Lee Van free
JF-Expert Member
- Aug 14, 2024
- 1,535
- 5,332
Wonder Boy Chasambi nakupa hongera sana kwa kurudi kibabe mchezoni baada ya kujifunga kwa bahati mbaya na kupelekea majonzi makali kwa mashabiki wa Simba na kupeleka furaha kubwa kwa mashabiki wa Yanga.
Ulitukanwa sana, ulidhihakiwa sana na walitaka kukutumia wewe kama ngazi ya kupeleka tafrani klabuni kwako, kwa kifupi walitamani taharuki itokee Klabu ya Simba.
Wajinga wachache wa Simba walikulaumu, lakini welevu wengi wa Simba walikuwa pamoja na wewe.
Soma Pia: Full Time: Simba SC 3-0 Tanzania Prisons | NBC Premier League | KMC Complex | 11 Februari, 2025
Wajinga wengi wa Yanga walikufurahia kwa kosa lako la kibinadamu ulilofanya, lakini kwa mechi hii kati ya Simba na TZ Prizoni umeweza kucheza vizuri na umefunga goli zuri kati ya magoli matatu mliyofunga yaliyowezesha kuirudisha Simba kileleni.
Umewaaibisha na kuwanyong'onyesha.
Wajinga wa Yanga nasikia waliandaa keki ya kukupongeza, waliandaa kuchangishana hela na waliandika jina lako kwenye jezi za Yanga kwa ajili ya kukupongeza kinafiki ili kuleta mvurugano klabuni kwako.
Hongera sana kwa Viongozi wa Simba kwa kuzima uzandiki, unafiki na fitina hizo, baada ya kung'amua njama hizo dhaifu na kuweza kumjenga Chasambi kisaikolojia.
Kwa kifupi goli ulilofunga Chasambi, limewafunga midomo Yanga na kuwaaibisha.
Nimeona baada ya kumalizika mchezo wa Leo mashabiki wa Simba wamekupa Hela nyingi ikabidi mshabiki mmoja akupe kapu la magoli ili uwekee Hela.
Ushauri wangu, nakushauri kapu hilo usilitipe, ulitunze, katika maktaba Yako ya soka pamoja na medali ama zawadi nyingine zinazotunzika ili iwe ukumbusho wako utakapojaaliwa kustaafu soka.
Nasema hivi kwa sababu watu waovu katika soka la Tanzania walitaka kukuchonganisha na Klabu Yako, uongozi wako na mashabiki wako lakini wamefeli.
Kumbuka wewe sio mchezaji wa Simba TU, Bali wewe ni mchezaji wa Tanzania kwa ujumla.