Chemistry hii ya mapishi ya msosi inashangaza sana

Chemistry hii ya mapishi ya msosi inashangaza sana

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Jana nilifanya kitu tofauti kabisa na mazoea..lakini nikapata matokeo ya kushangaza mno..pishi zima ndani ya jungu moja

Ubao ulikuwa umebana kisawasawa kutupia macho kwenye jokofu kuna haragwe lililochemshwa jana na mtindi robo lita
Sangara mbichi na mnavu fresh
Nyanya zilikuwepo na vitunguu
Hoho Zilikuwepo na karoti
Chumvi ilikuwepo na chili sauce
Na maji pia ...jiko la gesi na vyombo vya kupikia

Uvivu wa kupika ulikoma minyoo tumboni ilipoanza rabsha..ni kama ilikuwa inafyonza mabandana..nikajisemea kumbe huku ndio kuumwa njaa..basi inauma kweli...
Wife hayuko na sina mpango wa kando kwasasa ...chamdeko alishanishit kwa kibuti live toka mwaka juzi...Mwaj pale kwa mama muuza anayeokoaga jahazi kaenda kwenye kigodoro tangu juzi huko kimbiji hajarudi mpaka leo...nasikia kajiozesha kwa msela mmoja mwenye baiskeli za kukodisha

Nikajiwazia lazima nipike nile nishibe ..lakini haya mambo ya kuanza kupika kila kitu na kwake kunachafua sana vyombo na kupoteza muda..nikawaza mbona kwenye sahani tunachanganya...mbona mdomoni vinaingia pamoja ..mbona tumboni vinakaa pamoja na vikitoka ile end product wala huwezi kujua kipi ni kipi....!?

Nikainjika jungu langu motoni nikaweka ile ndondo ya jana
Nikachambua mchele robo nikatia chunguni
Nikakata nyanya mapande manne nikatia..na karoti na hoho hivyohivyo
Juu yake nikaweka mnavu kisha samaki halafu nikamalizia na chumvi mtindi na chili sauce NIKAFUNIKA JUNGU langu..vikaanza kutokota...

Si unaujua moto wa gesi ulivyo? Nususaa kubwa nikaipua jungu langu...ile mixer ile....haikutoka boko lakini ....nimeshiba mpaka leo japo nilipakua nusu tuu
Nimeokoa muda na vyombo na maji...nipo tu hapa nasubiri kula ndaza...
Kama umeipenda hii chemistry nakushauri jaribu....ila SIHUSIKI NA MATOKEO....[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
[emoji23][emoji23][emoji23]ningekuwa na mitungi ningezalisha gas

IMG_1245.jpg
 
Mixer ya ndondo na mtindi, bahati nzuri wife hakuwepo. Gesi uliyotengeneza ungeweza kuihifadhi ingetusaidia senti za uchaguzi kaka.
 
Mixer ya ndondo na mtindi, bahati nzuri wife hakuwepo. Gesi uliyotengeneza ungeweza kuihifadhi ingetusaidia senti za uchaguzi kaka.
[emoji16][emoji23][emoji23][emoji3][emoji2][emoji1][emoji23][emoji28][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Jr[emoji769]
 
Back
Top Bottom