Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Batshuay ni forward nzuri sema anapewa nafasi ndogo.
 
Kwa mpira waliocheza ajax,bora kukutana na Barcelona kuliko Ajax.
Nisijue ni uzuri wao au ni ubovu wetu!!.
 
Batshuay ni forward nzuri sana kuliko Tammy ,pia hapewi sana nafasi kama Abraham.
Mo sarah alipokuwa Chelsea alikuwa akipigwa benchi. Kila kocha anamtu wake.
I'm sure mpaka msimu uishe ubora wa batshuay utakuwa ushaonekana.
 
Penalti 2, red card 2 aiseeeee kuna timu zinatembelea nyota balaaaa
 
Match ya Valencia ni ya muhimu mno kushinda.... Ila nina imani tutafanya poa as chelsea amekuwa na performance nzuri sana ugenini msimu huu...
 
Game ya valencia ndio inafuata na chelsea atakuwa ugenini. Chelsea amepoteza game moja tu ugenini msimu huu(Dhidi ya man u). Performance ya chelsea ugenini siyo mbaya. Hiyo match atakayeshinda atakuwa amequalify moja kwa moja.
Game yenu vs Valencia ni Must Wing game

Valencia akikufunga atatimiza points 10 ambapo wewe hata umfunge Lille goli 50 na wewe utatimiza 10 hapo Valencia atasonga mbele kwa Head to Head na wewe utaenda Uropa
 
CHELSEA 4-4 AJAX, Champions League: Post-match reaction, ratings

By Mlanzi

Ngoja nianze na Reece James raia wa England ambae anaupiga kama professional player na nafasi yake uwanjani ni full back. Mwezi December tarehe 8, mwaka 1999 ndio alizaliwa pale London Borough of Redbridge, United Kingdom, na sasa ametimiza umri wa miaka 19. Bao la Reece James ndo bao lililoturejesha kileleni katika ile comeback ya kihistoria dhidi ya Ajax.

Kabla sijasahau, first half Ajax walikuwa 3-1 huku wakiwa na shuti moja tu on target, meaning sisi tulikuwa tumejifunga mabao mawili yani 2 own goals.

Zile red cards mbili kwa Ajax zote zilikuwa sahihi kabisa, Tadic alimchezea leg breaker Tammy Abraham na Veltman alikuwa ameushika mpira ndani ya box kosa linalozaa yellow card na penalty juu. Tunahaki ya kujipongeza kwa hii comeback japo tulikosa umakini katika first half. Marcos Alonso ameniangusha kile kiwango hakikuwa cha UEFA Champions League alionekana kuwa chini sana.

Second half ilikuwa powa sana na kama kawaida yetu tulikutana tena na mkono VAR baada ya bao safi kutoka kwa Cesar Azpilicueta kukataliwa kwa kile kilichodhaniwa kuwa handball kutoka kwa TammyAbraham. Hii ilikuwa moja kati ya zile crazy game.

Ndani ya dakika 90+ mambo mengi sana yalijitokeza. Kwanza own goal kutoka kwa Tammy Abraham ndani ya dakika mbili za mwanzo. Pili, Christian Mate Pulisic kushinda penalty iliyotiwa kambani na Jorginho ndani ya dakika tano za mchezo. Tatu, Tammy Abraham kutupia kutokana na through ball ya Mateo Kovačić na bao kukataliwa kutokana na kuwa offside.

Nne, Ziyech wa Ajax kufunga bao tamu kwa njia ya freekick kutoka upande wa kulia mwa uwanja na Kepa Arrizabalaga kujifunga wakati akiokoa.

Tano, Marcos Alonso kupumzishwa half na Reece James na kumfanya Cesar Azpilicueta kuhamia katika left back.

Sita, Kurt Zouma kufanya Maradona-esque style kwa kukimbia na mpira umbali upatao 70-yard na kukosa kosa kufunga.

Next up tutawakaribisha Crystal Palace pale Stamford Bridge katika Premier League siku ya Juma Mosi

KTBFFH
 
Game yenu vs Valencia ni Must Wing game

Valencia akikufunga atatimiza points 10 ambapo wewe hata umfunge Lille goli 50 na wewe utatimiza 10 hapo Valencia atasonga mbele kwa Head to Head na wewe utaenda Uropa
Hakuna mtu wakwenda uropa hapa,huko jalalani mtabaki wewe Asernal na ndugu yako man U.
 
Penati 2, kadi 2 nyekundu

Wale waliokuwa wanaponda penati pindi Man Utd wanapopata sidhani kama nitasikia tena kelele zao
 
Batshuay ni forward nzuri sana kuliko Tammy ,pia hapewi sana nafasi kama Abraham.
Mo sarah alipokuwa Chelsea alikuwa akipigwa benchi. Kila kocha anamtu wake.
I'm sure mpaka msimu uishe ubora wa batshuay utakuwa ushaonekana.
Wewe sio shabiki wa Chelsea na wala mpira hujui. Batshuayi anajulikana na wanaojua mpira, mpaka Batshuayi sio kaliba ya Chelsea, kumtegemea Batsuayi akupe magoli 9 kwenye mechi 11 ni ndoto za alinacha au hadithi za abunuasi.
 
Umeona like yangu huko Bosi?
 
Huyo jamaa ana uchambuzi mzuri me namkubali Sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…