Steven Joel Ntamusano
JF-Expert Member
- Jun 17, 2023
- 5,203
- 3,913
Suala dogo sana sisi mashabiki tunalikuza na nia ni kutaka kuivuruga morali nzima ya Simba, sidhani kama msimu huu hilo lengo linaweza kufanikiwa.Ishu sio kumtaja Max ishu kusema kwenye timu yangu ya Simba hakuna ninayemtizama na kujifunza kwake (Role Model)
Angejibu tu Max kwenye jibu la kwanza bila kudharau wachezaji wenzake ingekaa poa sana nadhani wala kusingekuwa na mijadala kama hii
Wajinga tu, wanataka kuzipa nafasi ya dini zao hizi timu mbili za kariakoo.Uhuru wa kujieleza uzingatiwe...Mim ni yanga lakini namkubali sana Muhammed Hussein Zimbwe junior...
Maisha sio magumu kiasi hicho mkuu
Inaweza kuwa unamkubali Zimbwe na pia unamkubali Pacome. Lakini kama hayupo mchezaji wa yanga unaemkubali Kwa wewe shabiki sio ishu . Ila Kwa mchezaji kuropoka kuwa hakuna mchezaji unaevutiwa nae Kwenye timu yako, hapo akili yako inakuwa haiko Sawa. Pamoja na kwamba hiyo ni ajira lakini mchezaji unatakiwa uwe na kaushabiki Kwa hiyo timu unayochezea Kwa wakati huo, hivyo unatakiwa uwe makini na kauli na ndio maana huko ulaya wachezaji wanaziba midomo wanapohisi kauli zao zinaweza kuwaletea shida.Uhuru wa kujieleza uzingatiwe...Mim ni yanga lakini namkubali sana Muhammed Hussein Zimbwe junior...
Maisha sio magumu kiasi hicho mkuu
Mkuu sasa hivi mnataka muanze kumlaumu Ally Kamwe. Nadhani yeye amefanya kama mtu wa propagandist na hii hata kwenu ipo. Yan unaangalia udhaifu uko wapi unatumia hapo kumchangamsha mpinzani ilimradi akose raha na amani.Hii imekuzwa na kufanywa kuwa agenda kuu na Ally Kamwe kwa jinsi alivyoiwekea michambo.
Amekukosea we usie na upeo wa kutafakari, ulitaka aseme uongo aingie dhambin kwa sababu yako?
View: https://www.youtube.com/watch?v=NTfMlQAdvLs
Mtangazaji: Katika uchezaji wako wa mpira Chasambi, nani unamtizama kama kioo kwako"
Chasambi: Namtizama kama kioo kwenye timu yangu au......?
Mtangazaji: Role model wako
Chasambi: Kwenye timu yangu
Mtangazaji: Akaitikia kwa kutikisa kichwa
Chasambi: Kwenye timu yangu hapana, hakuna (anatikisa kichwa kukataa)
Mtangazaji: Kokote
Yaani timu nzima hakuna mchezaji anayeweza kumtazama kama kioo. Yaani timu nzima ikiwepo Tshabalala na Kapombe? Maana hapa hukuulizwa kuhusu nafasi anayocheza. Yaani hata watu wanaopambana kufa na kupona kina Fabrice Ngoma sio kioo kwake. Hata kama, ndio utaje mchezaji wa Yanga?!!!! Iko wapi Ubaya Ubwela.
Amewadharau wachezaji wenzake wote kwa kusema hakuna mchezaji anayeweza kumtazama kama kioo na hakuna anachojifunza kwao.
Dogo nafikiri Simba na Yanga hazijui vizuri
Mimi naona kabisa hafurahii kukaa benchi pale Simba kwa sababu anajiona ana uwezo ndio maana ameamua kupuyanya tu kwenye media. Hapo anatafuta soko huko Yanga. Hii ni makusudi!Umri unaweza kuchangia ila ni kama alidhamiria kutoa jibu hilo lenye ukakasi.
Niliwahi kusema kitengo cha media pale Simba kiongezewe watu. Mchezaji au kiongozi wa Simba akihojiwa inabidi mtu wao wa media awepo pale. Kama kuna swali hatakiwi kujibu anamzuia. Kama kuna jibu amepuyanga kama hili, anamwambia mwandishi hilo jibu asilitumie.
Kaangalia vijana wenzake wa Moro kina kibwana, kibabage, msher na job.Mimi naona kabisa hafurahii kukaa benchi pale Simba kwa sababu anajiona ana uwezo ndio maana ameamua kupuyanya tu kwenye media. Hapo anatafuta soko huko Yanga. Hii ni makusudi!