Chato pajengwe Chuo Kikuu cha Afya kama MUHAS

Mr_Teacher

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2021
Posts
362
Reaction score
343
Wanabodi salaam.

sitokei kanda ya ziwa na wala sipapigii debe Chato nyumbani kwa Mzee JPM, ila naleta mada hii kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Pale Chato pamejengwa Hospitali kubwa ya Rufaa ya Kanda, ina majengo mazuri sana na nina Imani hata vitendea kazi pia, lakini nna mashaka bado idadi ya wagonjwa ni ndogo hata ukilinganisha na ya pale Bugando, wengi wamepiga kelele kuwa Mzee JPM alivutia kwao, sawa but ni Tanzania moja hii.

Nashauri ili kuipa hii hospital ubize na kuweza kufanya kazi kwa viwango kama ulivyo ukubwa wake pale Chato pajengwe Chuo kikuu cha Afya kama ilivyo MUHAS.

Chuo kiitwe tu Chato University of Health and Allied Sciences (CUHAS), tukifanya hivi maana yake wanafunzi wa CUHAS wataitumia hii hospital ktk mafunzo yao kama ilivyo wa MUHAS wanavyoitumia MNH. hii itasaidia sio tu kutibu watu wengi pale lakini pia kuongeza fursa kwa watanzania wanaotaka kusomea kada za Afya kwa kuongeza wigo mpana wa vyuo lakini pia kutaongezeka Ajira.

Nawasilisha, aone Rais Samia Suluhu ili aone namna.
 
Mtwara inajengwa hospitali ya rufaa; na kusini kote hakuna chuo kikuu! Kwanini isiwe Mtwara na badala yake iwe Chato?

Nyie watu hata mjifiche vipi, katu rangi yenu haiwezi kufichika! Unaweza usiwe wa Kanda ya Ziwa lakini ukawa MATAGA uliekuwa unaunga mkono ujinga ujinga!
 
Chato ni muhimu kuliko huko kwenu,endeleeni kula chamaki nchanga.
 
Mtwara inajengwa hospitali ya rufaa; na kusini kote hakuna chuo kikuu! Kwanini isiwe Mtwara na badala yake iwe Chato?

Nyie watu hata mjifiche vipi, katu rangi yenu haiwezi kufichika! Unaweza usiwe wa Kanda ya Ziwa lakini ukawa MATAGA uliekuwa unaunga mkono ujinga ujinga!
nilisahau kuhusu Mtwara, ni sawa kabisa nako pakaboreshwa kuwa na Chuo Kikuu kwa ajili ya Ukanda ule, nazidi kuunga mkono hoja
 
Yaani wagonjwa ni wachache halafu upeleke na chuo wakajifunzie kwenye hao wagonjwa wachache! Hii ni akili kweli? Au chuo kinaongeza idadi ya wagonjwa?
kikijengwa Chuo jua kuwa kutaongezeka makazi pia, lakini zaidi kutafunguka fursa nyingi za kibiashara pia, hivyo wagonjwa watapatikana tu!!! na zaidi zaidi wataletwa wagonjwa wengi wa rufaa
 
Wewe, hebu pumzika chato chato chato mnachangia sh ngapi pato la taifa kiasi kila kitu kije huko kwenu.... Mna kipi special?
 
Mtwara inajengwa hospitali ya rufaa; na kusini kote hakuna chuo kikuu! Kwanini isiwe Mtwara na badala yake iwe Chato?

Nyie watu hata mjifiche vipi, katu rangi yenu haiwezi kufichika! Unaweza usiwe wa Kanda ya Ziwa lakini ukawa MATAGA uliekuwa unaunga mkono ujinga ujinga!
Vyuo vikuu vipo kusini acha uongo
 
Waliosema Chato itakuwa Kama Gbadolite ya Mobutu walikuwa wamemaanisha hiki kinachotokea sasa. Tutajidanganya kupeleka wataalamu na dawa na vifaa kwa muda, lakini mwisho wa siku itabidi tubadili matumizi ya jengo.
Unayoiongelea Referral Hospital unaongelea uwapo wa Madaktari bingwa (specialists). Ni daktari bingwa gani atakubali kukaa Chato?
 
Wanabodi salaam.

sitokei kanda ya ziwa na wala sipapigii debe Chato nyumbani kwa Mzee JPM, ila naleta mada hii kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Pale Chato pamejengwa Hospitali kubwa ya Rufaa ya Kanda, ina majengo mazuri sana na nina Imani hata vitendea kazi pia, lakini nna mashaka bado idadi ya wagonjwa ni ndogo hata ukilinganisha na ya pale Bugando, wengi wamepiga kelele kuwa Mzee JPM alivutia kwao, sawa but ni Tanzania moja hii.

Nashauri ili kuipa hii hospital ubize na kuweza kufanya kazi kwa viwango kama ulivyo ukubwa wake pale Chato pajengwe Chuo kikuu cha Afya kama ilivyo MUHAS.

Chuo kiitwe tu Chato University of Health and Allied Sciences (CUHAS), tukifanya hivi maana yake wanafunzi wa CUHAS wataitumia hii hospital ktk mafunzo yao kama ilivyo wa MUHAS wanavyoitumia MNH. hii itasaidia sio tu kutibu watu wengi pale lakini pia kuongeza fursa kwa watanzania wanaotaka kusomea kada za Afya kwa kuongeza wigo mpana wa vyuo lakini pia kutaongezeka Ajira.

Nawasilisha, aone Rais Samia Suluhu ili aone namna.
Mkuu Leo ndege zmetua ngp gapo airport chato?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom