Chelsea wanakwama wapi?

Joined
Dec 28, 2016
Posts
50
Reaction score
52
Sarri zamani alikuwa na kosa mmoja, la kuwapangua wachezaji huku Kante akipelekwa mbele, Kovacic/Ross nao wanapatikana mbele, alafu mlinda ukuta anakaba kama anaangalia movie la Sunnillshet vile, anakaba kwa kukodoa macho tu, hatii mguu, hatii mwili, bahati mbaya ni kimbaumbau na bahati mbaya anakuwa targetted yeye na wapinzani wakitaka kufanya maisha magumu kwa Chelsea

Nilihoji mwanzoni mwa msimu, nikasema ukiweka wagumu watatu katikati ambao hakuna creative midfielder hata mmoja huku mbele una Giroud au Morata ambao hawana msaada mkubwa kila wapatapo nafasi, unabaki na watu wawili ambao ni Hazard na mwingine ambaye mara nyingine anakuwaga kama mamluki naye..ukikaba Hazard na Jorginho kikamilifu, basi unakuwa umeikaba Chelsea yote kiurahisi...as long Jorginho anakabia macho huku wakiwa na beki Luiz ambayo mda wowote anajiroga mwenyewe, basi unashinda mechi vizuri au kupata matokeo yoyote yasiyohuzunisha sana

Kosa la pili amelifanya hivi karibuni, kuwasema hovyo wachezaji, mabishano yake na Hazard kupitia press conference kwamba he is more of individual ndio tunaona Bournemouth wanapata matokeo makubwa sasa, huyu ndio key kwa kufanya miujiza yote pale mbele alafu unamsema hadharani tena vibaya,mwisho wa siku anapunguza work rate ambayo inaigharimu the whole team..unhealthy relationship baina ya wachezaji ni moja ya changamoto kubwa za walimu wengi, Sarri maisha yake yanaweza kuwa mafupi pale darajani kama ataendeleza tabia zake za kuhamishia lawama za matokeo mabaya kwa wachezaji wake....

Wanafunzi wazuri wakifeli mitihani, mtu wa kwanza kulaumiwa ni mwalimu ambaye ameshindwa kuwa maarifa au mbinu sahihi namna ya kufaulu mtihani, Chelsea bado ina wachezaji wazuri,na wamemuongeza Gonzalo Higuain katika safu yao ya ushambuliaji, kwa kifupi unaweza kusema wana team imara ambayo wakikosa matokeo basi mbinu za mwalimu inabidi zitizamwe zaidi kuliko performance ya wachezaji...Kante ambaye yupo vizuri kwenye majukumu ya kiungo mkabaji apewe nafasi kwenye eneo ambalo analimudu na Jorginho ambaye Sarri anamuita technical footballer asogee mbele akaongeze creativity

#Steph

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kocha mzuri lkn si kwa ligi ile ya Uingereza. Kweli pasi 'mingi sana kama yote lakini hazina maana' coz sio productive! Japo Conte alizingua kuwakazia 'wachezaji lialia na kuzira kwa kufanya mgomo baridi wakisemwa kdg kujitoa kwa ajili ya timu' lkn bado atabaki bora sana vs Sarri! Nje ya top 4 inawahusu!
 
Uadui kati ya kocha na Hazard unachangia pia
 
Naam pasi nyingi lakini msaada mdogo na ubaya wa pasi zinapigwa kwenye half ya Chelsea wenyewe, huku ni kupoteza mda kwa namna iliyojificha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chelsea wanachukua mpira pale, Luiz anafinya kidogo anampa Kante, Kante anasogea anampa Pedro, Pedro anafunguka anampa Hazard, Hazard anachambua kama karanga mpaka ndani ya box halafu anarudisha mpira kwa Luiz, Luiz anarudisha kwa Goli kipa, aisee ndio kazi hiyo Chelsea wanapiga pass nyingi kama wapo mazoezini, sasa huo ni mpira au uwendawazimu?
 
Hahahaaa mkuu umeelezea vizur sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kocha wenu anachanganya Bangi na sigara ,yaani kante umchezeshe kama attacking midfielder unategemmea nn? Jonginyo yeye Kazi yake kupiga pasi zone yenu tu,na ndiye anaongoza Kwa pasi then sina uhakika kama ana assist hata moja,angekuwa anatoa pasi zone ya adui saiz chelsea ingekuwa inaongoza ligi
 
Ndio mbinu za kocha hizo ngumu kufahamu analenga nini.
 

Naam pasi nyingi lakini msaada mdogo na ubaya wa pasi zinapigwa kwenye half ya Chelsea wenyewe, huku ni kupoteza mda kwa namna iliyojificha

Sent using Jamii Forums mobile app

Hayo ni matokeo ya kushabikia mpira wa Premier League tu bila ya kuwa unachungulia na ligi nyengine. Mkuu uwanjani kila mtu anapangiwa na kazi yake. Kwa mfumo wa kocha aliekupo timu inahitaji iwe na deep lying player maker. Sasa huyo kante hata akicheza hapo chini mnapotaka hatoweza kupatendea haki. Atashindwa kuposes mpira inavotakilikana. na ndio mana anachezeshwa Box to Box. na sio attacking kama munavosema. Tatizo lilokuepo ni kua Kante anashindwa kuicheza vizuri hiyo position mpya aliyopangwa na hilo ndio moja ya tatizo kuu la timu. Sasa hilo sio kosa La Sarri wala Jorginho. Tatizo lipo kwa Kante kashindwa kuadopt position mpya na timu iankosa mchezaji mwengine wa kucheza ile position.
Mnaanza kuuliza na assist kiukweli mumelewa na typical british mentality. Jorginho sio kazi yake kutoa assist, assist zinatakiwa zitolewe na Hazard, Pedro, Wilium. Deep lying Midfield kazi yake ku poses game na kucool tempo ya game. pamoja na kuwasplier mipira mawinga na mafull back ili wapate kufanya mashambulizi. sasa ikiwa hao mawinga wanacheza ovyo yeye kahusika na nini? Chelsea wanajitahidi sana kwenye position dominating na hiyo ndio kazi kuu ya Jorginho. Masuala ya mashambulizi ni kazi za wengine amabao kiulweli wanashindwa kuzifanya kazi zao vizuri.
 
Team nzima wachezaji ni hazard na lingolo unategemea wapate nini,?

Ova
 

Mkuu tatizo la Chelsea kuu ni kuwa wachezaji wengi wameshachoka na hawawezi tena mpira wa kiwango cha Chelsea. Wachezaji kama Pedro, Giroud, Willium, Luiz, Fabrigus, Azpilicueta, Cahil,Moratta, Rudiger. Hawa wote ni either wameshapoteza ubora wao na wengine ni mabomu yaliongia kwenye timu.
Willium anapocheza vizuri mechi moja basi musubiri baada ya mechi 7 mbele ndio utaona tena performance nzuri kwake. Jama anaoksa consistence na ndio tafauti kubwa kati ya Big player na mchezaji wakawaida. Nahao wachezaji wakiengereza kina Barkley nao tukae kimya tu kwa kweli.
Hata wakimtimua Sarri baada ya mwaka watatimua na mwengine ikiwa kuanzia management ya timu mpaka mashabiki wao bado hawajatambua kama tatizo kuu ni wachezaji.

Tatizo jengine ni kuwa wachezaji waliokuepo wengi ni wachezaji ambao wanashindwa kuadoptor au kutumika vizuri katika mfumo wa kocha. Mchezaji kama Kante kocha ametumia mda mwingi kumueka sawa na mwisho ameanza kumwaga mchuzi kwenye vyombo vya habari ili mufahamu lakini bado wagumu kufahamu. Kante hachezeshwi Attacking kante anachezeshwa Box to Box. Kazi yake kuu ni kumcover Jorginho nasio kushambulia. Kazi nyengine ni kumsaidia Jorginho kuchezea mpira ambayo anafell moja kwa moja. Mana timu pinzani zote zimekua zikimkalia man marking Jorginho na ndio sababu kuu ya chelsea kuanza kuharibu baada ya kuanza vizuri. Sasa jamaa kila wakati anaonekanwa mbele ya goli kama striker binafsi sifahamu ata anakwenda kufanya nini kule.

Na ndio mana siku zote Sarri anawalalamikia wachezaji kuwa anachowambie wakifanye uwanjani sicho wanachokifanya. wanacheza wanavojua wao. Na ndio ikafikia stage ya kuwachana mpaka kwenye vyombo vya habari.
 
Mkuu analysis yako ni nzuri,lakini umeongelea scenario moja tu"Wakati wanamiliki mpira". The opposite is worse for Gorginho kucheza deep midfield. hawezi kuintercept mipira, hana speed , hana physic ya kupambana na wahuni wa EPL. YOUR THINKING IS THE SAME AS SARRI'S AND ITS THE ONE COSTING CHELSEA CURRENTLY. Mpira siyo kuposses tu, inatakuwa kuwa na plan ya kurecover the ball when you loose it.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…