Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Jukwaa la Vijana la CHAUMMA limeikosoa Bajeti Kuu ya Serikali ya Sh trilioni 62.33 kwa mwaka 2026/2027, likidai ni "kiini macho" kinacholinda matumizi ya viongozi huku wananchi, hasa vijana, wakiendelea kukabiliwa na umaskini na ugumu wa maisha. Mratibu wa jukwaa hilo, Masoud Kimambo, amesema bajeti hiyo haiwezi kutatua changamoto za kiuchumi zinazowakabili wananchi wa kawaida.
"Swali la msingi; hizi fedha zinawezaje kubadilisha maisha ya kijana? Nimezunguka mikoa karibu yote Tanzania zaidi ya mara tatu, nchi ina umasikini uliokithiri usioelezeka! Mtu asiyeijua Tanzania akiambiwa rasilimali tulizonazo na akaangalia hali halisi ya uchumi, atasema hapa hakuna uongozi wa aina yoyote na serikali hii ya CCM haina mpango wowote kuweza kudeal na changamoto za watanzania," amesema Kimambo.