PreGE2025 CHAUMMA inatakiwa kuonewa Huruma, matapeli wa Siasa huwa hawana huruma

PreGE2025 CHAUMMA inatakiwa kuonewa Huruma, matapeli wa Siasa huwa hawana huruma

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
Wahenga walisema, ogopa sana mwanamke aliyeamua kumwacha mumewe, halafu kila siku anamsema huyo aliyekuwa mumewe. Na tena walisema, ogopa sana, na ukimbie kabisa, kama una mahusiano na mke wa mtu, halafu ukamsikia huyo mwanamke akisema kuwa anakule da sana wewe, na kwamba yupo tayari kumwua mumewe ili wewe umwoe.

Pamoja na uovu wako, lakini Ukiwa na akili, utamkimbia kabisa huyo mwanamke. Lakini ukiwa mwendawazimu, utasema huyu mke wa mtu ananipenda sana mimi, kiasi cha kuwa tayari hata kumwua mumewe, ili awe na mimi. Kwa uhayawani wako, ukakubali ushetani wa huyo mwanamke, akimwua huyo mumewe, nawe ukamchukua, hakika, atakayefuatia kuuawa na huyo mwanamke, ni wewe.

HD55, wameamua kuondoka CHADEMA, kwa sababu wamepewa ulaji, na kuahidiwa mengi, kila siku wanahangaika kuisema CHADEMA, wakiamini kwa kufanya hivyo, watazidi kumhadaa mume mpya. Wamemwahidi mume mpya kuwa wana uwezo wa kuiua CHADEMA, japo hawana uwezo huo, lakini wanaamini kwa hadaa hizo wataendelea kukomba pesa za mume mjinga.

Lakini wakikosa wanachokitarajia kwa mume moya, mume mpya ataachwa, na kusemwa vibaya, zaidi ya CHADEMA.

CHAUMMA ni ya kuhurumiwa kwa sababu haikuwatafuta HD55, na wala haijawagharamia. HD55. Hawa HD55 hata wakienda CHAUMMA, siku zote respect yao itakuwa kwa CCM, maana ndiyo inayowagharamia, na ndiyo inayowaelekeza waende wapi ili kufanikisha mission.

CHAUMMA kuwapokea HD55, ndiyo mwanzo wa mwisho wao.
 
Wale washenzi wanaingia kiprojekti tu ili kuikomoa chadema. Baadae watahama na kwenda kwa wafadhili wao.
 
Hivi mzee Hashimu Rungwe hana stress kweli? Mana yeye alikuwa amezoea ukifika uchaguzi anauza sura, sasa hao wageni siyo kikwazo kwake kutokuuza sura mwaka huu?
 
Back
Top Bottom