Chelsea Vs Liverpool

Chelsea Vs Liverpool

athury92

New Member
Joined
Sep 13, 2016
Posts
2
Reaction score
4
Liverpool inaendelea kukabiliwa na mechi ngumu Ijumaa, watakapozuru Chelsea kwa mchezo wao wa nne ugenini, wa tano kwa ujumla kwenye Ligi Kuu Uingereza.

Habari kuu zilizoenea kutoka kwenye mkutano wa Jürgen Klopp na waandishi ni Mjerumani huyo kubainisha kuwa Emre Can amerejea mazoezini lakini anahitaji kuchunguzwa tena kabla ya kuingia kikosi cha kwanza. Kwa sababu hii, Jordan Henderson anatarajiwa kucheza sehemu ya kiungo.

Dejan Lovren atarejea kushirikiana na Joel Matip baada ya tatizo lake la jicho, Ragnar Klavan bado anasumbuliwa na tatizo la goti, Mamadou Sakho, Joe Gomez na Sheyi Ojo bado wapo nje, na Simon Mignolet bado anayo nafasi kubwa kuendelea kukaa langoni licha ya Loris Karius kupona.

Chelsea imepata pigo mapema wiki hii ilipobainishwa kuwa beki na nahodha wao John Terry ataikosa mechi hii muhimu kwa sababu ya majeraha, wakati beki mwenzake wa kati Kurt Zouma akiendelea kuuguza majeraha.

[http://images]

Kwa sababu hii, David Luiz anapewa nafasi kubwa kucheza mechi yake ya kwanza kwa mara ya pili tangu alipokamilisha uhamisho wake kutoka PSG siku ya kufungwa dirisha la usajili majira ya joto.

Mbele kabisa, Oscar anaweza kuchezeshwa mbele ya Nemanja Matic na N'Golo Kante pamoja na Eden Hazard na Willian wakishirikiana kumlisha Diego Costa ambaye amekuwa kwenye kiwango cha juu msimu huu.

Liverpool cha kwanza (4-3-3): Mignolet; Clyne, Lovren, Matip, Milner; Henderson, Wijnaldum, Lallana; Mane, Coutinho, Firmino.

Chelsea kikosi cha kwanza (4-3-3): Courtois; Ivanovic, Luiz, Cahill, Azpilicueta; Matic, Kante, Oscar; Willian, Hazard, Costa.

1474003695820.jpg
 
Liverpool FC tunashinda gemu hii bila wasiwasi...best player of the month...Mane ana Goli lake
 
Back
Top Bottom