MAONI YANGU KUHUSU MCHEZO WA JANA.
Jana tumeshuhudia kwa mchezo wetu wa kwanza katika ligi kuu Uingereza na binafsi nilipata wasaa wa kuangalia na kufuatilia katika dakika zote 90. Itoshe kusema kwa sasa kuna mabadiliko makubwa mno katika klabu yetu, ile hali ya upambanaji ambayo tulikosa msimu ulio pita kwa sasa unaiona kabisa. Wachezaji karibia wote wamecheza vizuri, ni kuna makosa madogo madogo tu nadhani ata mwalimu ameyaona.
Enzo ni mchezaji haswa ujio wa Caisedo utamfanya huyu awe hatari zaidi, Enzo ata namba 10 anacheza jana kaonyesha kiwango cha juu sana. Jackson ni mtu bhana yaani anakaa sehemu sahihi ambapo mpira ukija unamkuta yupo, huyu jamaa namtabiria kufunga magoli kuanzia 20 msimu huu. Sterling jana kacheza vizuri ila bado ni takataka tu. Mjumuiko wa Silva na Disasi ni hatari sana wote wazuri sana yaani, ila kwa jana beki zetu zilikuwa zinakatika sana. Ndio maana tunahitaji DM kama Caisedo na taarifa zinasema kila kitu tayari. Ujio wake utafanya beki zetu zitulie zaidi.
Gallagher jana kacheza vizuri aendelee kukaza zaidi, ma kapteni wetu wako vizuri sana hapa tuwaombee tu majeraha yawapite mbali. Mudryk sio wa kupewa dakika 10 tu inabidi apewe dakika zaidi, yaani kwa dakika alizo cheza kaonyesha madhara zaidi kuliko Sterling. Ila nimeumia kutopata ushindi maana wale jamaa tulikuwa tumeisha washika na walikuwa wameingia kwenye mfumo kabisa.
So far tuko vizuri sana kwa sasa, Poch ana kitu aisee.