GE2025 CHAUMMA yawasha moto Same Magharibi urejeshaji fomu za watia nia

GE2025 CHAUMMA yawasha moto Same Magharibi urejeshaji fomu za watia nia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Mkoani Kilimanjaro kimezindua ofisi zake za Jimbo la Same Magharibi Mkoani humo sambamba na kuanza kupokea fomu za watiania walioomba ridhaa ya kuchaguliwa kugombea nafasi ya Ubunge

Akizungumza Agosti 13, 2025 wakati akirejesha fomu ya kuwania ubunge Jimbo la Same Magharibi Gervas Mgonja amesema kuwa Jimbo hilo linakabiliwa na ukosefu wa ajira kwa vijana, miundombinu ya barabara, huduma duni za afya, elimu,maji na ukosefu wa fursa sawa za kiuchumi hivyo ni wakati wa chama hicho kukomboa haki za wananchi na kuweka mazingira mazuri ya maendeleo



 
Subirini matusi sasa,kuna watu wanaamini wao ndio wako sawa tu!!
 
Back
Top Bottom