Cheka: Sijapigwa India

Cheka: Sijapigwa India

Mbona sijaelewa pia namna pambano lilivyohitimishwa?.
Mbona kama kimizengwemizengwe tu.
 
Hiyo inaitwa TKO cheka alikataa kuendelea na pambano ukiangalia kwa uhalisia nilikua naona pambano kama 50 50 lakin cheka alipo kwenda kwenye kona hapo namuona na promota j msangi kama second wake hakukua na ngumi kali iliyo sababisha cheka kuacha pambano oll in oll mabondia wetu wengi wanapo kwenda nje huuza mapambano ili kuwatengenezea record mabondia pinzan
 
Bondia Mtanzania Francis Cheka ambaye mwishoni mwa wiki alipoteza pambano lake nchini India alilopigana na raia wa nchi hiyo Vijender Singh, ameibuka na kusema kuwa mpinzani wake huyo hakumpiga, ila alibebwa na mwamuzi

Akizungumza kwa njia wa simu kutoka nchini India, Cheka amesema katika raundi hiyo ya tatu, alipata tatizo katika kifaa chake cha kulinda meno kwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na kikohozi, na wakati anakifanyia marekebisho, ndipo mwmuzi akatangaza mshindi, bila kumuuliza Cheka mwenyewe kama alikuwa anaendelea au la.

Pia Cheka amekanusha taarifa za kuwa amlipoteza pambano hilo kwa kuwa akili yake ilikuwa katika pambano lililoko mbele yake dhidi ya Dulla Mbabe.
Huyu kila akipigwa lazima alete visingizio vya kuonewa.
 
Malipo ni hapahapa duniani yeye mwenyewe alidundwa hapa dar na bado akatangazwa kashinda
 
  • Thanks
Reactions: MC7
watalaamu hebu nisaidieni hapo ni kuna ngumi kadhaa kapigwa lakini jinsi pambano lilivyoisha sijaelewa kidogo hapo nami nimepata shaka hebu tuwe wachinguzi wakati mwingine
Zile ngumi zilipoingia "TEETH PROTECTOR" ilianguka .. Ukicheki vizuri hata bondia mhindi alikuwa anamuonesha refa ishara kuwa Cheka hana kilinda Meno.... Sasa Cheka nafikiri akaenda kwenye Kona yake kuwaambia Bila kumwambia refa.. Refa akahisi Cheka hajiwezi... Akamfata... Nafikiri hapo tatizo kubwa ni lugha... Alishindwa kuwasiliana na refa
 
Bondia Mtanzania Francis Cheka ambaye mwishoni mwa wiki alipoteza pambano lake nchini India alilopigana na raia wa nchi hiyo Vijender Singh, ameibuka na kusema kuwa mpinzani wake huyo hakumpiga, ila alibebwa na mwamuzi

Akizungumza kwa njia wa simu kutoka nchini India, Cheka amesema katika raundi hiyo ya tatu, alipata tatizo katika kifaa chake cha kulinda meno kwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na kikohozi, na wakati anakifanyia marekebisho, ndipo mwmuzi akatangaza mshindi, bila kumuuliza Cheka mwenyewe kama alikuwa anaendelea au la.

Pia Cheka amekanusha taarifa za kuwa amlipoteza pambano hilo kwa kuwa akili yake ilikuwa katika pambano lililoko mbele yake dhidi ya Dulla Mbabe.
Dunia hii ya leo ni kijiji uongo wa namna huo hauendani na wakati. Huyu bwana amepigwa nadhani hata yeye moyoni anajua hivyo kwani hata kujitayarisha kwake kwa pambano hilo ilikuwa inaonyesha huyu bwana anakwenda kule kuvuta mkwanja tuu na siyo kupigana. Hivi sasa jamaa anatafuta visingizio ili asipigane leo eti anadai pesa za pambano hilo wakati wa kupima uzito wakati inaeleweka[naye alikwisha saini makubaliano kuwa apewe advansi [4m] na hizo alipewa na nyingine ni baada ya pambano. Mimi ushauri wangu kwa huyu bwana ni kwamba aendelee na biashara yake ya chupa za plasitic kwani wakati umempita na kuna vijana hawana adabu ambao wanaweza kumuadhiri.
 
Zile ngumi zilipoingia "TEETH PROTECTOR" ilianguka .. Ukicheki vizuri hata bondia mhindi alikuwa anamuonesha refa ishara kuwa Cheka hana kilinda Meno.... Sasa Cheka nafikiri akaenda kwenye Kona yake kuwaambia Bila kumwambia refa.. Refa akahisi Cheka hajiwezi... Akamfata... Nafikiri hapo tatizo kubwa ni lugha... Alishindwa kuwasiliana na refa
angalau naweza kukubaliana nawe maana watu hawaangalii vema hii video.
 
Zile ngumi zilipoingia "TEETH PROTECTOR" ilianguka .. Ukicheki vizuri hata bondia mhindi alikuwa anamuonesha refa ishara kuwa Cheka hana kilinda Meno.... Sasa Cheka nafikiri akaenda kwenye Kona yake kuwaambia Bila kumwambia refa.. Refa akahisi Cheka hajiwezi... Akamfata... Nafikiri hapo tatizo kubwa ni lugha... Alishindwa kuwasiliana na refa
hapo nakubali, maana naona watu wavivu kuangalia kwa umakini
 
Sijaupenda mchezo wa Cheka kwa kweli. Sasa sijui anaji-guard vipi, halafu kaweka mguu wa kushoto mbele. Gabacholi anamtandika badala ya kubadilisha mguu anainama na kupiga hewa, si ndio anapoteza pumzi bure tu. Cheka hana techniques za kimchezo, abaki kuwapiga mabaa medi, kaniudhi kweli kweli.
 
Tyson alikuwa ataki upuuzi kama huu, dawa ya mchezo wa box ni kumtwanga mtu KO tu basi kuzima ubishi, hizi TKO au ushindi wa point ndio uleta porojo nyingi.

Huyu Cheka alishachezeaga kichapo Diamond jubilee ajabu akaja kupewa yeye ushindi wa point.
Nakumbuka hilo pambano alipigwa ila akabebwa, Pia Ni Kawaida yake kulalamika
 
Kwahiyo video yake ni ya uongo?!yani tumeona akifuatwa na muamuzi akiulizwa na anakubali mwamuzi anamaliza pambano yeye anajifanya mdosi alibebwa?!

Uongo huo wenzie walikuwa wanafanya kipindi hiko teknolojia hamna hatuoni mapambano ya nje sio sasa
Labda anadhani hakuna aliyeona video he he he he
 
Angalieni video vizuri... Kama unataka kutoa hoja.... Angalia vizuri video iliyopostiwa..... Tatizo nililooona ni NI LUGHA NA KANUNI....
 
Back
Top Bottom