CHAUMMA yamvua rasmi u-Katibu Mkuu Salum Mwalimu

Wanarudia makosa yale yale ya vyama vyote vya siasa Tanzania. Wangempa nafasi ya kujitetea kabla hawajamuondoa kwenye cheo chake. Ndio mwanzo wa kupelekana Mahakamani na kukivuruga chama chao. Kitakachofuata ni kundi Mwalimu likipinga hatua hiyo.

Amandla...
 
Umasikini wa roho,ni ugonjwa mkubwa sana na mbaya sana kwa hivi vyama masikini!. Kosa la Salum Mwalimu ni,baada ya kupewa gari VXR ya serikali wakati wa uchaguzi,baada ya uchaguzi,aliendelea kuonekana na VXR sasa anaendesha mwenyewe!,kwanza walimtuhumu kuiba gari la tume,walipogindua kuwa ni lake,wanataka maelezo kapata wapi fedha wakati Chauma ni apeche alolo,wanadhani ni fedha za chama chao Salum kawaibia
View: https://youtu.be/pKurLGCz14Y?si=TeE2xh2x1IgCnrWt ,kumbe kainunua kwa pesa yake ya mfukoni!

P
 
Aende mahakamani kwani kafukuzwa uanachama, ukatibu ni cheo cha kuteuliwa bosi akiona hufai anakuondoa mda wowote.
 
Magari ya tume walikubaliana wauziwe watu binafsi? Na kumbuka ile ni mali ya umma je unaiuza kama kitu chakavu wakati kimetembea muda mfupi tu na kilometa chache au unaiuza kwa thamani ipi halisi?

Hawa wahuni kina Sista Nyahoza na wazenji kuna ujinga mwingi wanatufanyia.
 
Hiyo ni nafasi ya kuteuliwa , mamlaka ya uteuzi kama unaona hutoshi tena kwenye nafasi hiyo inakuondoa. Hapo ndiyo imeisha hiyo atulie awekeze tu hela aliyovuna aachane na siasa au amfuate mke wake huko CCM kama alivyofanya Bananga.
 
Kama kuna Mtu aliamini Salum Mwalimu siyo Dalali pole yake.
 
Sasa rudi kizimkazi ukavue pweza,kamba na mkizi,Chadema sidhani kama mlango upo wazi bado kwako,labda iwapo hutaki kurudi kizimkazi jaribu geti la kijani.
 
Kosa lingine ni kupora mke wa mwanachama wake
 
Kwa vile drama ni part ya maisha yao, ngoja tusubirie kitachojiri labda wanataka kuchezesha watu akili
 
Aende mahakamani kwani kafukuzwa uanachama, ukatibu ni cheo cha kuteuliwa bosi akiona hufai anakuondoa mda wowote.
Hakuna sheria inayo mzuia kwenda Mahakamani kama anaona hakutendewa haki. Ingekuwa hawajaongelea mambo ya ubadhirifu angeweza kumezea. Hili la kumchafua hataliachia.

Wangemkubalia ombi lake la kukaa pembeni wakati wanafanya uchunguzi. Hapakuwq na haja ya ubabe.

Ni yale yale ya jamaa wa Zanzibar walivyoisumbua Chadema.

Amandla...
 
Masuala ya siasa we mgeni, kavuliwa ukatibu aende mahakamani? labda akafungue kesi ya jinai kusingiziwa kuiba mali za chama au kudhalilishwa defamation case lkn sio kurudishiwa ukatibu.

Ya Zanzibar ni tofauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…