GE2025 CHAUMMA wasibezwe. Tujifunze kutoka kwa waingereza

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Fundi Mchundo

Platinum Member
Joined
Nov 9, 2007
Posts
13,075
Reaction score
11,682
Nawashauri wale ambao wanapata shida kusoma zaidi ya paragraph moja waishie hapa. Nilichoandika ni kijigazeti hivyo yatawatia hasira bure.

Hivi karibuni kumetokea vijimaneno vikiashiria kuwa wameishiwa pumzi na kuwa wafadhili wao wamewatema.
Kwa mtazamo wangu ni mapema mno kutangaza kifo cha Chaumma mpya.

Wiki hii aliyekuwa mbunge wa chama cha Labour, Zarah Sultana, amejitoa kwenye chama hicho na kutanguza kuwa yeye pamoja na aliyekuwa kiongozi wa chama cha Labour, Jeremy Corbyn watashirikiana kuanzisha chama kipya cha siasa ambacho ideology yake ni kushoto kwa Labour. Viongozi hawa wamejitoa Labour baada ya kufanyiwa figisu figisu nyingi na uongozi wa sasa wa Keith Starmer. Poll zimeonyesha kuwa chama hicho kama kitaanzishwa kitaweza kupata angalau 10% ya kura zote. Ushauri wanaopewa ni kuwa wasijaribu kugombea katika majimbo yote bali wajikite katika majimbo machache ambako wana nafasi kubwa zaidi ya kushinda. Hao wabunge wachache ndio utakuwa msingi wa chama hicho kuweza kuwapa ushindi mkubwa zaidi katika chaguzi zijao. Mfano mwingine unaotolewa ni wa chama cha Reform UK ambacho kilianza kama Brexit Party 2018 na hakikupata hata mbunge mmoja katika uchaguzi wa 2019. Katika uchaguzi wa 2024 kilishinda viti vitano. Katika polls za sasa hivi, Reform UK kina support kubwa kuliko Conservatives.

Kwa mifano hii, wanachama wapya wa Chaumma kuondoka Chadema hakuna tofauti na Sultana na Corbyn kuondoka Labour. Wote walifikia uamuzi huo baada ya kuona kuwa uongozi mpya hauna mpango nao. Uzoefu wao katika siasa za Tanzania na ukweli kuwa walifanya hivyo kutokana na kusimamia kile wanachoamini, future yao ni bright. Ishara nyingine ya nuru ni matamshi ya wafuasi wa chama chao cha awali kuwa hawakufukuzwa bali waliondoka kwa hiari yao. Hii ni tofauti na kelele za "good riddance" zilizokuwa zikipigwa walipotangaza kujitoa. Kipindi cha kampeni za uchaguzi kitakapoanza, hizo kelele zitazidi kubadilika.

Kwa vyovyote vile ninawapongeza kwa kusimama kidete kwenye Principles zao bila kujali kama zitawagharimu.

Amandla...
 
Kumfananisha Hashimu Rungwe Spunda mzee wa ubwabwa na Jeremy Corbyn ni kulikokosea hili jukwaa heshima.
 
Hakuna chama hapo mimi ni THE GREAT GENIUS NINAYE ZUNGUMZA chauma hakipo hata katika hatua ya kufa maana akijawai kuwa hai ni chama mfu na kiliundwa kiwe hivyo na ccm
 
Wakati mwingine ni heri unyamaze tu. Wapi nilipomfananisha Hashimu Rungwe na Jeremy Corbyn? Hashimu Rungwe ametoswa na chama kipi kama alivyotoswa Corbyn? Watu kama nyie ndio mnalivunjia heshima JF kwa kurupuka kujibu swali ambalo hata halijaulizwa. Punguzeni uchawa. Someni, mtafakari ndio mjibu. Ndivyo tulivyokuwa tunafanya wakati wa JF ya zamani.

Amandla...
 
Back
Top Bottom