Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Niliomba Lampard afukuzwe katikati ya mechi ya Lei city. Sikuona cha maana alichokua anakifanya kocha kwakweli.
Wenda FL ndiyo alikua na uwezo mdogo au ni wasaidizi wake. Uongozi wa timu imechelewa sana kumwondosha Frank.
 
So lini mtaanza kuifunga Arsenal?
 
Wanangu, mnaniudhi sana mnavosema Kepa atarudi kwenye nafasi yake.

Naomba niwe mkweli, Kepa akirudi bc naacha kushabikia Chelsea rasmi.
 
Fanya vyovyote Mason Mount abakie..! Lakini pia Chilwell na James wanatia shaka
 
kuna watu humu wasema Tuchel amefeli na PsG ila hawasemi ameshindwa nini..

1. Kachukua makombe yote huko ufaransa ( mtasema ligi rahisi)

2. Kafika fainali uefa na amefungwa na timu bora kabisa Bayern Munich ambayo ilikuwa imetimia kila idara na imetoka kumuwasha Barca goli 8.

3. Mlitaka mafanikio gani zadi ya hayo?


4. Pep Guardiola hajawahi kufika fainali ya uefa akiwa na Bayern na Man city zilizotimia kila idara, mbona hamsemi amefeli!?
 
Fanya vyovyote Mason Mount abakie..! Lakini pia Chilwell na James wanatia shaka
Chilwel sidhan kama anatia shaka kule kushoto hakuna upinzani
Alonso ashajifia tangu wakati wa sarri,

James mapungufu yake ni kwenye defens akiweza kurekebisha hayo anakuwa mzuri
Maana azplicueta age ishaanza kumtupa mkono.

Mount hii ni hazina, dg anajituma sana, natumai ataendelea kupigania namba na kuwa prove watu wrong
 
James siyo mlinzi yule kiungo wa pembeni kulinda naona km wanamfoji tu, kante arudi kuwa defense midfield. Mbele kiungo mshambuliaji Odoi aamniwe ila tunahitaji striker wa kufunga magoli magumu(forcing goal striker) atusaidie kutuamulia matokeo ya match ngumu. Giroud hana huo ubora ingawa alikuwa na umbo na height nzuri.
 
Hili hawawezi kuliona. Watu ni wanafiki sana.
 
Chelsea ina striker gani mwenye magoli kama Mbappe? Ina striker gani kama Icardi?

Chelsea ina LW gani Neymar? Imewahi kua na LW gani kama Neymar?

RW kama Di Maria? Mnaye?

Ni timu ambayo on paper inatakiwa ikufunge goli nyingi. Practically hua inakuaje?

Barca iliyopigwa nane zaidi ya Messi nani alikua lethal? Si ndiyo hayo Barca ikafeli Anfield? Tangu msimu wa kuzingua Anfield Barca ilikua ipo shimoni.

Hiyo fainali umeona PSG ilivyokua inacheza?
 
Mchezaji anaeweza kujiangusha kama Neymar au?? Wachezaji zaid ya Di maria chelsea wapo, ishu ilikua kocha, mana kama Zieych,Timo,Pulics ni wachezaji wazur kuliko hat huyo Di maria wako. Huyo Di maria akija chelsea hapati namba.Nachokiona Tuchel anakuja kuchukua ujiko tu mana wachezaji wapo tena wazur kuliko PSG yenye wachezaji wawili Mbape na Neymar.
 
Neymar anajiangusha ila ana magoli mengi kuliko LW wenu yeyote au hata St wenu yeyote.

Chelsea ina wachezaji wazuri hii siyo siri kila mtu anajua. Shida ilikua kuwaconnect au siyo?

Tutakaa hapa tuone Tuchel ataiunganishaje timu. Hii timu ingekua deadly kama Frank agefigure out njia kuja kwa Tuchel means na yeye aanze kuinject new issues ambazo zinaweza kua dawa ya muda mrefu au mfupi au hata isiwe dawa kabisa.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Uchebe atawafaa kuendeleza pale super Frankie alipoishia ?
Si kweli ndugu zangu ?

Mpaka aje kocha mpya aweke falsafa zake, apate first 11 Yake ,,,Ni March na april huko ,,,, mtapoteana mpaka muombe poo [emoji1787][emoji1787]
Mpaka mwezi wa 6 wakijishtukia wapo Milembe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…