Nemesis
JF-Expert Member
- Feb 13, 2008
- 5,517
- 4,477
Wakuu niulize kitu kimoja.. Hizi Bajaj huwa haziko registered?.. ina maana mtu akikimbia hawezi kutafutwa kwa njia yoyote kupitia vitambulisho vya mmliki wa Bajaj hiyo!...
Hakika nadhani sasa tuna kila sababu ya kuwa na vitambulisho maanake madereva wote siku hizi wakiua wanatoka mkuku tu na hawapatikani tena..Tukumbuke kifo cha Salome Mbatia..
Mkuu, bajaji zinasajiliwa na hii inayohusika na ajali hii ni yenye namba T736 AXE ambayo inamilikiwa na Zuwena Feith. Polisi wamemtaka Zuwena ajisalimishe ili asaidie polisi hasa kuhusu dereva aliyetoroka baada ya ajali.
But who knows labda dereva ameambiwa akimbie au alikufa na wameficha ili kesi iwe rahisi kwa mheshimiwa. Kwa spidi waliyokuwa nayo wote wawili, siyo rahisi kwa dereva wa bajaji kutoka mzima na kuweza kukimbia.