Naona ziiiiiiiii
Ngoja nitoe jibu la hili swali la kwanza labda itasaidia kupata jibu la swali la pili.
Watu waliupenda utabiri wa hali ya hewa wa kampuni A kwa sababu 75% ya utabiri wake ulikuwa si sahihi hivyo ni rahisi kujua nini kitatokea kesho kulingana na utabiri wa kampuni husika.Mathalani,utabiri unasema kesho mvua itanyesha,kunauwezekano wa 25% wa mvua kesho kunyesha na kuna uwezekano wa 75% wa mvua kutokunyesha.So what do you do,unasikiliza utabiri kisha unajua ya kwamba yote yaliyotabiriwa kuna uwezekano wa 75% wa kutokutokea.
Tofauti na kampuni B ambayo kuna uwezekano wa 45% wa kutokea na 55% ya kutokutokea yale yaliyotabiriwa hivyo uncertainity inakuwa kubwa kidogo na unashindwa uchukue lipi.
Sasa tujaribu kudadafua swali lapili kwani linashabihiana na hili.