Charles William: Taarifa ya Nchimbi inakuonyesha hajajiuzulu kwa kutaka, Rais hamuitaji

Charles William: Taarifa ya Nchimbi inakuonyesha hajajiuzulu kwa kutaka, Rais hamuitaji

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079


Mtangazaji wa Wasafi Media, Charles William, ametoa uchambuzi kuhusu msamiati na lugha iliyotumika kwenye barua ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Makamu Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi.

Charles William amebainisha mambo makuu mawili yanayoashiria kuwa Dkt. Nchimbi hajajiuzulu kwa hiari yake kamili bali kutokana na shinikizo na kutokuridhika na mwenendo wa mambo ndani ya chama.

Soma
Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu

Mabadiliko ya Rais na Shinikizo la Kisiasa

Katika uchambuzi wake, Charles ameeleza kuwa kauli ya Dkt. Nchimbi kwamba ameamua kujiuzulu baada ya "kujiridhisha pasipo kuacha shaka kuwa Rais anahitaji mabadiliko" ina maana nzito ya kisiasa.

"Kwa lugha nyingine anajaribu kusema kwamba Rais hanihitaji. Ndio maana ya Rais anataka mabadiliko"

Kujitenga na Utii wa Chama na Siasa

Charles William ameeleza hitimisho la barua hiyo ambapo Dkt. Nchimbi anaeleza kustaafu siasa na kuahidi "kuendelea kuwa raia mwema wa Tanzania," badala ya kutumia lugha ya kimila ya makada wa CCM ya kuahidi kuendelea kuwa "mwanachama mtii" au kutoa ushirikiano kwa serikali.
 
1787747250384.png
 
Ni dhahiri Samia kwa kutokujiamini hataki mtu mwenye akili na mawazo mbadala
Samia anataka watu kama Aweso.Mwana fa. na kama hao wakiwa na jukumu la kumsifia na kumuabudu kwa kila hali.
Pili anataka watu vibaraka wanaotambua kuwa kula yao inamtegemea yeye hawa ni kina Mwigulu M.akonda .Kabudi nk
Tatu amewajaza Wazanzibari kila sehemu hawa anawaona ndugu zake akina Wanu. Mbarawa.Mombo.Thabit Kombo nk
Nne anategemea sana nguvu ya Polisi .Jeshi kumuweka madarakani kwa gharama yoyote
Tetesi ni kuwa jeshi kwa sasa limejaa watu toka kwao.
Hima Watanganyika nchi yetu inatekwa killing mno.
 
Back
Top Bottom