Msanii Cheedy hivi karibuni Konde Kang walivunja mkataba nae ikalazimika imlipe million 10 kama sehemu ya kuvunja mkataba.
Wakati akihojiwa na East Africa Radio, Cheedy amefunguka kuwa; "Mkataba waliotengeneza Konde Gang hauendani na uwekezaji wanaouweka kwa sisi wasanii. Haiwezekani uweke kipengele cha kuvunja mkataba nao ni lazima ulipe billion 1 wakati hakuna uwekezaji wa maana uliyoweka ufanye ulipe hiyo hela.
"Nilitegemea vitu vingi, nashangaa kwa muda wote niliyokuwa pale sijapata hata promotion yakuweleweka yakufanya niuze kazi zangu."