Che Guevara alikaa Tanzania miezi mitano

CHE alikuwa mkombozi Wa kweli alikataa kuwa PM Wa Cuba na kuendelea NA ukombozi mpaka US army NA CIA wakamuua

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Kumbukumbu mujarab

Ernasto Rafael Guevara de la Serna au maarufu kwa jina la Che Guevara. Alizaliwa tarehe 14 Mei 1928 huko Rosario, Argentina; na kufariki tarehe 9 October 1967 huko la Guera, Bolivia. Alikuwa ni msomi mwenye taaluma ya udaktari alihitimu mafunzo yake ya udaktari mwaka 1953. Alikuwa sio raia wa Cuba kwa kuzaliwa lakini alikuwa ni mmoja wa viongozi wa nchi ya Cuba. Hakuwahi kuwa mwanajeshi ila alikua mfuasi wa itikadi za kisoshalist za Carl Marx na alipata mafunzo ya kijeshi kwa ufupi kupitia kwa mwanamapinduzi Fidel Castro.

Che anajulikana zaidi kwa harakati zake za kimapinduzi dhidi ya tawala za kibepari huko Amerika ya Kusini na hapa kwetu Africa. Wakati akisoma Che alizunguka katika nchi mbalimbali za Amerika ya Kusini ambapo alijionea jinsi gani umaskini ulivyokithiri.alisikikitishwa na hilo huku akiwaona wananchi wengi wakiathirika huku wachache wakinufaika na mali za nchi hizo. Aliwaza na kufikiri njia pekee ya kubadilisha hali hiyo ni mapinduzi; na ndipo alipoamua kuzisoma kwa undani falsafa za Carl Marx na baada ya hapo alijihusisha na harakati za kisoshalist. Akiwa kijana wa miaka 24 alivutiwa na taarifa za kuwepo kwa kijana mwenzake alieko huko Cuba akijulikana kwa jina la Fidel Castro, ambaye ni mwanajeshi muasi aliekuwa na itikadi kama zake za kijamaa aliyeamua kupigana na majeshi ya serikali ya Rais Batista huku yeye akiwa na jeshi dogo.
 
Comrade Ernesto Guevara Lynch in Congo then to Tanzania before leaving to Guatemala
 
Attachments

  • 1425188768776.jpg
    1425188768776.jpg
    13.8 KB · Views: 675
  • 1425188784942.jpg
    1425188784942.jpg
    17.4 KB · Views: 311
  • 1425188799648.jpg
    1425188799648.jpg
    38.2 KB · Views: 291
Kuna tetesi nyingne kwamba Mapinduzi ya Zanzibar(1964) yalikua na mkono wa Che..kwaajili ya usiri mkubwa wa hiyo mission haikuweza kuwa documented.

Huko Congo alichemka baada ya kumkuta Laurent Kabila akiwa anapenda sana kula bata na kuserebuka na totoz kila siku..
 
Hii kuwa mkono wake katika mapinduzi ya Zanzibar haina ukweli ndugu yng, kwasabb Che alikuja akakuta Tanzania ishaungana na Zanzibar, maana yake ni kuwa mapinduzi yalifanywa kabla ya kuja Che
 
Ernasto Rafael Guevara de la Serna au maarufu kwa jina la Che Guevara. Alizaliwa tarehe 14 Mei 1928 huko Rosario, Argentina; na kufariki tarehe 9 October 1967 huko la Guera, Bolivia. Alikuwa ni msomi mwenye taaluma ya udaktari alihitimu mafunzo yake ya udaktari mwaka 1953. Alikuwa sio raia wa Cuba kwa kuzaliwa lakini alikuwa ni mmoja wa viongozi wa nchi ya Cuba. Hakuwahi kuwa mwanajeshi ila alikua mfuasi wa itikadi za kisoshalist za Carl Marx na alipata mafunzo ya kijeshi kwa ufupi kupitia kwa mwanamapinduzi Fidel Castro.

Che anajulikana zaidi kwa harakati zake za kimapinduzi dhidi ya tawala za kibepari huko Amerika ya Kusini na hapa kwetu Africa. Wakati akisoma Che alizunguka katika nchi mbalimbali za Amerika ya Kusini ambapo alijionea jinsi gani umaskini ulivyokithiri.alisikikitishwa na hilo huku akiwaona wananchi wengi wakiathirika huku wachache wakinufaika na mali za nchi hizo. Aliwaza na kufikiri njia pekee ya kubadilisha hali hiyo ni mapinduzi; na ndipo alipoamua kuzisoma kwa undani falsafa za Carl Marx na baada ya hapo alijihusisha na harakati za kisoshalist. Akiwa kijana wa miaka 24 alivutiwa na taarifa za kuwepo kwa kijana mwenzake alieko huko Cuba akijulikana kwa jina la Fidel Castro, ambaye ni mwanajeshi muasi aliekuwa na itikadi kama zake za kijamaa aliyeamua kupigana na majeshi ya serikali ya Rais Batista huku yeye akiwa na jeshi dogo.
Uyu jamaa nilikuwa namkubali sana,mwanamapinduzi halisi.Nina noti ya Cuba INA picha yake.
 
Mdau asante, nashauri ui-scan hiyo noti na uibandike ili nasi ambao hatujawahi kufika Cuba tujioneee!!!
 
Hii kuwa mkono wake katika mapinduzi ya Zanzibar haina ukweli ndugu yng, kwasabb Che alikuja akakuta Tanzania ishaungana na Zanzibar, maana yake ni kuwa mapinduzi yalifanywa kabla ya kuja Che

Katika siku ya kuazimisha mapinduzi ya zanzibar..February 12 1965..Che alikua mgeni rasmi na katika speech yake alisema ""Zanzibar is our friend and we gave them our small bit of assistance, our fraternal assistance, our revolutionary assistance at the moment when it was necessary"
 
Kwa muda huo aliweka makazi yake mafupi siku za wiki end katika kijiji cha Kaole (Makaz<i yako kwenye shule ya Kaole Sec)pembezoni mwa mji wa Bagamoyo enzi hizo ukijulikana kama Bwagamoyo...
 
Back
Top Bottom