Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Chama kimetoa ufafanuzi rasmi baada ya kusambaa kwa barua ya kujitoa uanachama ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Bara, Ndugu Kabendera. Taarifa hiyo imeeleza kuwa Kabendera ni miongoni mwa waasisi wa Chama na alihudumu hadi Septemba 29, 2024, alipofanyiwa mabadiliko ya kiutendaji.
Baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Taarifa kwa Umma, Kabendera hakuridhika na uteuzi huo, akaacha kushiriki shughuli za chama. Pia hakuhudhuria ziara ya kichama Mbeya mnamo Februari 25, 2025, hali iliyopelekea nafasi yake kuzibwa na Ipyana Samson Njiku.
Soma zaidi: Mmoja ya waasisi wa CHAUMMA, Eugene Kabendera aachana na ubwabwa wa Rungwe, asema Chama hakiendani na maono yaliyofanya wakianzishe
Chama kimemtakia kila la heri Kabendera na kuelekeza nguvu katika maandalizi ya uzinduzi wa Operesheni Chaumma 4Change (C4C) utakaofanyika Mwanza, Juni 1, 2025.
====
Tumeona barua ya aliyekuwa Mwanachama wetu ya kujitoa uanachama, tunapenda kutoa ufafanuzi ufuatao;
1. Ni kweli kuwa ni miongoni mwa Waasisi wa Chama chetu, na ni kweli kuwa aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara mpaka tarehe 29/9/2024 kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi pale Rungwe Hotel Sinza na baada ya hapo tarehe 30/9/2024 kwenye kikao Cha Halmashauri kuu ya taifa iliyoketi pale ofisi za chama palifanyika MABADILIKO ya kiutendaji alipoteuliwa Ndugu Mohamed Masoud kuwa Katibu Mkuu taifa na Manaibu wake Faki Salum (marehemu) Zanzibar na Rahmani Rungwe Naibu Katibu Mkuu Bara
2. Ndugu Kabendera aliteuliwa kuwa mkuu wa idara ya habari na taarifa Kwa umma uteuzi ambao hakuridhika nao na kuanzia hapo alijiweka pembeni na shughuli zote za Chama na hakuwahi kufika ofisini wala kwenye tukio lolote la Chama.
3. Chama kilifanya ziara ya kichama Mkoani Mbeya tarehe 25/2/2025 na hakuhudhuria ziara hiyo wala kuitolea taarifa kwa umma kama yalivyokuwa majukumu yake.
4. Baada ya ziara hiyo Kamati kuu ilikaa mjini Mbeya na kuziba nafasi hiyo Ili shughuli za Chama ziendelee Kwa kumteua ndugu Ipyana Samson Njiku na kuthibitishwa katika nafasi hiyo tangu tarehe 25/02/2025.
Tumeona barua yake hiyo ambayo imesambazwa mtandaoni, kwa sasa tunamtakia kila jema huko aendako
Kwa sasa Chama kimewekeza nguvu zake zote kwenye tukio kubwa la uzinduzi wa Operesheni Chaumma 4
Change (C4C) itakayofanyika Mwanza tarehe 01 Juni, 2025.
Imetolewa leo Jumanne, tarehe 27 Mei, 2025.
Ipyana Samson Njiku
Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano, uenezi na taarifa kwa umma.