sasa huku ndio nini ikiwa habari zipo kwenye kijarida na kijarida ni cha bure ,hapo peke yake kumetanuka wigo wa habari ,aidha ikiwa kijarida kimebeba habari nyepesi au nzito kama wananchi hawatatumia redio kifua kueneza habari hizo nguvu ya kudai kioja hicho kijadiliwe kitaifa itakuwa chini ni lazima hiyo hadi kopi iwekwe hapa kwa wale wasio na ubavu wa kukipata hicho kijarida bila ya shaka yeyote watajisomea na hivyo upo uwezekano wa kuwaamsha ndugu na jamaa zao waliolala na mazingahombe ya EPA kuwa kuna mbuzi mwengine ameanza kupigiwa gitaa ,weka hizo nyaraka hapa ,yaani tunaweza kuziita nyaraka za JF. Au bado mnahogopa ,jamani dunia ya leo si ya kuogopana tumaamini kabisa wenye madaraka wamewekwa na sisi wapiga kura kama ni hivyo tusione taabu kuwatolea uvivu.
Maana kama mkuu wa jeshi kuna ushahidi alikuwa anajilimbikia mabilioni kwa njia ya wizi wakati askari wake wanavaa ndara na hata wanapostaafu bado huwa wanababaika,yaani nilimkuta Kapteni wa Jeshi ambae wakati nikiwa kazini alikuwa rafiki yangu mkubwa sana kikazi na tukifahamiana tu japo yeye alikuwa mkiristo na mimi ni muisilamu ,lakini dini zetu hazikutufanya tuwe na mirengo mikali kiuhusiano.
Mimi niliacha kazi baada ya kupata matatizo ambayo yalinikuta tukiwa kwenye mazoezi ya risasi za moto na hivyo sikuweza na sikuruhusika kuendelea tena kwani kiafya nilikosa sifa za kuendelea na hata yeye alinishauri nirudi uraiani kwani kuendelea huko ni kujizidisha madhara ,kwa ufupi nilitakiwa niwe mwenye kutulia na kutofanya harakati zozote za nguvu,nilitenguka tindi ya mgongo wakati tukipakia zana nzito kwenye gari na hapo ndipo ulipokuwa mwisho wa shughuli zangu za kijeshi ,ingawa madaktari walifanikiwa kunisaidia na walisema niliwahi kukurupuka ndio athari hazikunilemaza.
Okay baada ya hapo na miaka kupita kwa bahati nilikutana na yule kapteni ambae alikuwa mkuu wangu wa kazi na bosi ,nilishangaa sana nilivyomkuta anaendesha baiskeli na viatu ni kanda mbili zilizokwisha kabisa na hana hata nyumba ya maana ,nilipomuuliza aliniambia amestaafu lakini baada ya hapo hakuweza tena kupata ushirikiano wa kutoka kazini,na alizidi kueleza kuwa kinachowafanywa wawe wanahangaika ni mpangilio mzima wa kikazi huwa hauna mshiko wa kuweza kufanya kitu cha baadae muda wote unakuwepo kambini na familia yako na huna maisha ya uraiani.Hivyo wanashindwa hata kujiendeleza kwa maisha ya kustaafu inakuwa kama ni watu wepya kwenye jamii yao ya kijijini.