Chatanda awasili Mwanza kushiriki mazishi ya Jane Msoga

Chatanda awasili Mwanza kushiriki mazishi ya Jane Msoga

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
IMG-20240503-WA0014.jpg

📅 03 Mei, 2024
📍 Mwanza

Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) amewasili Uwanja wa Ndege Mwanza usiku wa kuamkia tarehe 03 Mei, 2024 kushiriki mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti Umoja wa Wanawake Wilaya ya Sengerema Ndg. Jane James Msoga.

Ndg Jane alifariki tarehe 01 Mei, 2024 katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza Seko Toure na anatarajia kuzikwa Sengerema Mjini - Kata ya Nyampurukano Mei 03, 2024.


#UWTimara
#JeshiLaMama
#Kaziiendelee
 
CHATANDA ASHIRIKI IBADA YA MAZISHI YA ALIYEKUWA MWENYEKITI UWT WILAYA YA SENGEREMA NDG. JANE MSOGA

📅 03 Mei, 2024
📍 Mwanza Sengerema

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) amefika Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza katika Kanisa la AICT (African Inland Church Of Tanzania) kwaajili ya kushiriki Ibada ya Mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti Umoja wa Wanawake Wilaya ya Sengerema Ndg. Jane James Msoga ambaye alifariki Dunia tarehe 30 Aprili, 2024 Katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza Seko Toure.

Mwenyekiti Chatanda akiwa Sengerema amepokelewa na viongozi wa Chama na Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya Bi. Senyi Ngaga na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Wajumbe Kamati ya Siasa Wilaya, Wenyeviti wa UWT Wilaya sita za Mwanza.

Marehemu Jane ameacha Mume na Watoto 11 wakiwemo watoto wakike 7 na Wakiume 4. Mwili wake unatarajia kuhifadhiwa katika nyumba yake ya Milele Sengerema Mjini Kata ya Nyampurukano tarehe 03 Mei, 2024.

Ibada hiyo imehudhuriwa na Mjumbe Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Viti 20 Tanzania Bara Ndg. Ellen Bogohe, Mwenyekiti CCM Sengerema, viongozi wa UWT Mkoa wa Shinyanga, Wajumbe Baraza Kuu UWT Taifa, Mbunge Jimbo la Buchosa, Wabunge Viti Maalum Mkoa wa Mwanza.

Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe. Amina 🙏🏼

#UWTimara
#JeshiLaMama
#Kaziiendelee
 

Attachments

  • IMG-20240503-WA0054.jpg
    IMG-20240503-WA0054.jpg
    81.7 KB · Views: 3
  • IMG-20240503-WA0057.jpg
    IMG-20240503-WA0057.jpg
    62 KB · Views: 2
  • IMG-20240503-WA0062.jpg
    IMG-20240503-WA0062.jpg
    159.4 KB · Views: 2
  • IMG-20240503-WA0058.jpg
    IMG-20240503-WA0058.jpg
    94.6 KB · Views: 2
  • IMG-20240503-WA0059.jpg
    IMG-20240503-WA0059.jpg
    109.2 KB · Views: 3
  • IMG-20240503-WA0051.jpg
    IMG-20240503-WA0051.jpg
    52.3 KB · Views: 4
  • IMG-20240503-WA0055.jpg
    IMG-20240503-WA0055.jpg
    87.3 KB · Views: 3
  • IMG-20240503-WA0053.jpg
    IMG-20240503-WA0053.jpg
    80.2 KB · Views: 3
  • IMG-20240503-WA0052.jpg
    IMG-20240503-WA0052.jpg
    94.5 KB · Views: 3
  • IMG-20240503-WA0056.jpg
    IMG-20240503-WA0056.jpg
    61.3 KB · Views: 2
Back
Top Bottom