Chato's Story/Chato's Land

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Chato ya kwanza ni kitabu kipya kinachoeleza historia ya kijiji cha Chato Tanzania.

Chato ya pili ni jina la movie iliyochezwa mwaka wa 1972 muigizaji akiwa Charles Bronson.

Kitabu cha Chato kama ingekuwa movie ingekuwa na waigizaji wakubwa wa sifa.

Halikadhalika ingekuwa movie ya kuvutia na kusisimua sana khasa ukizingatia kuwa "script writers" ni waandishi watatu mashuhuri sana katika tasnia ya uandishi wa magazeti.

Kitabu kina kasi kubwa. Ni kitabu cha mkasa mmoja kwenda mwingine.

Mikasi ikifatana na maelezo ya wahusika wakuu.

Ingekuwa movie tungesema ina "dialogue," ya kuvutia.

Ukianza ukurasa wa kwanza hukifungi na kukiweka chini hadi umegonga tamati.

Movie Chato's Land wachambuzi wa senema wanasema haina, "dialogue," yaani mazungumzo ni kidogo sana.

Matukio ya unyama na ubabe wa Sheriff na kundi lake la askari Wamarekani wanaomtafuta Apache jina lake Chato aliyemuua Shariff umechukua nafasi ya mazungumzo.

Mambo haya mawili ndiyo yaliyonipelekea kurudi nyuma kuangalia upya senema niliyoiona miaka 50 iliyopita Empire Cinema na kutaka kujua kama kuna kipi naweza kufananisha kati ya kisa cha Chato ya Tanzania ya leo karne ya 21 na kwao Chato, Apache Muhindi Mwekundu aliyethubutu kumuua Sheriff katika mji wake.

Walioshuhudia ugomvi ule walisema kuwa Sheriff ndiye aliyemchokoza Chato kisa kaingia kwenye "salon" ya Watu Weupe ilhali yeye kwa upande wa mama ni Red Indian mtu dhalili hana hadhi kunywa whisky pamoja na Wazungu lau kama baba yake ni Mweupe.

Kaingia mahali si pake.
Lakini Chato akivaa nguo kama Mmarekani yeyote yule na akijihisi hivyo.

Sheriff yeye kachukizwa na kule kujifaragua huko.

Hapo ndipo ugomvi ulipoanza na kuishia kwenye kuchomoleana bastola.

Sheriff akisimama kwenye dhana kuwa pale ni kwake ana madaraka ya utawala.

Hiki ndicho kilichomponza.

Kalamu na akili ya binadamu kuna wakati vinakutana na kuhadithia hadithi moja katika miaka iliyopishana sana.

Chato huyu wa Marekani ya karne ya 19 hata kwa mbali hakupata kuwaza kuwa mkasa wake utakuja siku moja kufananishwa na kijiji chenye jina lake Afrika.

 
Watanzania,itachukua miaka 1000 mingine ili iweze kuinuka.waandishi kama Asbert ngurumo,Jesse kwaayu,wanaongozwa na njaa ya tumbo na akili,fedha wanayolipwa na Nape. Nnauye haiwezi kumaliza njaa zao,wasifikiri watanzania ni wajinga,hapana,waandishi wa hicho kitabu wao ndio wajinga na wapumbavu,kile walichokiandika,hakiwezi kuleta matokeo tarajiwa.wanapoteza mda na kujidhariridha,watanzania ukweli wanaujua kuhusu jpm kipenz Chao.

Asbert ngurumo ni mkimbizi wa mchongo.kandalasi aliyopewa na akina nape nnauye hawezi kuifikisha mahari tarajiwa,na kama anataka aone matokeo mazuri ya kazi yake,aisimame kwenye mkutano mkubwa na ayaseme hayo,kama atabaki salama.
 
Sahihi kabisa. JPM wanamchukia tu mitandaoni ambao hawafiki 5% ya watz wote.
Rest ease mzee wetu.
 
Tupo na JPM hadi mwisho wa nyakati. Mageuzi ya nchi aliyofanya JPM kizazi kijacho ndio kitajivunua na kumtambua JPM sababu itachukua muda mrefu zaidi tena kufanyika.

Kama mimi nilizikuta ndege za toka enzi ya Nyerere, na hazikununuliwa kwa miongo mitatu mpaka alipokuja Magu.

Nilikuta reli ya Nyerere na hakukuwa na reli nyingine mpaka Magu alupojenga SGR.

Nilikuta mabwawa ya umeme ya Nyerere mpaka Magu alipojenga kubwa kabisala Nyerere dam.
 
Mwendazake lilikuwa janga kubwa ambalo vizazi na vizazi hawatamsahau.
 
Itachukua pia miaka mingi bila watanzania kufungwa midomo na mfumo kandamizi kama wa Klemens Otto von Matternich.Watanzania Hata watasahau viongozi wao kupigwa risasi,kupotezwa na kukutwa wameuwawa kwenye viroba. Halikadharika kauli za kuudhi matusi na kubaguliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…