Cheka: Sijapigwa India

AKILI TATU

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2016
Posts
2,659
Reaction score
2,827
Bondia Mtanzania Francis Cheka ambaye mwishoni mwa wiki alipoteza pambano lake nchini India alilopigana na raia wa nchi hiyo Vijender Singh, ameibuka na kusema kuwa mpinzani wake huyo hakumpiga, ila alibebwa na mwamuzi


Akizungumza kwa njia wa simu kutoka nchini India, Cheka amesema katika raundi hiyo ya tatu, alipata tatizo katika kifaa chake cha kulinda meno kwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na kikohozi, na wakati anakifanyia marekebisho, ndipo mwmuzi akatangaza mshindi, bila kumuuliza Cheka mwenyewe kama alikuwa anaendelea au la.


Pia Cheka amekanusha taarifa za kuwa amlipoteza pambano hilo kwa kuwa akili yake ilikuwa katika pambano lililoko mbele yake dhidi ya Dulla Mbabe.
 
Reactions: MC7
Cheka analeta Porojo tu. Yeye, Akubali kuwa alipigwa, mbona kawaida tu!
Video hii hapa:
 
Cheka analeta Porojo tu. Yeye, Akubali kuwa alipigwa, mbona kawaida tu!
Video hii hapa:
Miaka ya nyuma kabla ya teknolojia hii timu zetu za mpira zikienda nje basi huja na lundo la malalamiko mara walichezeshwa uwanja una maji mkiwauliza wenzenu walikuwa samaki ?mara ooh hatukwenda na viatu vinavyohimili hali ya maji unawaza unakwenda vitani na manati tu? sasa ndio haya au labda lugha?
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji15][emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Akubali tu kashindwa na amita bacha' hapo atakua kishachochea pili pili kichaa fanya mchezo nini..ve keval sveekaar karane ke lie makka ke lie ek achchha ek hai, to agale doosara vah paagal nahin hai shachhochhai viphal raha hai ..
 
Aisee sisi ni wabishi yani kitu kimechezwa live lakin jamaa bado anabisha sijui ingekua wamepigiana vichochoroni angesemaje.

Ndo maana michezo mingi tunashindwa baada ya kujipanga upya anaanza sound nyingi,njoo pale taifa stars timu inapigwa 7 kocha anasema wachezaji wamecheza vizuri sana...tubadilike
 
Tyson alikuwa ataki upuuzi kama huu, dawa ya mchezo wa box ni kumtwanga mtu KO tu basi kuzima ubishi, hizi TKO au ushindi wa point ndio uleta porojo nyingi.

Huyu Cheka alishachezeaga kichapo Diamond jubilee ajabu akaja kupewa yeye ushindi wa point.
 
Mbn kwenye video tumeona waz jamaaa akimtandika huku akiweka na machejo?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] cheka bwana
 
Kwahiyo video yake ni ya uongo?!yani tumeona akifuatwa na muamuzi akiulizwa na anakubali mwamuzi anamaliza pambano yeye anajifanya mdosi alibebwa?!


Uongo huo wenzie walikuwa wanafanya kipindi hiko teknolojia hamna hatuoni mapambano ya nje sio sasa
 
Ila mim sjaelewa pambano limeishaje hapo na jamaa kapigwaje? Wataalam wanisaidie kdogo
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji15][emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
Kulikuwa na vituko vingi sana miaka hiyo watakuja na kusema ooh taa zilizimwa uwanjani mnawauliza wenzenu walikuwa bundi? jibu hakuna tuache Porojo mambo yamebadilika. Nakumbuka enzi hizo gor mahia na afc leopards zipo vizuri Kenya walikuwa wakienda nje wanachezea kichapo sasa wamepeleka mtangazaji nae kauzu utasikia redioni "baba moi Kenya inaonewa huku "kumbe wapi!
 
watalaamu hebu nisaidieni hapo ni kuna ngumi kadhaa kapigwa lakini jinsi pambano lilivyoisha sijaelewa kidogo hapo nami nimepata shaka hebu tuwe wachinguzi wakati mwingine
 
Huyu Dulla Mbabe anachapa ngumi huyu dg hatar... Hebu tusubir
 
Reactions: MC7
Tukiacha uswahili nchi yetu itapiga sana hatua
 
Tukiacha uswahili nchi yetu itapiga sana hatua
Visingizio unadhani tumekutana navyo barabarani? ni vya kurithi kuna waqt timu yetu moja ilikwenda nje basi walivyorejea na kusema mji waliotakiwa kwenda kama iringa wenyewe wakapelekwa kigoma baadae ndio wanaambiwa kuwa huo sio mji wanaotakiwa wacheze sasa fikiria mziki wa gari toka kigoma mpaka iringa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…