Che Guevara alikaa Tanzania miezi mitano

Che Guevara alikaa Tanzania miezi mitano

Dhafir

Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
97
Reaction score
123
Eduardo Mondlane (mwanzilishi wa chama cha kupigania uhuru Msumbiji cha FRELIMO akiwa na Ernasto Che Guevara katika ofisi za FRELIMO jijini Dar es salaam mwaka 1966. Che Guevara alikuwepo Dar es salaam kwa miezi 5 kati ya mwaka 1965 hadi 1966. Akiwa Dar es salaam Che Guevara alitumia jina la siri ( code name) '' TATU '' ni jumla ya herufi katika jina C, H, E (CHE).

Alikuwa mteja wa mara nyingi katika mgahawa wa Zahir ulipo katika mtaa wa msikiti jijini Dar es salaam ( mgahawa huo bado upo) na aliishi katika ubalozi wa Cuba, kutoka Dar es salaam, Che Guevara alielekea Congo. Eduardo Mondlane aliuwawa kwa bomu jijini Dar es salaam ambalo lilitegwa katika kitabu alichotumiwa toka Ujerumani Magharibi na alizikwa makaburi ya kinondoni.

Nafasi yake ya uongozi wa FRELIMO ili chukuliwa na Samoa Machel
 
Attachments

  • 1425126463883.jpg
    1425126463883.jpg
    48.8 KB · Views: 1,535
Mleta mada Kuna mzee wangu mmoja anakaa
Mikocheni pale azura anamjua vizuri mondlane
Maana mpaka tukio lile la kulipukiwa na bomu wakati huo walikuwa ma jirani.
Ukitaka stori za mondlane anazo nyingi. Kweli mleta mada hii umenigusaaa jamaa alikuwa shujaa
 
Eduardo Mondlane (mwanzilishi wa chama cha kupigania uhuru Msumbiji cha FRELIMO akiwa na Ernasto Che Guevara katika ofisi za FRELIMO jijini Dar es salaam mwaka 1966. Che Guevara alikuwepo Dar es salaam kwa miezi 5 kati ya mwaka 1965 hadi 1966. Akiwa Dar es salaam Che Guevara alitumia jina la siri ( code name) '' TATU '' ni jumla ya herufi katika jina C, H, E (CHE). Alikuwa mteja wa mara nyingi katika mgahawa wa Zahir ulipo katika mtaa wa msikiti jijini Dar es salaam ( mgahawa huo bado upo) na aliishi katika ubalozi wa Cuba, kutoka Dar es salaam, Che Guevara alielekea Congo. Eduardo Mondlane aliuwawa kwa bomu jijini Dar es salaam ambalo lilitegwa katika kitabu alichotumiwa toka Ujerumani Magharibi na alizikwa makaburi ya kinondoni. Nafasi yake ya uongozi wa FRELIMO ili chukuliwa na Samoa Machel
Ndomana mpaka sasa msumbiji wanaitaka Ile nyumba aliyofia mondlane ambayo kwa sasa inamilikiwa na tajiri wa kihindi murtaza
 
Jamani huyu CHE alikuwa akienda popote duniani penye harakati za ukombozi au ilikuwaje?
 
Che alishiriki katika mapambano sehemu nyng ya dunia ukianzia Cuba, Congo na baadh ya maeneo na akafia ktk kuikomboa Bolivia
 
Mleta mada Kuna mzee wangu mmoja anakaa
Mikocheni pale azura anamjua vizuri mondlane
Maana mpaka tukio lile la kulipukiwa na bomu wakati huo walikuwa ma jirani.
Ukitaka stori za mondlane anazo nyingi. Kweli mleta mada hii umenigusaaa jamaa alikuwa shujaa

Mkuu unaweza ukamuuliza story zake ukazimwaga humu? Hiyo nyumba ipo maeneo gani alipofia Eduardo Mondlane?
 
Mkuu unaweza ukamuuliza story zake ukazimwaga humu? Hiyo nyumba ipo maeneo gani alipofia Eduardo Mondlane?

Hiyo nyumba iko mikocheni daraja la mlalakuwa kama inaelekea kawe unaingia kuliaa nyumba hiyo inangalia beach.
Nyumba ya mzee wangu huyo iko kushoto ambayo sahv ni azura club
 
Mkuu unaweza ukamuuliza story zake ukazimwaga humu? Hiyo nyumba ipo maeneo gani alipofia Eduardo Mondlane?

Dah huyo mzee ana stori nyingi sana, mkuu hyo nyumba tangu afe mondlane haikaliki
maana tangu nyumba hyo itoke mkononi mwa
Wamozambiq kuwa ya watu binafsi wenye nyumba wanauza, isha milikiwa na watu wengi mfano konyagi washaitumia wakaiuza,
Akanunua mama mmja wa kihaya akaiuza, greenlandbank nao washaimiliki wakaiuza, Reginald mengi ashakuwaga na ofisi alipanga aliondoka, sahv kainunua mhindi murtaza ndpo wametokea serikali ya msumbiji wanaitaka nyumba yao iwe sehemu ya kumbukumbu yao ya mondlane
 
Alitoka Congo ndo akaja tz..
Alishindwana na wakongo kutokana na tabia yao ya kuendekeza anasa hata kwenye issue serious,che aliwahi kuelezea kuwa wakati alipokuwa msituni kongo akiwafunda askari wa ki mapinduzi,ilipofika jioni wale askari walimtaka waagane ili waende mjini kuserebuka kusaka mademu!! Che akaona hawa viumbe bado hawajahitaji mapinduzi ki ukweli,hivyo akaachana nao na ndipo alipopitia TZ on the way kurudi zake kwao,pia alipitia zanzibar, NB hata wakati alipokuwa safarini kuelekea huko congo alipitia hapa pia.
 
Yeah..jamaa alisema wakongo hawakuwa tayari kwa mapinduzi..
 
#CHE :- Ni jina la Asili kutoka kabila la Watu wa kusini mwa Tz yani #Wayao ambao hutumia #CHE maana yake Mwenye kumiliki ambao hao Wayao ki Asili ni watu kutoka Mozambique yaani Msumbiji kwa hyo ni mule mule na mleta Thread
 
Back
Top Bottom