Chemsha bongo: Shilingi 100 iko wapi?

 
ELEWA kuwa AMANA (asset) = Mtaji (capital/equity) + madeni (liabilities). Hii ni 'accounting equation'.

in other words (kwa maneno mengine);

AMANA (asset) - madeni (liabilities) = Mtaji (capital/equity) [hii ni hesabu ya msingi sana. nafikiri ni darasa la tatu]

au/na (or/and);

AMANA (asset) - Mtaji (capital/equity) = madeni (liabilities).

sasa tuanze kuchambua sentensi kwa sentensi;

Unataka kwenda kununua nguo dukani, nguo inauzwa shilingi 10,000, huna pesa kwa wakati huo so unaamua kukopa 5,000 kwa dada na 5,000 kwa kaka.
AMANA (asset) = Mtaji (capital/equity) + madeni (liabilities).
10,000 = 0 + 10,000
angalizo;
mtaji ni 0 kwa kuwa haukuwa na hela yoyote ya kununulia nguo.

unapoenda dukani unakuta nguo inauzwa 9,700 so unarudishiwa 300.

when applying discount treatment in this transaction;
AMANA (asset) = Mtaji (capital/equity) + madeni (liabilities).
10,000 = 0 + 10,000


angalizo;
AMANA ni 10,000 kwa maana kwamba 9,700 ni nguo (Non current asset); na 300 ni hela kutoka kwenye discount aka punguzo (cash - current asset).

unaamua kupunguza deni, unampa kaka shilingi 100 na dada 100 na wewe unabaki na 100.

HAPA CASH (300) inaanza kutumika. Kwa hiyo katika cash (300) iliyotumika kulipa deni ni 200, kwa hiyo;
AMANA (asset) = Mtaji (capital/equity) + madeni (liabilities).

9,700 (nguo) + 300 (cash) = 0 + 10,000

9,700 (nguo) + [300 (cash) - 200 (kwa ajili ya kulipa deni) = 0 + 10,000(deni) - 200 (deni linapunguzwa)

kwa hiyo tunapata;

[9,700 (nguo) + 100 (cash)] = 0 + 9,800


angalizo;
bado mtaji ni 0 kwa kuwa haukuwa na hela yoyote ya kununulia nguo tokea hapo awali.

kwa hiyo kaka anabaki anakudai 4900 na dada 4900. ukichukua 4900 ya kaka na 4900 ya dada inakuwa 9800

AMANA (asset) = Mtaji (capital/equity) + madeni (liabilities).

[9,700 (nguo) + 100 (cash)] = 0 + 9,800

[9,700 (nguo) + 100 (cash)] = 0 + [4,900(deni la kaka) + 4,900(deni la dada)]

[9,700 (nguo) + 100 (cash)] = 0 + 9,800

ukiongeza na 100 yako inakuwa 9900. je mia imekwenda wapi?

AMANA (asset) = Mtaji (capital/equity) + madeni (liabilities).
HAIWEZEKANI, HAIKUWEZEKANA NA HAITOWEZEKANA AMANA IJUMLISHWE NA MADENI. SIKU ZOTE AMANA TOA MADENI UNAPATA MTAJI. AU MADENI UJUMLISHE MTAJI UPATE AMANA. SHS 100 NI AMANA NA 9800 NI DENI, HAVIWEZEKANI VIKAJUMLISHWA. NI KAMA 'MAFUTA' NA ' MAJI' KAMWE HAVICHANGANYIKI.

 
Kwa ujuzi wangu
Kwa kuwa wao ndo walikuwa wanakudai 4900 kila mmoja yaani jumla 9800 kumbuka ulikuwa umewapa sh 200 hivyo ukijumlisha inakuwa 10000
 
mmh!kumbe jf kuna zaidi ya wasomi!
 


ulikopa 10,000
ukatumia 9,700
zikabaki 300
ukalipa deni 200
ukabakiwa na tshs 100
unaulizia 100 ipi???? Hakuna 100 iliyobaki
 
Kwa kuwa alikopa 5000 kwa watu wawili, akawa na jumla 10,000. Baada ya kupata discount ya sh 300 allitumia 9,700. Hivyo kabla ya yote kama angewarudishia 150 kila mmoja wangekuwa wanamdai 4850 kila mmoja, lakini aliwapa mia mia kila (Jumla 200) hivyo kila mmoja alikuwa anadai 4,950 ambapo jumla ya wote wawili ingekuwa 9,900 akijumlisha na ile 100 aliyobaki nyo inakuwa 10,000.

10000 - 9700= 300 (Baada ya DIscount)

9700/2 = 4850 ( Kama angeamua kuwalipa baada ya discount ili kupunguza deni 150 kila mmoja)

4850+100 = 4950 (Baada ya kutoa Jumla 200 kwa wote wawili kupunguza deni na anabaki na 100 mkononi)

4950*2 = 9900 (Baada ya kupunguza deni Jumla ya madai yao)

9900 + 100 = 10,000/= (Akijumlisha na ile 100 ya mkononi)
 
Tungekuwa siku zote 2naelimishana kwa hivi! Da wangapi wangenufaika,
USHAURI
tupunguze majadiliano ya mapenzi na siasa. tuwe tunagusa na hv.MIMI NIMEPENDA NA NIMENUFAIKA SANA.
AHSANTEN.
 
Nimekopa kwa dada sh. 5000 na kwa kaka sh.5000, kwa hiyo nadaiwa sh. 10000. Nikinunua nguo kwa sh. 9700, nabakiwa na sh. 300. Nikaamua kumrudishia dada sh. 100 na kaka sh. 100. Kwa hiyo dada bado ananidai sh. 4900 na kaka sh. 4900, jumla nadaiwa sh. 9800 ambazo ni sawasawa na 9700 niliyonunulia nguo + 100 niliyobaki nayo.


Kwa maana nyingine: Nikinunua nguo nabakiwa na sh. 300 lakini nadaiwa sh. 10000, nikitoa sh. 200, yaani mia kwa dada na mia kwa kaka, nabaki na deni la sh. 9800. Kwa hiyo ukitaka iwe 10000, chukua deni la sh. 9800 ninalodaiwa, kisha jumlisha na mia mbili ambayo nimekwishalipa, yaani, sh. 9800, deni + sh. 200 ambayo nimelipa, jumla = sh. 10000.

Sh 100 ipo ktk sh9700 uliyonunulia nguo. Ikiwa umepunguza deni na kua sh9800, sh100 uliyobakiwa nayo na sh 100 iliyopo kwenye sh 9700 zitafanya jumla ya sh 10000.
 

Imezoeleka sana hapa jamvini
 

Bila shaka imekatwa VAT
 
Tungekuwa siku zote 2naelimishana kwa hivi! Da wangapi wangenufaika,
USHAURI
tupunguze majadiliano ya mapenzi na siasa. tuwe tunagusa na hv.MIMI NIMEPENDA NA NIMENUFAIKA SANA.
AHSANTEN.

mia iko wapi?
 
Tumia cauchy euler equation formular utapata jibu kiulaini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…