Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
CHEGE CUP NGAZI YA MKOA KUANZIA KUTIMUA VUMBI DESEMBA 2023 NDANI YA WILAYA YA RORYA MKOA WA MARA
"Nimeamini tunaweza kutengeneza timu nzuri sana ya Wilaya ya Rorya na tukashindana kokote. Michezo ya leo siyo mwisho, lengo ni kukimbizana na Michezo ya Fainali ambayo tunaenda kuandaa Chege Cup kwaajili ya Mkoa wa Mara" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya
"Niliona Ili tuweze kupata timu ya Wilaya nianzishe ligi ya Chege Cup kuanzia chini ngazi ya Kata na Mashindano yakaanza ndani ya Kata, mkaenda kwenye Tarafa, tukapata washindi wa kuja ngazi ya Wilaya yaani Robo Fainali, tukaingia mshindi wa tatu na leo tumeingia Fainali" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya
"Lengo ni kutafuta vipaji vyote vinavyoanzia ngazi ya Kata na tunapounda timu ya Wilaya tuwe tumechukua kwenye Kata zote bila kuchukua wachezaji kutoka eneo moja. Ninaamini wachezaji 45 watakaotajwa leo wanakwenda kutengeneza mfumo mzuri ambapo tutawachuja tupate wachezaji 25" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya
"Desemba 2023 nitaweka Chege Cup ya Mkoa wa Mara nishirikishe Wilaya zingine waje wacheze Rorya kwa kushirikiana waje wacheze na sisi tukiwa tumeandaa timu ya Wilaya. Tutaendelea kusajili endapo kuna kijana mwenye uwezo mzuri tutamuita kwenye kambi" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya
"Mimi nitatoa Kombe la Mkoa ambapo litachezewa Wilaya ya Rorya, siwezi kutoa Kombe bila kujua wachezaji wanatoka wapi. Hatukutaka kuchagua wachezaji wanaotoka Tarafa Moja, tunataka tuwe na wachezaji kutoka Tarafa zote halafu tuunde timu ya Wilaya kisha tukashiriki Michezo" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya
"Tuliandaa zawadi, mshindi wa nne atapewa 200,000; mshindi wa tatu atachukua Ng'ombe mmoja; mshindi wa pili ataondoka na Ng'ombe wawili; Mshindi wa kwanza atachukua Ng'ombe watatu. Hakuna aliyekuja kushiriki Michezo hii atakayeondoka bure" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya