Kuna chemba ya maji taka inayotiririsha uchafu kando ya Soko jipya la Kariakoo, ambalo limezinduliwa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan. Chemba hiyo ipo kwenye kona ambapo daladala za kuelekea Masaki hupaki.
Chemba hiyo limekuwa kero ya muda mrefu kwa wananchi na wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao pembezoni mwa soko hilo, ambapo wengi tupo kwenye hatari ya kupata magonjwa.
Jambo la kushangaza ni kwamba tulipata matumaini tulipoona usafi ukifanyika mara baada ya kutolewa taarifa ya ujio wa Rais Samia kuzindua soko hilo. Hata hivyo, baada ya uzinduzi hali imerejea kama ilivyokuwa awali, ambapo maji taka yametapakaa tena katika eneo hilo.
Nabakia kujiuliza; je, mamlaka za Jiji na DAWASA hawaoni umuhimu wa kutafuta suluhisho la kudumu la chemba hilo lililopo karibu na soko la Kariakoo, linalotajwa kuwa soko la kimataifa? Kiukweli, uwajibikaji unahitajika.
Ni aibu kuona mazingira yanayolizunguka soko hilo yakiwa machafu kwa kiwango hicho, huku waliopewa dhamana wakiendelea kupokea mishahara na kukaa katika ofisi za umma bila kuchukua hatua stahiki.
Huu ndio mwanzo wa kusambaa kwa magonjwa ya kuambukiza ikiwemo Kipindupindu na magonjwa mengine ya tumbo, kwa kuwa kuna watu wanauza bidhaa mbalimbali ikiwemo za chakula.
Pia soma: Responded - Rais Samia: Wasimamizi wa soko la Karikoo zingatieni miundombinu ya majitaka na usafi
Usafi wafanyika, chemba yazibwa ~ Chemba iliyokuwa inatiririsha maji taka kando ya Soko Jipya la Kariakoo yasafishwa