Mtiania mwenza wa urais wa Tanzania kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Devotha Minja amesema chama hicho kimejipanga kuhakikisha kila Mtanzania anapata lishe bora kupitia mpango wao wa “ubwabwa kwa wote”.
Mpango huo, amesema, unalenga kuondoa njaa na kupunguza magonjwa yanayohusiana na lishe nchini.
“Chama chetu kinataka kila Mtanzania awe na chakula cha kutosha na lishe bora, ili kuimarisha afya na ustawi wa taifa letu,” amesema Devotha
Devotha ameyasema hayo leo Jumatano, Agosti 20, 2025, wakati akizungumza katika ziara ya kutafuta wadhamini wa mtiania wa urais, Salum Mwalimu, Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.