Mwandishi wa habari kutoka Wasafi Media, Charles William, ameeleza kuwa urasimu katika upatikanaji wa kibali na ukomo wa uhuru wa kihariri ndivyo vitu vinavyovizuia vyombo vya habari vya serikali na kurasa za taasisi zake kuripoti kwa haraka matukio makubwa nchini, yakiwemo ya utekaji na mauaji.
Charles amebainisha kuwa tofauti na vyombo vya habari vya binafsi ambavyo vina mfumo wa haraka wa kutoa na kuchapisha maudhui, vyombo vya serikali hupitia michakato mirefu ya kisheria na kiofisi kabla ya kutoa habari yoyote, jambo linalofanya taarifa zao kuchelewa au kutochapishwa kabisa.
Mbali na changamoto hiyo ya urasimu, Charles pia ameongeza kuwa uhaba wa bajeti na vifaa vya kazi kwa maafisa habari wa taasisi hizo huchangia kurudisha nyuma ubunifu na uwezo wao wa kufika maeneo mbalimbali kwa wakati ili kuandaa na kusambaza maudhui ya kutosha kwa umma.
Je, unakubaliana na hoja ya Charles?