Chato: Raia walalamika kupigwa na Askari wa Maliasili

Chato: Raia walalamika kupigwa na Askari wa Maliasili

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Wakazi wa Kata ya Buseresere Wilayani Chato Mkoani Geita wamemuomba Waziri wa Maliasili na Utalii kuchukua hatua kwa askari wa maliasili wanaowapiga na kuwadhalilisha wananchi nyakati za usiku na mchana wakati wakiendesha zoezi la kutafuta mkaa majumbani kwa madai ya kukomesha uchomaji mkaa.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Buseresere wananchi hao wamesema askari hao kwa kushirikiana na mgambo wamekuwa wakiendesha operesheni hiyo bila kushirikisha viongozi wa serkali za vijiji na kujeruhi watu.

Diwani wa Kata ya Buseresere, Bw. Geodfrey Miti amesema tatizo hilo amelifikisha ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa, lakini hatua hazijachukuliwa na amewataka wananchi kuwadhibiti askari hao pindi wanapoingia katika maeneo yao.
 
Kwahiyo mwendazake alipowahamishia Sungura, swala, pundamilia na simba walishangilia walijua watapata mgao wa kitoweo?

Hamna namna wachapwe tu.
 
Back
Top Bottom