Chat gpt imenitimizia ndoto ya kuandika kitabu changu, sina haja ya kumlipa proof reader kusahisha makosa ya grammer / broken english

Chat gpt imenitimizia ndoto ya kuandika kitabu changu, sina haja ya kumlipa proof reader kusahisha makosa ya grammer / broken english

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Nilikuwa na ndoto ya muda mrefu sana ya kuandika kitabu changu cha taaluma niliyosomea, kuna somo nipo nondo vibaya mno !!

Hofu yangu kubwa ilikuwa ni english kwenye mambo ya grammer, articles, prepositions, nk.

Chat GPT imenipa confidence kubwa sana, nachofanya naandika kurasa moja au mbili siku nayokuwa na muda then naitupia kwenye chat gpr naandika "I am writing a book, Polish my english" Kazi kwisha, Mtambo unatema yai, kuna usahishaji binafsi kidogo sana naufanya mfano kufuta sentensi na kuweka msamiati wa kitaalam kuendana na somo.

Nikimaliza kuandika kitabu sana sana ntalipa wa kukipangalia na Graphic designer wa cover
 
Hongera... kwenye kupolish tu ulichoandika chatgpt apewe maua yake... anafanya vizuri sana
 
Kwangu kutumia chatgpt ni mtihani maana haina ile flow ya kibinadamu maana imekuwa designed kuwa na standard English ambayo hutumika kwenye ishu za academic.

Kwa hiyo Mimi ni kheri nitumie quillbolt na nikiona kuna utata, nitatumia chatgpt kunyoosha sentensi lakini nitakuwa strict ili isiharibu tone na mtiririko wa mwanzo.

Lakini njia nyingine napenda mtu asome ili anipe feedback ya kibinadamu na sio kiroboti..

Ila kama kwako ipo sawa, hongera mkuu.
 
Ngoja na sisi tukuandikie vizuri kwa ChatGPT.

Nilikuwa na ndoto ya muda mrefu ya kuandika kitabu changu na kukiweka kwenye Amazon, soko kubwa la kimataifa.

Hata hivyo, hofu yangu kuu ilikuwa ni kuhusu matumizi sahihi ya Kiingereza, hasa kwenye sarufi, matumizi ya prepositions, herufi kubwa, na mengineyo.

Kwa bahati nzuri, ChatGPT imenipa ujasiri mkubwa sana. Kile ninachofanya ni kuandika kurasa moja au mbili siku ninapopata muda, kisha naituma kwenye ChatGPT na kusema, "I am writing a book, Polish my English." Na hapo kazi inakuwa imekwisha!

Nikimaliza kuandika, mpango wangu ni kumtafuta mtaalam wa kuhariri maandishi yangu kwa ukamilifu na mbunifu wa picha kwa ajili ya sampuli ya jalada la kitabu.

Ndoto hii sasa inaonekana kuwa karibu kufikiwa!
 
Kwangu kutumia chatgpt ni mtihani maana haina ile flow ya kibinadamu maana imekuwa designed kuwa na standard English ambayo hutumika kwenye ishu za academic.

Kwa hiyo Mimi ni kheri nitumie quillbolt na nikiona kuna utata, nitatumia chatgpt kunyoosha sentensi lakini nitakuwa strict ili isiharibu tone na mtiririko wa mwanzo.

Lakini njia nyingine napenda mtu asome ili anipe feedback ya kibinadamu na sio kiroboti..

Ila kama kwako ipo sawa, hongera mkuu.
Madini yote ya maarifa ya kitabu nachoandika ninayo kichwani, Chat Gpt inasahisha lugha tu

Chat gpt imekamilika vizuri kwenye lugha kuzidi academics, weka maarifa yako itayapendezesha kwenye lugha lakini ukitegemea maarifa kutoka chat gpt huwa kuna muda inakosea na ni ngumu kuwa sawa na aliyejifunzia darasani, ndio maana wanafunzi wengi wavivu wanaotegemea chatgpt iwajibie maswali wanadakwa kirahisi na walimu
 
Sijui hata ni kitu gani, am I being out of touch?
 
ChatGTP na Ai zote hazina kitu zinashindwa..

Unaweza ukaandika Flow yako ya kielimu na miaka yake, Kazi ulizofanya/ajira, internship/fields, Qualifications,
Person details zako, achievement zako, hobbies n.k

Halafu unaicomand "Construct My CV" Ipe dk 1½ uone show.
 
