Chenge ashikiliwa polisi kwa ajali ya gari iliyosababisha vifo


Mkuu, bajaji zinasajiliwa na hii inayohusika na ajali hii ni yenye namba T736 AXE ambayo inamilikiwa na Zuwena Feith. Polisi wamemtaka Zuwena ajisalimishe ili asaidie polisi hasa kuhusu dereva aliyetoroka baada ya ajali.

But who knows labda dereva ameambiwa akimbie au alikufa na wameficha ili kesi iwe rahisi kwa mheshimiwa. Kwa spidi waliyokuwa nayo wote wawili, siyo rahisi kwa dereva wa bajaji kutoka mzima na kuweza kukimbia.
 

Unajua ishu sio ku-crucify Chenge; Sheria za barabarani si anazijua, inawezekana ni kawaida yake kuendesha gari kwa speed kubwa huku akiwa amelewa. Kunywa pombe na kuendesha gari ni kusa tayari kwa sababu unahatarisha usalama wako na wa wengine. sasa hapa kisichoeleweka ni kitu gani???
 
Ha! So unafikiri hilo ni tatizo kwa Chenge! Like I said hii ni minor inconvenience kwake.

Mkuu hapa hatufuati majina kama angekuwa na hizo pesa si angekuwa na Valid Insurance
Kwa kifupi kulipia bima kumemshinda vinginevyo kama unataka kumtukana mimi simo
Najua utasema Mzembe au Mpumbavu waka sheria anazijua kinyume nyume
(Ikiwa insurance tuu tatizo jee kulipa libel compensation itakuwaje ? )
 

Kuna tofauti ya bima na road license
 
Kuna tofauti ya bima na road license
Nipe tofauti haraka maana naona tunababaishana ,mimi nasema gari iliyokuwa akiendesha ilikuwa na bima ambayo inamalizika tarehe 22/04/09 ,sasa nifahamishe road license ni kitu gani maana sijawahi kukisikia.Maana sijajua umezungumza kitu gani ?
 
Nipe tofauti haraka maana naona tunababaishana ,mimi nasema gari iliyokuwa akiendesha ilikuwa na bima ambayo inamalizika tarehe 22/04/09 ,sasa nifahamishe road license ni kitu gani maana sijawahi kukisikia.Maana sijajua umezungumza kitu gani ?

Ukiangalia vema kuna vibandiko (stickers 3) hapo kwenye windscreen
Ya kwanza ya square ni Road Licence ambayo ndo ina expire 22/4
Inayofuata ni insurance amabyo inaonyesha imekwisha expire tangia 6/6/2007
Ya chini kabisa ni sticker ya usalama barabarani
una jingine?
 
Nipe tofauti haraka maana naona tunababaishana ,mimi nasema gari iliyokuwa akiendesha ilikuwa na bima ambayo inamalizika tarehe 22/04/09 ,sasa nifahamishe road license ni kitu gani maana sijawahi kukisikia.Maana sijajua umezungumza kitu gani ?

Kazi kweli,Road Licence ni ile inayolipiwa kila mwaka TRA na insurance ni bima,vitu viwili tafauti.Huyu driver wa bajaj hajakimbia wala kupewa kitu apotee kwa kuwa kungekuwa na uwezekano wa habari hii kujulikana baadae mi nahisi atakuwa kanyamazishwa 'kenya style' na sitashangaa maiti kupatikana msituni baada ya muda.
 

Asafali umetumia lugha nyepesi zaidi kumuelimisha Mwiba. Thanx
 
Bado hamjanieleza tofauti yake kabsaa naona mna matatizo ya hukumu, Sasa Chenge aliendesha gari isiyokuwa na Bima au isiyokuwa na road licence,hilo ni suali ?Pengine mtaniambia panajieleza lakini nyinyi mnasemaje ?

kuna mtu kazidi kufahamisha kuwa road licence ni ile inayolipiwa kila mwaka ,sasa hajamalizia na Bima ni ipi ,mbali ya yote kwa upande wangu nizionavyo kwa mlivyozieleza zote zitakuwa ni bima ,lakini kwa mlivyoeleza ,nionavyo Bima haswa huwa ile ambayo inaonyesha kabila ya gari,aina ya gari kama ni basi au bajaji ,rangi ya gari,engene namba ya gari au Chasisi number ikiwa gari haina chasis nafikiri inawekwa engene namba,nguvu ya gari ,mahali ilikotengezwa ,nambari ya gari,kama gari ni ya binafsi,shirika au serikali,shirika liliyoidhamini gari ,muda ambao kwa gari kongwe huwa ni mwaka,aidha aina ya bima wenyewe kama ni first party au third part,kwa nchi zilizoendelea hawabandiki tena makaratasi ukutani wanakupa kipande chenye maalumati yote hayo sawa na ukurasa wa mwanzo wa pasi zetu za kusafiria .

