GE2025 CHAUMMA yaahidi kuondoa njaa na magonjwa ya lishe

GE2025 CHAUMMA yaahidi kuondoa njaa na magonjwa ya lishe

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
Mtiania mwenza wa urais wa Tanzania kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Devotha Minja amesema chama hicho kimejipanga kuhakikisha kila Mtanzania anapata lishe bora kupitia mpango wao wa “ubwabwa kwa wote”.

Mpango huo, amesema, unalenga kuondoa njaa na kupunguza magonjwa yanayohusiana na lishe nchini.

Soma pia: Salum Mwalimu mgombea urais na Devotha Minja mgombea mwenza kupitia CHAUMMA



“Chama chetu kinataka kila Mtanzania awe na chakula cha kutosha na lishe bora, ili kuimarisha afya na ustawi wa taifa letu,” amesema Devotha
Devotha ameyasema hayo leo Jumatano, Agosti 20, 2025, wakati akizungumza katika ziara ya kutafuta wadhamini wa mtiania wa urais, Salum Mwalimu, Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.
 
Hii Slogan ilikuwa nzuri na kuvutia Chini ya Mzee Hashimu Rungwe, sio Kwa Hawa matapeli waliovamia chama chetu.
 
Back
Top Bottom