Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu, amepokea rasmi mapendekezo ya sifa na vigezo vya wanawake wa chama hicho wanaotarajiwa kuteuliwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi kupitia viti maalum katika uchaguzi ujao.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam siku ya Alhamisi mara baada ya kupokea mapendekezo hayo, Mwalimu amesema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa chama kuhakikisha wanawake wanashirikishwa kikamilifu katika uongozi, sambamba na kuzingatia uwiano wa kijinsia kama ilivyoainishwa kwenye katiba ya chama na miongozo ya kitaifa.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Mapendekezo hayo yamewasilishwa kwake na Katibu wa Kamati Maalum ya Viti Maalum, Bi. Moza Ally, aliyeteuliwa na Mwalimu mwenyewe kuongoza mchakato huo wa ndani kwa lengo la kuweka misingi madhubuti ya uteuzi wa wanawake wenye uwezo, maadili na uadilifu wa kutumikia wananchi kupitia vyombo vya uongozi.