30 ingawa lolote linaweza kutokea ndani ya kipindi hicho
 
Swali: Kwa nini ulimfukuza Kim Poulsen kwa haraka haraka?
 

Naamini Mkwasa atafanya vizuri sana.. maana kupitia ligi kuu amewafahamu vyema wote wachezaji wote wa Tz.. hivyo kuwaunganisha hata pata tabu.
Kila la heri Mkwasa a.k.a Master.
 

Kwahiyo pale fire Mkwasa anahama sasa ili wakimfukuza baadaye arudi tena pale pale fire?
 
Mimi huwa sielewi kitu kimoja, Hivi selection ya wachezaji wa timu ya taifa huwa inafanyikaje? au wanachagua majina na si kipaji? au ni usimba na uyanga? mbona nchi hii kuna jamaa wanapiga mpira balaa wapo pembezoni mwa mjini, I suggest iundwe scouting team ipite sehemu mbalimbali za nchi hii kusaka vipaji vijana wasukwe ki-Professional Ethics, vinginevyo na huyu atatimuliwa tu
 

Mkuu hilo lilishanyika na ndo tukapata Taifa Starz-Maboresho.. Na hilo zoezi zima liligharimu milion mia tatu [300m].
 
Swali: Tumeshindwa kufuzu AFCON, leo unatupa jibu la uwekezaji kwenye soka la vijana, kwani umelitambua hilo baada ya sisi kushindwa au kabla ya uchaguzi?

Jamal Malinzi: Kwenye ilani yangu sikutoa ahadi ya Kufuzu AFCON. Niliyoyaahidi yapo kwenye ilani yangu na ipo wazi kila sehemu. Niliahidi kupambana na kujenga mfumo wa soka letu. Nikukumbusheni lipi nisilolifanyia kazi kati ya yote niliyoahidi.
 
Swali: Taifa Stars imefeli licha ya kupewa kila kitu, je huoni ni wakati wa kuweka nguvu zaidi kwenye Twiga Stars?

Jamal Malinzi: Tunatambua mchango wa Twiga Stars. Kidogo tunachokipata kutoka FIFA tunakipeleka huko. Juhudi za kuihudumia Twiga Stars zinafanyika.
 
Swali: Tunajua mshika mawili, moja humponyoka, je hamkufikiria kuhusu changamoto ya Mkwasa kuitumikia Yanga inayokabiliwa na mechi za kimataifa na Taifa Stars inayohitaji maandalizi zaidi?
 
Swali: Mmeongeza wachezaji wa kigeni, hauoni ni kama kuwanyima fursa wachezaji wazawa?

Jamal Malinzi: Kanuni za Ligi sio msahaufu, tunaendelea kupokea maoni, endeleeni kuchangia huu mjadala ambao upo dunia nzima kwa sasa. Lakini tusisahau changamoto ya uwezo wa wachezaji wetu. Nao wanahitaji kutoka nje kama wageni wanavyokuja kwetu.
 
Swali: Nani atalipa gharama za kuvunja mkataba wa kocha?

Jamal Malinzi: Licha ya mengi kuandikwa, TFF italipa gharama zote.
 
Swali: Kocha, umesema kuwa kujitolea kwako kuwapa nafasi vijana wasio na uzoefu ndio kumeangusha, je, ukipewa fursa nyingine utabadili hio falsafa?

Kocha Nooij: Sina cha kujutia, sidhani kama ningelifanya mambo tofauti na nilivyofanya awali endapo fursa hii ingejirudia.
 
Kwahiyo pale fire Mkwasa anahama sasa ili wakimfukuza baadaye arudi tena pale pale fire?

Mkwasa Hakai Fire Japo Alikuwa Anakaa Hapo Zamani Jirani Kabisa Na Kwao Said Tully Wa Simba Na Kwa Sasa Mkwasa Anaishi Tegeta Nyuki Kwa Mkewe Mheshimiwa Mkuu Wa Wilaya Betty Mkwasa Na Kuna Salon Moja Ya Kiume Hapo Hapo Jirani Na Njia Ya Kuelekea Chuo Kipya Cha Uandishi Wa Habari Cha PSJ Muda Mwingi Hukaa Hapo Kupiga Stori Na MASELA Na Wazee Vijana Wenzie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…