Chemsha bongo: Thibitisha hapa kuwa wewe una vyeti orijino

Chemsha bongo: Thibitisha hapa kuwa wewe una vyeti orijino

Wewe ni muuzaji wa duka, mteja anakuja na shilingi elfu Kumi (10,000/-) feki anataka Mkate wa shilingi 2,000/- ...wewe bila kujua unaipokea lakini unagundua hauna change ya kumpa mteja unaamua kuomba change kwa jirani yako na hiyo hiyo 10,000 feki kisha unamrudishia mteja shilingi elfu nane (8,000/-) na mkate, baadae jirani anakuja kukuambia ile pesa uliyompa ni feki unaamua kuichukua na kumpa shilingi 10,000/- halali. Je, utakuwa umepata hasara ya shilingi ngapi?

A. 12,000

B. 18,000

C. 10,000

D. 20,000

E. 8,000

F. 2,000


Jaribu

ELEZEA JIBU LAKO KWA KINA
 
Mmeanza kuleta habari za Facebook huku!!! Hapo umekula hasara ya 20, mkate 2000/= , Chenji 8000/= na 10000/= ya jirani ako
 
Jibu ni c 10000 kumbuka 8000 uliyomrudishia mteja na 2000 uliyobaki nayo umeitoa kwa jirani baada ya kuomba chenji hivyo basi ile pesa feki ukirudishiwa na jirani na ww kumrudishia pesa yake original inamaana ya kwamba ile hasara sasa iko kwako ambayo ni thamani ya mkate 2000 na 8000 ya chenji.
 
Mkate wa 2000 na chenji ya 8000 jumla 10000....kama kuna mtu anajibu zaid ya hilo basi atakuwa bashite
 
Hasara sh 8000
Kiuhalisia jirani anatolewa kwenye hesabu katoa pesa kisha karudishiwa.
Pili Jamaa ilibid apate hasara ya 10000 ila alibakiza 2000 halali km mauzo ambayo ilibaki toka kwa jirani.
Hvo jamaa anapata hasara 8000.
 
Leo nimeamini kuwa somo la hesabu ni gumu sana nchi hii kama hesabu ndogo km hii wameishindwa
 
Hasara sh 8000
Kiuhalisia jirani anatolewa kwenye hesabu katoa pesa kisha karudishiwa.
Pili Jamaa ilibid apate hasara ya 10000 ila alibakiza 2000 halali km mauzo ambayo ilibaki toka kwa jirani.
Hvo jamaa anapata hasara 8000.
apa umekoroga chukulia ile elfu kumi ni yakwako hukuiomba kwa jirani alaf mrudishie elfu nane kwahiyo elfu mbili uliyo ikata hapo ni faida au hasara yako ni ile elfu ambayo n fake kwahyo una loss ya elfu kumi tu
 
ile 10000 inayozunguka mda wote toka kwa mteja kuja kwako mpka kwa jirani ni fake...kwa hyo itoe kwny mahesabu..yn tupa kapuni..

inshu imeanzia hapa...
jirani yako alikupa change ya sh10000 tena halali. sasa tayr una 10000 halali,,, katika hela ile alokupa jirani unampa mteja sh 8000 na mkate wake wa 2000...yani imepotea kama ilivo,,,, inamana hapo wew dukan hujaingiza kitu......isipokuwa umepoteza 10000 kwa kumpa mteja 8000 na mkate juu.......atakua anajisifu sana huko aliko mana nisawa na kusema umempa vyote hvo bureee............haya tuendelee

baada ya kama dk 5 jirani anakustua,,, oyaa hela ulonipa ni fake,,, bs kwa mara nyngne tena unaamua kuchukua 10000 yako nzuri kabisa na kumpa jirani.

HITIMISHO
8000 Ulompa mteja+2000 ya mkate+10000 ulompa jirani-10000 fake=20000.

umepata hasara ya sh 20000.


mlatinoh king
Bashite
 
Back
Top Bottom