Chemsha bongo: Shilingi 100 iko wapi?


umeangalia vizuri mifukoni mwako!? Teh teh
 
Mambo vipi?ulikopa kwa dada yako buku 5000 na kwa bro 5000,ukanunua kitu chako kwa buku 9700,so ikabaki 300,sasa mdogo wangu,kwa kuwa ulikopa kwa watu wawili tofauti,tunagawanya kwa 2 ile 9700,uliiyoitumia,ambayo jibu lake ni 4850,so ulitumia 4850 ya dada yako na 4850 ya kaka yako,then ukabaki na 150 ya kaka yako na 150 ya dada yako,ukaamua kupunguza deni la 100 kwa dada yako,ambapo itakuwa 4950,na ukafanya hivyo kwa kaka yako nayo ikawa,4950,ukijumlisha inakuwa 9900,ukiweka na mia uliyobaki nayo inakuwa msimbazi kamili.
 

Mwanangu uko juu sana!!!!!!!!
uko sahihi wengine hamna kitu!
 

mkuu umetisha!
 
JF sio tena GT yaani swali lina mwaka mmoja jibu ndio leo.
Halafu UDSM chuo bora,MZUMBE sijui nini , aaah
 
chemsha akili kidogo...!! then unipe jibu. nguo inauzwa 10000/= huna pesa ukaenda kukopa kwa dada 5000/= na kaka 5000/= jumla 10000/= ukaenda dukani ukaomba upunguziwe ukauziwa 9700/= ukabakiwa na 300 ukapunguza deni kaka yako ukampa 100 dada ukampa 100 ukabaki na 100 jumla kaka akawa anakudai 4900 na dada 4900 ukijumlisha unapata 9800/= ukiongeza na 100 yako uliyobakinayo unapata 9900/=je? 100 iko wapi? nisaidie jibu,

ukipatia nakutumia vocha yako.
 
Gawanya deni 9700kwa wa wawili alafu walipe kila mmoja na jumlisha na uliyobaki nayo
 
Cash in:
kutoka kwa kaka - 5000
kutoka kwa dada - 5000
Jumla 10000.

Cash out:
Kununua nguo- 9700
Kumlipa kaka -100
Kumlipa dada -100

Jumla 9900

Balance jumla cash in -jumla cash out.
10000-9900=100.

mfukoni alibakiwa na 100, na cash flow inaonyesha balance ni 100.

hivyo hakuna mia iliyopotea.
 



:A S-rap: hiyo 100 imebaki kwenye suruali aliyo nunu .:msela:
 
Big up!, hesabu sio machungwa yanayoweza kuoza!kama hataki akaendelee kusomea kitandani
 

5000 - 100 = 4900
5000 - 100 = 4900.

4900 × 2 = 9800.

ukumbuke kule ulibakiwa na 100 tu.

9800 + 100 = 9900. Ile 100 imekwenda wapi?

Nachotaka kuelewa ni kwamba ni nini kinafanya hesabu hiyo kutoa jibu ambalo si sahihi.

{Error iko wapi?
Kwanini mia isionekane?
Kwanini mia ipotee?}
 
Mkuu waliotunga kanuni za hesabu hawakuwa wajinga na hizo kanuni hazikutungwa kwa siku moja, Mali uloyonayo mkononi na ile unayodaiwa huwezi kuzijumlisha pamoja na zote zikawa positive, tatizo lako unajumlisha hela uliyo nayo na ile unayodaiwa kama vile unayo. Mali uliyonayo mkononi zinaenda pamoja na mali unayodaiwa zinaenda pamoja na baada ya hapo unaweza kutafuta balance kama ukilipa utabakiwa na kitu au utaendelea kudaiwa. Sasa wewe unapojumlisha 9800 ambayo ni deni na 100 uliyonayo mkononi unapata 9900 basi niambie hiyo 9900 ni nini? Ni mali uliyonayo au ni deni?

Anyway nisikaze sana msuli maana thread yenyewe imekaa kwenye utani na udaku labda umeamua kututania au umeamua kutupa udaku jinsi watu walivyokuwa wanapata taabu kuitafuta hiyo mia bila kuelewa kanuni za mali zinatawaliwa na vitu viwili ama unacho ama unadaiwa. Na kama huna halafu hudaiwi maana yake hujielewi.
 
mkuu majibu yote yale hayajatosha, kwamba hela imebaki kwenye nguo?hivi ungepunguziwa ukauziwa 9500, nawe kuamua kuwalipa uliowakopa 200 mmoja na mwingine 200, si kila mmoja angekudai 4800!Jumla yake ni 9600 ilhali wewe una 100 ukijumlisha na deni ni 9700!Utaanza kuuliza 300 imeenda wapi?Utakuwa mwehu lazima!Lakini kwa sababu ya utani tumechukulia poa tu sidhani kama kweli unakomaa mia imeenda wapi!
 

Ulimhola baba nyakwana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…