Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Kabisa inatakiwa washabiki wa Chelsea tuombe mbinu za uvumilivu toka kwa washabiki wa Arsenal kujijenga vizuri kisaikolojia maana si kwa uhitaji wa ubora wa timu haraka haraka kwa kiasi hichi ilihali Kocha ni mpya, wachezaji wengi ni wa viwango vya chini kiubora, majeruhi na hata team chemistry bado haijatengamaa kulingana na muda ambao Kocha Mkuu GP kakaa na timu.
 
Wachezaji hakununua GP bali walinunuliwa chini ya Kocha wa zamani TT, punguza chuki binafsi kwa GP ili ubongo uruhusu akili yako kudadavua hoja kimantiki.
 
Ten Hag wa Man UTD ana CV gani kumzidi TT, lakini mbona klabu imemuamini na walianza vibaya kwa kufungwa hata na Brentford FC lakini hado hado wameshaanza kutengamaa na kuwa timu nzuri?

Usikariri maisha kuwa kila Kocha wa kufundisha klabu kubwa lazima awe na CV kubwa.

CV kubwa ya Kocha Mkuu yeyote itabaki kuwa CV na mafanikio ya Kocha Mkuu yeyote hayaangalii CV.

Mfano mzuri ni Carlo Ancelotti alipokuja mara 2 zote darajani alipata mafanikio gani ilihali alikuwa na CV kubwa tu kubeba makombe ya UEFA na klabu bingwa ya dunia?
 
Na CV kubwa inapatikana kwenye timu kubwa, GP naye atapatia CV kubwa ya kwanza hapa hapa Chelsea na yeye kuingia kwenye orodha ya makocha wakubwa kwa sababu ya Chelsea
Hakuna kocha aliyetoka tumboni mwa mama yake akiwa na CV kubwa wala hakuna kocha aliyeshushwa kutoka mbinguni tayari akiwa na CV kubwa. Hizo CV kubwa wanazipata hapa hapa duniani na GP ndio ameanza safari ya kupata CV kubwa kama TT, kama PEP, Kama MOU kama So and so
 
Kuelekea game na Ars8, tuna majeruhi nane

Wachezaji 6 ni rulled out
  1. N'Golo Kante - Thigh Injury - Availability = Ruled Out
  2. Kepa Arrizabalaga - Ankle/Foot Injury - Availability = Ruled Out
  3. Ben Chilwell - Thigh Injury - Availability = Ruled Out
  4. Carney Chukwuemeka - Thigh Injury - Availability = Ruled Out
  5. Wesley Fofana - Knee Injury - Availability = Ruled Out
  6. Reece James - Knee Injury - Availability = Ruled Out
Wachezaji wawili wanaweza kuwepo kwenye bench na au kucheza kabisa kama fitness inaruhusu
  1. Mateo Kovacic - Calf/Shin/Heel Injury - Availability = 100%
  2. Denis Zakaria - Body Crump - Availability = 100%
 
Predicted line up against Ars8 on Sunday
  • Location: London, England
  • Stadium: Stamford Bridge
  • Date: Sunday 6 November
  • Kick-off Time: 15:00 EAT
  • VAR: Jarred Gillett
  • Referee: Michael Oliver
Formation 4-3-3

Sterling ----------------Auba ----------------Mount

Jorginho -------------- Denis -------------- Galagher

Cucurella ------Koulibally ------Silva ------ Chalobah

----------------- Mendy ---------------------

OR

Formation 3-4-3

Sterling -----------Auba -------------Mount

Cucurella -------Jorginho ------ Denis ------- Cheek

Koulibally ------------Silva ------------ Chalobah

--------------------- Mendy ---------------------
 
Chelsea ni timu ya sita katika historia ya UEFA kuweza kushinda mechi 100
Je timu zingine ni zipi?
  1. Real Madrid
  2. Bayern Munich
  3. FC Barcelona
  4. Manchester Utd
  5. Juventus
  6. Chelsea
Siwaoni wababe kama Liverpool na Ac Milan maana hawa jamaa ndio wametuzidi UCL kwa mbali. Nawaza walikua wanachukuaje yale makombe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
4-3-3[emoji3581]

3-4-3[emoji777]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hii ni timu au hospitali ya rufaa?
Acheni visingizio Kenge nyie, sisi tunachotaka muifunge hio misukule ya Arteta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…