Chatanda: Wazazi zungumza na watoto wenu kulinda maadili

Chatanda: Wazazi zungumza na watoto wenu kulinda maadili

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Jumuiya ya Wanawake CCM (UWT) imeungana na Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii katika kuadhimisha Siku ya Familia Duniani, ikiwataka wazazi kuungana katika suala la malezi badala ya kumwachia mzazi mmoja.

Hayo yamezungumzwa leo Mei 15, 2024 jijini Dodoma na mwenyekiti wa UWT, Mary Chatanda wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa jumuiya hiyo.

Chatanda amesema jamii kwa sasa imekumbwa na changamoto za malezi zinazotokana na sababu mbalimbali, ikiwemo masuala ya teknolojia na utandawazi, kukosekana kwa amani na upendo ndani ya familia, ambayo yanapelekea malezi duni kwa wototo na kuongezeka ukatili wa kijinsia.

Amesema kwa kuliona hilo, UWT imetengeneza kamati mbalimbali za kupambana dhidi ya ukatili wa wanawake na watoto inayofanya kazi nchi nzima.

Vilevile Chatanda amesema wazazi na walezi wanao wajibu wa kutimiza mahitaji ya msingi kwa watoto ambayo ni lishe bora, mavazi, malazi na elimu ili kuwajengea mazingira mazuri ya ukuaji kiakili na kisaikolojia.
 
Huyu huyu Chatanda aliyesema anaipenda CCM kuliko watoto/familia yake ama kuna Chatanda mwingine?
 
Huyu huyu Chatanda aliyesema anaipenda CCM kuliko watoto/familia yake ama kuna Chatanda mwingine?
Ndio huyohuyo mkuu..
Hawa watu ndio tunawategemea mawazo yao tu'compete na nchi timamu
 
Maadili...yepi
Watoto wenu washakata kamba
Sahvi

Ova
 
Back
Top Bottom