DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Klabu ya Fluminense ya Brazil imeweka historia kwa kuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia la Klabu la FIFA mwaka 2025 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Al Hilal ya Saudi Arabia katika mchezo wa kusisimua uliopigwa nchini Marekani.
Ushindi huo umeihakikishia Fluminense tiketi ya kukutana na Chelsea ya Uingereza katika hatua ya nusu fainali, mechi inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka duniani kote. Chelsea, bingwa wa UEFA mwaka uliopita, itakutana na wapinzani wa Amerika Kusini walio na historia na kasi ya kuvutia.
Wakati hayo yakiendelea, michezo miwili ya robo fainali ya #FIFACWC itapigwa leo ambapo Paris Saint-Germain itachuana na Bayern Munich, huku Real Madrid wakimenyana na Borussia Dortmund ya Ujerumani – mechi zitakazoamua timu mbili nyingine.