Madini yote ya maarifa ya kitabu nachoandika ninayo kichwani, Chat Gpt inasahisha lugha tu

Chat gpt imekamilika vizuri zaidi kwenye lugha kuzidi academics
nachomaanisha. Chatgpt inaweza isiharibu content Ila ikaharibu uwasilishwaji wa content zako ambayo inaweza kuharibu tone na mtiririko wako binafsi na hata maana uliyokusudia japo sio sana..

Ndio maana nikasema kama huwa unapitia na kuedit kile chatgpt inakupa na kukiona ni super.. Bhasi ishi nayo mkuu Ila kuna watu hiyo chatgpt hawaitumii, wanatumia copilot ya Bing ambayo wanaona ni bora zaidi.

Kwa hiyo unachoona ni sawa kwako. Tumia tu mkuu
 
Sijui hata ni kitu gani, am I being out of touch?
Kidogo sio sana mkuu na inategemea na field yako.

Chatgpt ni artificial intelligence system ambayo unaweza kuicommand kufanya chochote haswa cha kimaandishi. Iwe kuandika kitabu, proposal, movie script, kusahihisha grammar. Yani chochote kile

Unachofanya ni kuweka tu inputs zako.. Then inakutolea kitu na ikikosea unairekabisha. Ni kama chat tu ya kawaida na professional unayempa kazi ya kukuandikia kitu flani lakini sasa hii ni mfumo wa kidigitali
 
nachomaanisha. Chatgpt inaweza isiharibu content Ila ikaharibu uwasilishwaji wa content zako ambayo inaweza kuharibu tone na mtiririko wako binafsi na hata maana uliyokusudia japo sio sana..

Ndio maana nikasema kama huwa unapitia na kuedit kile chatgpt inakupa na kukiona ni super.. Bhasi ishi nayo mkuu Ila kuna watu hiyo chatgpt hawaitumii, wanatumia copilot ya Bing ambayo wanaona ni bora zaidi.

Kwa hiyo unachoona ni sawa kwako. Tumia tu mkuu
Yes lazima nihakikishe siwezi ku copy na ku oaste, baadhi ya sehemu naweza kuongeza au kupunguza vitu kadhaa kuendana na subject.

Ulimwengu wa AI unazidi kupanuka na kuboreshwa, zipo nyingi za ziada kama copilot, bing, Germini, n.k. uchaguzi ni wako kwa itayokidhi vigezo unavyohitaji
 
Hapo sawa mkuu. All the best kaka 🙏🏽
 
Kutumia ChatGPT kuandika kazi zangu naona ni ku-cheat, shortcut na uvivu. Sababu badala ya kujifunza vitu effectively na kudevelop as an individual, unabaki stagnant, incompetent na dependent kwa hiyo machine na aliyeitengeneza. Vilevile hiyo kazi inakuwa siyo ya mikono wala akili yako tena na ni ngumu kutake credits na kujipongeza. Ili nisikie satisfaction ya mafanikio ni lazima kitu nikiangaikie. Kama tatizo ni grammer basi nitatumia grammarly kuliko ChatGPT inayo rewrite kila kitu according to its parameters.

Anyway that's my view. Kumbuka tu kuna Algorithms zinazodetect AI written works.
 
Kutumia ChatGPT kuandika kazi zangu naona ni ku-cheat, shortcut na uvivu. Sababu badala ya kujifunza vitu effectively na kudevelop as an individual, unabaki stagnant, incompetent na dependent kwa hiyo machine na aliyeitengeneza. Vilevile hiyo kazi inakuwa siyo ya mikono wala akili yako tena na ni ngumu kutake credits na kujipongeza. Ili nisikie satisfaction ya mafanikio ni lazima kitu nikiangaikie.

Anyway that's my view. Kumbuka tu kuna Algorithms zinazodetect AI written works.
Kazi inakuwa ya akili yangu yenye maarifa husika na mikono yangu nayochapa kurasa za kutosha.. Hio Chat Gpt inarekebisha kiingereza kwenye kurasa nilizochapa.

Ni sawa na kuwa boss uandike ripoti, ukimaliza unampa secretary aipange vizuri

Wanaoitumia iwafikirie na kuwaandikia kila kitu mfano wanafunzi wavivu wa vyuoni huwa yanawakuta mazito, kazi zinafanana, kuna majibu inakosea, n.k.
 
Back
Top Bottom