Sasa kile kipande cha kati nafikiri ni ruhusa fulani ambayo pengine gari hiyo iliruhusiwa kwenda na kurudi Zanzibar kwa mwaka mmoja ,inakuwaje panakuwa na Zanzibar pale na halafu iwe Bima,wacheni kubambikiza.
 

hiyo ya ruhusa ya kwenda na kurudi zanzibar imenichekesha sana.

hivi hao waliogongwa na kufa wangekuwa watoto wake kamanda kova chenge angekuwa nje sasa?
 
But who knows labda dereva... alikufa... Kwa spidi waliyokuwa nayo wote wawili, siyo rahisi kwa dereva wa bajaji kutoka mzima na kuweza kukimbia.

Hata mimi wasiwasi huo umenijia. Ukiangalia impact ya ajali (kutokasna na gari la chenge linavyoonekana, ni vigumu kuamini kuwa abiria, waliokuwa wamekaa nyuma walikufa na dereva akaondoka, tena na nguvu za kukimbia
 

Mwiba wewe ni mbishi by nature. OK wewe unamiliki gari aina gani. Unaweza ukakuta tunajadiliana na mtu ambaye gari kwao mpaka ende mbunge ndo wanaliona.
Taka usitake huo ndo ukweli kuwa bima imekwisha! Full stooooooooooooooooop. Nenda ka grocery ka hapo jirani kapate kasoda kale ka mia 2 labda akili inaweza kufanya kazi kidogo. Pia ikielekea hapo grocery ukikuta gari lolote imepark hapo chungulia hapo kwenye kioo cha mbele ukirudi utatwambia umeona nini. C U baadaye
 
Saasa kutokana na maelezo yako nimekuuliza suali unipe tofauti, Road licenze inamalisikia mwaka mmoja ,na bima nayo je ,umetoka mkuku na makelele kibao.
Hapa lazima munipe maana ,sio mnapotosha ukweli ,ile ya kati sio bima ,pale mmevamia na mpiga picha ameenda ngowe na kupandisha watu mkenge. 😀

Au niwawekee sawa yale maandishi ya kati ili mjue kuwa Mheshimiwa gari yake ilikuwa na bima iliyo hai.Msione soo ?
 
Last edited:
mwizi ni mwizi na hatosheki....
hata insurance huna....
halafu kwa confidence zote unasema ulikua speed kati ya 80 -100 kmph kwenye maeneo ya makazi ya watu. hiyo ni speed kubwa sana kwenye maeneo ya watu.

huyu jamaa hana akili nina shindwa kueluewa hivyo vyeti vyake alivipataje
1. mara ya kwanza alivyoulizwa swali akajibu vijisenti
2. leo anatuambia alikua speed 80 -100 kwa confidence jamani huyu kweli ni
mwanasheria, ndio maana mikataba mingi ilikua mibovu chini yake
 
Naona mmekwama na mnafikiria mlivyopandishwa mkenge ,tatizo la gari sio kuwa halina bima bali tatizo gari haikusajiliwa,kwa maana hiyo gari haina kumbukumbu serikalini ,tokea iliposajiliwa mwaka 2006 na kumalizia 2007 .lakini inaonyesha alikuwa akiikatia Bima ,hapo hana kosa wakati yeye ni mtu mkubwa serikalini ,tunaweza kusema alikuwa halipi TRA ila akilipa Bima ,kwa ufupi akikwepa kodi na hakuna wa kumkamata ,hivyo utaona anarudia kule kule kwenye kutumia wazifa wake kukwepesha kodi. Take care ile ya kati ni Consignment Date 07/06/2006 hadi 06/06/2007 ada ya kulipa TRA ,sio Bima wandugu msikurupuke tu mtaumbuka baadae.natumai kuna watu wameshaliona hilo.Sijui wenye magazeti wanaoweka chambo kuuza magazeti yao.Nyie mliosema BIMA hivi TRA inashugulika na Bima ?

tabu wengine hapa wanakurupuka tu na kulaani kuwa hana ishuwarezi ,hata sijui kama wanafahamu maana yake ,basi watu wanasema na wao wanasema ,mtafungwa !
 
Naona tatizo ni dereva wa Bajaj yupo wapi ? Je alimalizwa kwa risasi ,pengine walikuwa wanafukuzana tokea walikotoka ,huwezi kujua !
 
Chenge alikuwa anatembea na huyo dada mmoja nini?
 
TWIST AND TURNS at every corner,what more will come out.sasa chenge anamjua marehemu mmojawapo-conspiracy or what,the press in tanzania must be having a field day
 
mmm...i think il agree with some people here that the middle sticker is the insurance tag ..and it expired in 07...that sticker has nothing to do with TRA...hence the words "commission of insurance tanzania" ...act of 1953 blah blah...
Kwenye Sticker ya insurance kuna
Veh No.
Make....Model...Color....
Commencement date (not consignment date)
Expiry date..06/06/2007
signature ya commissioner
then some numebr (policy i think
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…