AFC BOURNEMOUTH 2-2 CHELSEA, Premier League: Post-match reaction, ratings
By Mlanzi
Nikisema nianze kumzungumzia Marcos Alonso Mendoza sitamaliza leo[emoji91][emoji91][emoji91]! Itoshe tu kusema huyu ni mwamba aliyeliokowa jahazi..!!! Long live MarcosAlonso.
Unajuwa kunamuda huwa hivi Chelsea tumekwama wapi[emoji2369]!? Yani tumetoka kuwa na Striker tishio kama Didier Drogba, Diego Costa mpaka kudondokea kwa Michy Batshuayi[emoji2369]!! Yani kutoka kuwa na Midfielder aina ya Frank Lampard mpaka kuwa na akina Ross Barkley na Mason Mount[emoji2369]!! Lazima kuna sehemu tunakwama haiwezekani kutoka kuwa na defence ya akina Asley Cole, John Terry, Carvalho mpaka kuwa na akina Kurt Zouma na Tomori. Mungu atuonekanie kwa kweli haiwezekani tutoke kuwa na ma keeper kama Cudicini, Petr czech na leo tuwe na akona Willy Caballero pamoja na Kepa Arrizabalaga Revuelta.
Haki ya nani tena lazima kuna mkono wa mtu hapa[emoji2357]! Ndo maana team inashindwa ku competes na vitimu vidogo kama Bournemouth. Yaani clean sheets saba katika all competitions msimu mzima[emoji2369]? absolutely pathetic.
Anyway, twendezetu dimbani nadhani kijana Marcos Alonso alikuwa wa moto sana kiasi cha kuiweka Chelsea mbele kwa bao tamu linaloweza kumtoa nyoka pangoni katika dakika ya 33 kipindi cha kwanza. Bournemouth walifanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 54 kupitia kwa Jefferson Lerma.
Haikuwachukuwa muda mrefu Bournemouth kuongeza bao la pili kupitia kwa Josh King dakika ya 57 na kuufanya mchezo kuwa mgumu kwa upande wetu. Zikiwa zimebakia dakika tano katika dakika za kawaida mchezo kuisha Marcos Alonso tena alichana nyavu za Bournemouth na kufanya matokeo kuwa mbili kwa mbili na mapaka dakika tusini plus zinakamilika tulifanikiwa kuondoka na point moja inayotuweka hapo hapo tulipo katika nafasi ya nne.
Chelsea tulipata chances kadhaa dakika za lala salama but ubutu wa strikers wetu tulishindwa kuzibadilisha na kuwa mabao.
Kwa upande wa Frank Lampard aliendelea na mfumo wa 3-4-3 ukiwa ni mchezo wa tatu mfurulizo huku akiwa amefanya changes mbili kutoka katika starting lineups dhidi ya Spurs na Bayern Munich ambapo Fikayo Tomori alikuwa amechukuwa mikoba ya Antonio Rüdiger na Pedro Rodriguez kuchukuwa mikoba ya Ross Barkley.
Ilimlazimu kubadilisha shape na kuanza kutumia 4-2-3-1 Baada ya ujio wa Willian pamoja na Ross Barkley kuwapumzisha Jorginho na Fikayo Tomori.
Baadae Michy Batshuayi aliingia upande wa Olivier Giroud.
Chelsea tunabakia nafasi ya nne na kuwaacha Manchester United kwa points nne wakiwa na match mkononi ambapo watakuwa away hapo kesho kukipiga dhidi ya Everton.
Next up: tutakipiga dhidi ya Liverpool kwenye FA Cup siku ya Juma nne.
KTBFFH
Sent using
Jamii Forums mobile app