Chemsha bongo: Shilingi 100 iko wapi?

Wakuu heshima yenu....
Natumaini mu wazima mkipambana na mihangaiko ya kuimaliza january yetu pendwa...
Naomba mnisaidie kutegua hili fumbo ni mara nyingi nilikuwa nalisikia lakini sikulitilia maani sasa mwenzenu karibia naaibika....iko hivi...
Nilikuwa nahitaji shat dukan na linauzwa 10000 kwa kuwa sina fedha nilikopa dada 5000na kaka 5000 nilivyokwenda dukan nikapata punguzo na kuuziwa kwa sh 9700 nikabakiwa na 300.....sh 100 nikamlipa dada na kaka nikamlipa 100 nikabakiwa na sh 100. Hivyo dada akawa ananidai 4900 na kaka 4900 ukizijumlisha unapata 9800 pamoja n ile sh 100 iliyobaki inakuwa 9900.je sh 100 imeenda wapi ili itimie 10000????
 
Hapo umejumlisha hela unayodaiwa na hela uliyo nayo mkononi ndio tatizo,
Ni kama hesabu za hasi na chanya, Huwezi kujumlisha deni (hasi) na mali ulizonazo (chanya) kisha upate jumla unatakiwa utoe
kujumlisha ilitakiwa iwe hivi -4900 (deni) + -4900 (deni) + 100 (hela mkononi) = -9700 (deni)
Hapo unapata una deni la 9,700 kwa kuwa kiasi cha pesa ulichotumia baada ya kukopa hiyo 10,000 ni 9,700 tu, so matumizi yako ni sawa na deni lako...

Kama ushawahi kufanya biashara ni rahisi sana kuelewa
 
Mambo gani ya kupeana hesabu saa hizi? Mchana wote huu...tena jumatatu
 
Bado watu mnaumiza kichwa na hili swali? Mbona jepesi sana??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…