Chasambi katukosea heshima wana Simba, atuombe msamaha

Chasambi katukosea heshima wana Simba, atuombe msamaha

Ishu sio kumtaja Max ishu kusema kwenye timu yangu ya Simba hakuna ninayemtizama na kujifunza kwake (Role Model)
Angejibu tu Max kwenye jibu la kwanza bila kudharau wachezaji wenzake ingekaa poa sana nadhani wala kusingekuwa na mijadala kama hii
Suala dogo sana sisi mashabiki tunalikuza na nia ni kutaka kuivuruga morali nzima ya Simba, sidhani kama msimu huu hilo lengo linaweza kufanikiwa.
 
Kaongea ukweli wake sasa kama ndani ya timu yetu haoni mchezaji kioo kwake tutamlazimisha ili amwone wakati yeye haoni😂
 
Uhuru wa kujieleza uzingatiwe...Mim ni yanga lakini namkubali sana Muhammed Hussein Zimbwe junior...

Maisha sio magumu kiasi hicho mkuu
Inaweza kuwa unamkubali Zimbwe na pia unamkubali Pacome. Lakini kama hayupo mchezaji wa yanga unaemkubali Kwa wewe shabiki sio ishu . Ila Kwa mchezaji kuropoka kuwa hakuna mchezaji unaevutiwa nae Kwenye timu yako, hapo akili yako inakuwa haiko Sawa. Pamoja na kwamba hiyo ni ajira lakini mchezaji unatakiwa uwe na kaushabiki Kwa hiyo timu unayochezea Kwa wakati huo, hivyo unatakiwa uwe makini na kauli na ndio maana huko ulaya wachezaji wanaziba midomo wanapohisi kauli zao zinaweza kuwaletea shida.

Kusema hakuna mchezaji anaekuvutia Kwenye timu yako ni kuishusha hadhi timu yako.

Kama ni Uhuru wa kujieleza , mchezaji wa yanga akisema ni shabiki wa Simba utaona Sawa?
 
Kuna muda makolo huwa mnatusaidia kuprove kile alichotamka Rage ni sahihi kabisa. Kwa sababu haiwezekani kitu cha kawaida hivi mnakikuza kwa kiasi hiki. Uzuri wangu ni kwamba ile interview ya Max akiwataja Awesu, Feisal, Mtasingwa niliiona kabla lakini kwangu sikuwahi kuichukulia ivyo kwasababu ninaamini hayo ni mambo ya mpira na ni kitu kiko wazi ivyo wao kukubali anachofanya mwenzake nje ya Yanga ni jambo la kawaida.

Ukiwa shabiki wa mpira haya utaona kawaida. Ila ukiwa shabiki andazi andazi wa hizi timu ndio madhara yake haya. Hapa dogo ataanza kukosa confidence ashindwe ku perform vizuri waanze kulaumiwa Yanga.
 
Hajakosea ni maoni ya mtu na ameongea ukweli wake shida wanayanga wameifanya aonekane mkosefu
 
Hii imekuzwa na kufanywa kuwa agenda kuu na Ally Kamwe kwa jinsi alivyoiwekea michambo.
Mkuu sasa hivi mnataka muanze kumlaumu Ally Kamwe. Nadhani yeye amefanya kama mtu wa propagandist na hii hata kwenu ipo. Yan unaangalia udhaifu uko wapi unatumia hapo kumchangamsha mpinzani ilimradi akose raha na amani.

Ambacho hamkupaswa kufanya ni ku react baada ya ile post. Hii inamfanya aamini amefanikiwa, sasa kilichopo ni nyie mmepacick mnaanza kutafutana ubaya mwisho dogo atakosa utulivu ashindwe ku perform vizuri kwa sababu wenyewe mnamtia pressure.
 
Huyu dogo bwege chasambi ni shabiki wa utopolo Toka akiwa mdogo Bora tumuache aende utopoloni yanga
 
Dogo kaongea kama shabiki. Ili kulinda brand ya Simba alitakiwa ajibu kwenye klabu yangu kuna wachezaji wazuri ila role model wangu ni Maxi Nzengeli.

Ukiwa kwenye hizi timu mambo hayaishii tu uwanjani. Hata nje ya uwanja wewe ni balozi wa klabu yako.
 

View: https://www.youtube.com/watch?v=NTfMlQAdvLs

Mtangazaji: Katika uchezaji wako wa mpira Chasambi, nani unamtizama kama kioo kwako"
Chasambi: Namtizama kama kioo kwenye timu yangu au......?
Mtangazaji: Role model wako
Chasambi: Kwenye timu yangu
Mtangazaji: Akaitikia kwa kutikisa kichwa
Chasambi: Kwenye timu yangu hapana, hakuna (anatikisa kichwa kukataa)
Mtangazaji: Kokote

Yaani timu nzima hakuna mchezaji anayeweza kumtazama kama kioo. Yaani timu nzima ikiwepo Tshabalala na Kapombe? Maana hapa hukuulizwa kuhusu nafasi anayocheza. Yaani hata watu wanaopambana kufa na kupona kina Fabrice Ngoma sio kioo kwake. Hata kama, ndio utaje mchezaji wa Yanga?!!!! Iko wapi Ubaya Ubwela.

Amewadharau wachezaji wenzake wote kwa kusema hakuna mchezaji anayeweza kumtazama kama kioo na hakuna anachojifunza kwao.

Dogo nafikiri Simba na Yanga hazijui vizuri

Amekukosea we usie na upeo wa kutafakari, ulitaka aseme uongo aingie dhambin kwa sababu yako?
 
Umri unaweza kuchangia ila ni kama alidhamiria kutoa jibu hilo lenye ukakasi.

Niliwahi kusema kitengo cha media pale Simba kiongezewe watu. Mchezaji au kiongozi wa Simba akihojiwa inabidi mtu wao wa media awepo pale. Kama kuna swali hatakiwi kujibu anamzuia. Kama kuna jibu amepuyanga kama hili, anamwambia mwandishi hilo jibu asilitumie.
Mimi naona kabisa hafurahii kukaa benchi pale Simba kwa sababu anajiona ana uwezo ndio maana ameamua kupuyanya tu kwenye media. Hapo anatafuta soko huko Yanga. Hii ni makusudi!
 
Mimi naona kabisa hafurahii kukaa benchi pale Simba kwa sababu anajiona ana uwezo ndio maana ameamua kupuyanya tu kwenye media. Hapo anatafuta soko huko Yanga. Hii ni makusudi!
Kaangalia vijana wenzake wa Moro kina kibwana, kibabage, msher na job.
Kaona Bora atafute njia na yeye aje.
Hana kosa, kosa wanalo hao mashabiki wa simba
 
Back
Top Bottom